Joseph Selasini: Tunapata wapi msuli wa kudai demokrasia ndani ya nchi wakati tunaonyesha mkakati wa kuizuia ndani ya chama?

Kiukweli ni hoja ya msingi sana.mwanachadema yeyote apewe ruksa ya kugombea cheo chochote ndani ya chama.watakaoamua ni wanachadema wenyewe nani awe kiongozi wao kupitia kura.
 
Takataka za Mbowe zitakuja hapa na kutetea kwamba bila Mbowe chadema itakufa!

Yani watanzania sasa mnapaswa kujua kwamba siku Mungu akimchukua Mbowe chadema hakuna.
Kama mnajua hivyo muueni basi!
 
Takataka za Mbowe zitakuja hapa na kutetea kwamba bila Mbowe chadema itakufa!

Yani watanzania sasa mnapaswa kujua kwamba siku Mungu akimchukua Mbowe chadema hakuna.
Aah kuna mtu huku anasema akiondoka kwenye uongozi..SGR,Ndege na Umeme hamna mtu wa kuviendeleza.
 
Eti Chama cha demokrasia na maendeleo-upuuzi !


Cecil Mwambe aliyetangaza Nia ya kugombea uenyekiti ili ashindane na Mbowe anatukanwa kama si Mbunge wao kule mitandaoni.


Baadhi yao 'wamtusio ' wamefikia hatua ya kumtusi yeye na familia yake kisa yeye kutangaza nia ile.


Mytake;Tuelezwe rasmi kama hicho chama ni cha kidkteta au la!
Kama akina Etwege,Barbosa wote wapo wanamtusi Mbunge wao
 
Unaona kilivyo chama chako
Chama changu kipi mpendwa wangu? Mie changu ni kile cha Hashimu Rungwe, nakuhakikishia mwakani tutashinda kwa kishindo. 2015 CCM "walitubia" kura zetu, ilikuwa mzee Rungwe ashinde kabisa
 
Tulisema kuwa CDM siku ikishika nchi, watakuwa wazalendo wa milele na wapigania haki wa milele, bora hata wenye utamaduni wa kijiti hao kijani mchicha. Blueband itumike kwa mkate tu
 
CDM huu ni mtihani naamini hamtataka tuwafikirie kuwa SHENZISTAN kunawafaa. Au na nyinyi ni kama wale wanaosema UTAMADUNI WETU hauruhusu mtu mwingine kutangaza nia? Wakisikia jina la Membe basi vichwa vinavurugwa. UTAWALA BORA hauwahusu CCM peke yao kila chama kinatakiwa kionyeshe mfano.
 
*Anaandika Joseph Selasini Mbunge Wa Rombo (CHADEMA)*


Nilikuwa nasoma tu lakini neno hili limenifanya kuandika kitu.

Chama hiki ni cha kidemokrasia. Tunapata wapi msuli wa kudai demokrasia ndani ya nchi wakati tunaonyesha mkakati wa kuizuia ndani ya chama.

Mhe Mbowe kafanya mengi sana ni ikweli usioweza kujificha au kufichwa. Sasa ni wapi kwenye katiba yetu imeonyeshwa uchaguzi usifanyike au kiongozi aliefanya mengi mazuri na mvumilivu apite bila kupingwa?

Mhe Mwambe ni kiongozi wa chama. Mkiti wa kanda ya kusini, mjumbe wa kamati kuu na mbunge. Kweli ni tendo la kiniidhamu kumtukana kiasi hiki? Na je kumtukana kunatoa picha gani kwa walio nje ya mfumo wa Chadema?

Leo tuko na Mhe Mbowe na tunafikiri hakuna mwingine. Je hatuungi mkono hoja zote za CCM dhidi ya Mbowe? Nilidhani akipata wagombea wenzake hata wanne na akapita ataimarika zaidi na chama kitaonekana kuwa cha kidemokrasia na kuuwa kabisa hoja za kina Kibajaji na Msukuma?

Tunasema Magufuli anasigina katiba na sheria za nchi. Kwani katiba yetu si inamruhusi kila mwanachama kugombea nafasi yoyote ndani ya chama? Kama nimekosea naomba maelekezo.

Comments nyingi zinamchafua Mkiti Mbowe kwa kuwa hajatangaza kugombea na najua kwa sababu wakati na ratiba haijatoka na wanaomsemea hajawaomba kufanya hivyo isije kufahamika ana kundi maana kuwa na kundi kwa wakati huu kwa mujibu wa taratibu ni kuanza kampeni kabla ya muda na unaweza kuchukuliwa hatua.

Kuhusu kushika ilani mbona kile ni kitabu tu? Mbona Waislam wanashika biblia ni wakristu? Hata shati la kijani mbona wengi waliokuwa CCM wanayo? Mhe Bulaya, Mhe Sumaye na wengine hawana?

Naomba matusi haya pelekeni au elekezeni CCM sio wenyewe kwa wenyewe na nadhani hata wanachama wengine waje tu chama kitachangiwa pesa za kutosha kupitia fomu za kugombea nadhani ni mil 5 si haba.
Millioni 5 kugombea uenyekiti wa chama!! Kweli life is expensive.
 
Na siku Mungu akimchukua Jiwe ujue CCM imekombolewa!!
Takataka za Mbowe zitakuja hapa na kutetea kwamba bila Mbowe chadema itakufa!

Yani watanzania sasa mnapaswa kujua kwamba siku Mungu akimchukua Mbowe chadema hakuna.
 
Mnaomtukana na nyie CCM, mnakuwa na ID mbili au tatu mnazitumia kutukana na kuchagiza mambo ya CDM.
Eti Chama cha demokrasia na maendeleo-upuuzi !


Cecil Mwambe aliyetangaza Nia ya kugombea uenyekiti ili ashindane na Mbowe anatukanwa kama si Mbunge wao kule mitandaoni.


Baadhi yao 'wamtusio ' wamefikia hatua ya kumtusi yeye na familia yake kisa yeye kutangaza nia ile.


Mytake;Tuelezwe rasmi kama hicho chama ni cha kidkteta au la!
 
Tatizo lenu mnachanganya Chadema na Tanzania.
Ujanja aliofanya mbowe kusigina katiba ya chama inayomweka madarakani kwa miaka 20 sasa ndo mbinu hizo hizo ccm wameanza maandalizi ili ikifika 2024 nyimbo za tano tena kwa jiwe zianze kuimbwa kwa masipika makubwa.
 
Back
Top Bottom