Joseph Selasini: Tunapata wapi msuli wa kudai demokrasia ndani ya nchi wakati tunaonyesha mkakati wa kuizuia ndani ya chama?

.........Watanzania karibia wote wamelishwa unga wa ndele.

.......hawa wanasifu na kuabudu upande huu na hawa nao wanasifu na kuabudu upande wa pili.
 
Sijawahi kuona chama HOVYO kama Chadema na kuna wakati kimezunguka nchi nzima ili wapewa dola. Hivi chama hiki chenye misingi mibovu ya utawala ndicho kinategemewa siku moja kikomboe watanzania?

Suala la uongozi ndani ya chama ni kizungumkuti. Kuna mtu aliniambia Chadema ni gende la wakora acha niamini nikae kusubiri chama chenye nia ya dhati kukomboa mtanzania.
Anzisha chako tu roho yako isuuzike. Yanini uumizwe na vilivyoanzishwa na wengine? Waache na ukora wao kwani wewe una hasara gani?
 
Ni Kheri CDM mtu anaongea kama hivi, lakini haya ukiyasema Lumumba aisee hukawii kuanza kufuatwa na Noah Nyeusi..!! Kule ni kimya kimya na tai shingoni.
 
Mbowe ameifikisha juu Chadema lakini kwa mikono yake mwenyewe anaishusha. Kuongoza kidemokrisia siyo jambo dogo na si kweli kwamba kila kiongozi anaweza kufanya hivyo.
Tunalilia haki ya kusema na kufanya siasa kwa mh rais kumbe Sisi wenyewe tunawzuia wengine kugombea nafasi ambazo Katiba zetu zimewaruhusu!!
Ni aibu
 
Unaijuwa katiba ya CDM? Au unaimbishwa tu ? Watia huruma.
Ujanja aliofanya mbowe kusigina katiba ya chama inayomweka madarakani kwa miaka 20 sasa ndo mbinu hizo hizo ccm wameanza maandalizi ili ikifika 2024 nyimbo za tano tena kwa jiwe zianze kuimbwa kwa masipika makubwa.
 
JARIBU Kakosoe KWANZA HUKO kwenu hata kwa siri hukuishia kuomba radhi
Niemkuwa nikisema siku zote kuwa viongozi wengi wa upinzani ni waganga na wachumia tumbo. Na wengi walikimbikia upinzani baada ya kunyimwa nafasi za ulaji huko walikokuwa.

Mhe. Selesini unasema matusi yapelekwe CCM, kwanini? Nchii inahitaji siasa za kukosoana kistaarabu siyo kwa matusi. Kutukana ni kielelezo tosha cha kukosa akili na ustaarabu.

Kuweni mifano mema ya kile mnachokiamini na kukihubiri.

Tuanze kustaarabika sasa.
 
Mkuu;

Mimi ninamuheshimu sana Padri Selasini lakini amenishangaza aliposema matusi yapelekwe CCM!

Nadhani ameteleza katika hoja yake!
 
Unataka kuniambia Chadema uliianzisha wewe na genge lako?
Wewe anzisha chama chako roho yako isuuzike period. Au umelazimishwa na yeyote kuwa Chadema? Mbona vyama vipo vingi tu. Kuna CUF kuna ACT kuna CHaUMA kuna UPDP kuna TLP n.k. Kazi kupanua domo tu eti hutaki chama cha wakora. Waache na ukora wao umeitwa? By the way who are youuuuuuuuu?
 
😂😂😂😂😂😂😇😅 Selasini yamemfika shingoni, tukisema sisi wa CCM, kuwa Chadema ni saccos ya Mbowe tunajibiwa vibaya sana, sasa mambo hadharani.. Haaaaaaa.
 
Chama changu kipi mpendwa wangu? Mie changu ni kile cha Hashimu Rungwe, nakuhakikishia mwakani tutashinda kwa kishindo. 2015 CCM "walitubia" kura zetu, ilikuwa mzee Rungwe ashinde kabisa
Ha ha alisema waliompa pole ni wengi kuliko kura zake ,kwahiyo anamashaka aliibiwa
 
Tatizo lenu mnachanganya Chadema na Tanzania.
We ndo unachanganya mambo, chadema ilitakiwa ijenge confidence kwa wananchi kwa kuongoza chama kwa mfano, style ya kuongoza chama inaakisi pia mtakavyoongoza nchi mkishika madaraka sasa Kama mnasigina katiba ya chama mtashindwa kweli kusigana katiba ya nchi? Mbowe anaua heshima ya chama alichokijenga kwa jasho lake kabisa
 
.........Watanzania karibia wote wamelishwa unga wa ndele.

