Joseph Selasini: Tunapata wapi msuli wa kudai demokrasia ndani ya nchi wakati tunaonyesha mkakati wa kuizuia ndani ya chama?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
13,657
19,763
*Anaandika Joseph Selasini Mbunge Wa Rombo (CHADEMA)*

Nilikuwa nasoma tu lakini neno hili limenifanya kuandika kitu.

Chama hiki ni cha kidemokrasia. Tunapata wapi msuli wa kudai demokrasia ndani ya nchi wakati tunaonyesha mkakati wa kuizuia ndani ya chama.

Mhe Mbowe kafanya mengi sana ni ikweli usioweza kujificha au kufichwa. Sasa ni wapi kwenye katiba yetu imeonyeshwa uchaguzi usifanyike au kiongozi aliefanya mengi mazuri na mvumilivu apite bila kupingwa?

Mhe Mwambe ni kiongozi wa chama. Mkiti wa kanda ya kusini, mjumbe wa kamati kuu na mbunge. Kweli ni tendo la kiniidhamu kumtukana kiasi hiki? Na je kumtukana kunatoa picha gani kwa walio nje ya mfumo wa Chadema?

Leo tuko na Mhe Mbowe na tunafikiri hakuna mwingine. Je hatuungi mkono hoja zote za CCM dhidi ya Mbowe? Nilidhani akipata wagombea wenzake hata wanne na akapita ataimarika zaidi na chama kitaonekana kuwa cha kidemokrasia na kuuwa kabisa hoja za kina Kibajaji na Msukuma?

Tunasema Magufuli anasigina katiba na sheria za nchi. Kwani katiba yetu si inamruhusi kila mwanachama kugombea nafasi yoyote ndani ya chama? Kama nimekosea naomba maelekezo.

Comments nyingi zinamchafua Mkiti Mbowe kwa kuwa hajatangaza kugombea na najua kwa sababu wakati na ratiba haijatoka na wanaomsemea hajawaomba kufanya hivyo isije kufahamika ana kundi maana kuwa na kundi kwa wakati huu kwa mujibu wa taratibu ni kuanza kampeni kabla ya muda na unaweza kuchukuliwa hatua.

Kuhusu kushika ilani mbona kile ni kitabu tu? Mbona Waislam wanashika biblia ni wakristu? Hata shati la kijani mbona wengi waliokuwa CCM wanayo? Mhe Bulaya, Mhe Sumaye na wengine hawana?

Naomba matusi haya pelekeni au elekezeni CCM sio wenyewe kwa wenyewe na nadhani hata wanachama wengine waje tu chama kitachangiwa pesa za kutosha kupitia fomu za kugombea nadhani ni mil 5 si haba.
 
Eti Chama cha demokrasia na maendeleo-upuuzi !

Cecil Mwambe aliyetangaza Nia ya kugombea uenyekiti ili ashindane na Mbowe anatukanwa kama si Mbunge wao kule mitandaoni.

Baadhi yao 'wamtusio ' wamefikia hatua ya kumtusi yeye na familia yake kisa yeye kutangaza nia ile.

Mytake;Tuelezwe rasmi kama hicho chama ni cha kidkteta au la!
 
Katoa maoni yake WAZI ndio demokrasia. Hakudukuliwa wala hatohitaji kwenda kuomba radhi kwa kutoa mawazo, mitizamo yake. Wengi mnaotumwa na Nyapara wa barabara ambae amefanikiwa kujenga uoga na unafiki huko Lumumba, mtakuja juta kwa aibu.
 
Sijawahi kuona chama HOVYO kama Chadema na kuna wakati kimezunguka nchi nzima ili wapewa dola. Hivi chama hiki chenye misingi mibovu ya utawala ndicho kinategemewa siku moja kikomboe watanzania?

Suala la uongozi ndani ya chama ni kizungumkuti. Kuna mtu aliniambia Chadema ni gende la wakora acha niamini nikae kusubiri chama chenye nia ya dhati kukomboa mtanzania.
 
Niemkuwa nikisema siku zote kuwa viongozi wengi wa upinzani ni waganga na wachumia tumbo. Na wengi walikimbikia upinzani baada ya kunyimwa nafasi za ulaji huko walikokuwa.

Mhe. Selesini unasema matusi yapelekwe CCM, kwanini? Nchii inahitaji siasa za kukosoana kistaarabu siyo kwa matusi. Kutukana ni kielelezo tosha cha kukosa akili na ustaarabu.

Kuweni mifano mema ya kile mnachokiamini na kukihubiri.

Tuanze kustaarabika sasa.
*Anaandika Joseph Selasini Mbunge Wa Rombo (CHADEMA)*

Nilikuwa nasoma tu lakini neno hili limenifanya kuandika kitu.

Chama hiki ni cha kidemokrasia. Tunapata wapi msuli wa kudai demokrasia ndani ya nchi wakati tunaonyesha mkakati wa kuizuia ndani ya chama.

Mhe Mbowe kafanya mengi sana ni ikweli usioweza kujificha au kufichwa. Sasa ni wapi kwenye katiba yetu imeonyeshwa uchaguzi usifanyike au kiongozi aliefanya mengi mazuri na mvumilivu apite bila kupingwa?

Mhe Mwambe ni kiongozi wa chama. Mkiti wa kanda ya kusini, mjumbe wa kamati kuu na mbunge. Kweli ni tendo la kiniidhamu kumtukana kiasi hiki? Na je kumtukana kunatoa picha gani kwa walio nje ya mfumo wa Chadema?

Leo tuko na Mhe Mbowe na tunafikiri hakuna mwingine. Je hatuungi mkono hoja zote za CCM dhidi ya Mbowe? Nilidhani akipata wagombea wenzake hata wanne na akapita ataimarika zaidi na chama kitaonekana kuwa cha kidemokrasia na kuuwa kabisa hoja za kina Kibajaji na Msukuma?

Tunasema Magufuli anasigina katiba na sheria za nchi. Kwani katiba yetu si inamruhusi kila mwanachama kugombea nafasi yoyote ndani ya chama? Kama nimekosea naomba maelekezo.

Comments nyingi zinamchafua Mkiti Mbowe kwa kuwa hajatangaza kugombea na najua kwa sababu wakati na ratiba haijatoka na wanaomsemea hajawaomba kufanya hivyo isije kufahamika ana kundi maana kuwa na kundi kwa wakati huu kwa mujibu wa taratibu ni kuanza kampeni kabla ya muda na unaweza kuchukuliwa hatua.

Kuhusu kushika ilani mbona kile ni kitabu tu? Mbona Waislam wanashika biblia ni wakristu? Hata shati la kijani mbona wengi waliokuwa CCM wanayo? Mhe Bulaya, Mhe Sumaye na wengine hawana?

Naomba matusi haya pelekeni au elekezeni CCM sio wenyewe kwa wenyewe na nadhani hata wanachama wengine waje tu chama kitachangiwa pesa za kutosha kupitia fomu za kugombea nadhani ni mil 5 si haba.
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom