Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 14,047
- 20,411
*Anaandika Joseph Selasini Mbunge Wa Rombo (CHADEMA)*
Nilikuwa nasoma tu lakini neno hili limenifanya kuandika kitu.
Chama hiki ni cha kidemokrasia. Tunapata wapi msuli wa kudai demokrasia ndani ya nchi wakati tunaonyesha mkakati wa kuizuia ndani ya chama.
Mhe Mbowe kafanya mengi sana ni ikweli usioweza kujificha au kufichwa. Sasa ni wapi kwenye katiba yetu imeonyeshwa uchaguzi usifanyike au kiongozi aliefanya mengi mazuri na mvumilivu apite bila kupingwa?
Mhe Mwambe ni kiongozi wa chama. Mkiti wa kanda ya kusini, mjumbe wa kamati kuu na mbunge. Kweli ni tendo la kiniidhamu kumtukana kiasi hiki? Na je kumtukana kunatoa picha gani kwa walio nje ya mfumo wa Chadema?
Leo tuko na Mhe Mbowe na tunafikiri hakuna mwingine. Je hatuungi mkono hoja zote za CCM dhidi ya Mbowe? Nilidhani akipata wagombea wenzake hata wanne na akapita ataimarika zaidi na chama kitaonekana kuwa cha kidemokrasia na kuuwa kabisa hoja za kina Kibajaji na Msukuma?
Tunasema Magufuli anasigina katiba na sheria za nchi. Kwani katiba yetu si inamruhusi kila mwanachama kugombea nafasi yoyote ndani ya chama? Kama nimekosea naomba maelekezo.
Comments nyingi zinamchafua Mkiti Mbowe kwa kuwa hajatangaza kugombea na najua kwa sababu wakati na ratiba haijatoka na wanaomsemea hajawaomba kufanya hivyo isije kufahamika ana kundi maana kuwa na kundi kwa wakati huu kwa mujibu wa taratibu ni kuanza kampeni kabla ya muda na unaweza kuchukuliwa hatua.
Kuhusu kushika ilani mbona kile ni kitabu tu? Mbona Waislam wanashika biblia ni wakristu? Hata shati la kijani mbona wengi waliokuwa CCM wanayo? Mhe Bulaya, Mhe Sumaye na wengine hawana?
Naomba matusi haya pelekeni au elekezeni CCM sio wenyewe kwa wenyewe na nadhani hata wanachama wengine waje tu chama kitachangiwa pesa za kutosha kupitia fomu za kugombea nadhani ni mil 5 si haba.