.......hawa wanasifu na kuabudu upande huu na hawa nao wanasifu na kuabudu upande wa pili.
Wanacheza GAME hawa..
Bahati ya kuona msajili kaja juu na wamepewa barua ionekana hata ndani ya chama chao walikuwa bado wana majadiliano kuhurusu demokrasia ichukue nafasi yake ..
Wanataka kuudanganya umma hata wao ndani ya CHAMA chao walikuwa kwenye democracy process hivyo barua imekuta tayari wako vizuri..
Hata huyo Mhe. Mwambe amepewa maelekezo kukamilisha GAMEPLAN yao kuonyesha kuna democracy..
Kumbe Karata 3
 
*Anaandika Joseph Selasini Mbunge Wa Rombo (CHADEMA)*

Nilikuwa nasoma tu lakini neno hili limenifanya kuandika kitu.

Chama hiki ni cha kidemokrasia. Tunapata wapi msuli wa kudai demokrasia ndani ya nchi wakati tunaonyesha mkakati wa kuizuia ndani ya chama.

Mhe Mbowe kafanya mengi sana ni ikweli usioweza kujificha au kufichwa. Sasa ni wapi kwenye katiba yetu imeonyeshwa uchaguzi usifanyike au kiongozi aliefanya mengi mazuri na mvumilivu apite bila kupingwa?

Mhe Mwambe ni kiongozi wa chama. Mkiti wa kanda ya kusini, mjumbe wa kamati kuu na mbunge. Kweli ni tendo la kiniidhamu kumtukana kiasi hiki? Na je kumtukana kunatoa picha gani kwa walio nje ya mfumo wa Chadema?

Leo tuko na Mhe Mbowe na tunafikiri hakuna mwingine. Je hatuungi mkono hoja zote za CCM dhidi ya Mbowe? Nilidhani akipata wagombea wenzake hata wanne na akapita ataimarika zaidi na chama kitaonekana kuwa cha kidemokrasia na kuuwa kabisa hoja za kina Kibajaji na Msukuma?

Tunasema Magufuli anasigina katiba na sheria za nchi. Kwani katiba yetu si inamruhusi kila mwanachama kugombea nafasi yoyote ndani ya chama? Kama nimekosea naomba maelekezo.

Comments nyingi zinamchafua Mkiti Mbowe kwa kuwa hajatangaza kugombea na najua kwa sababu wakati na ratiba haijatoka na wanaomsemea hajawaomba kufanya hivyo isije kufahamika ana kundi maana kuwa na kundi kwa wakati huu kwa mujibu wa taratibu ni kuanza kampeni kabla ya muda na unaweza kuchukuliwa hatua.

Kuhusu kushika ilani mbona kile ni kitabu tu? Mbona Waislam wanashika biblia ni wakristu? Hata shati la kijani mbona wengi waliokuwa CCM wanayo? Mhe Bulaya, Mhe Sumaye na wengine hawana?

Naomba matusi haya pelekeni au elekezeni CCM sio wenyewe kwa wenyewe na nadhani hata wanachama wengine waje tu chama kitachangiwa pesa za kutosha kupitia fomu za kugombea nadhani ni mil 5 si haba.

Mh. Selasini ana hoja ya msingi.

Chadema kimebebwa na neno demokrasia na maendeleo. Haiwezekani kwamba hakuna mtu mwingine mwenye uwezo, msimamo thabiti na mfia chama wa kuwa Mwenyekiti. Haiwezekani.

Chama kutokwenda kidemokrasia pia kuna athiri maendeleo ya chama chenyewe. Chama kufika kilipo sasa ni zao la demokrasia (walikuwepo akina mzee Mtei wakaondoka, mzee Makani wakaondoka), na kuja kwa Mbowe ni kwa sababu demokrasia ilifuata mkondo wake.

Sasa wapo wanaomini sasa siyo wakati sahihi kwa sababu za intelijinsia kuwa kuna wanaowinda kumuweka mamluki. Inawezekana. Lakini ni hoja hafifu sana kwani hakuna wakati wowote ule ambao hakujawahi kuwa na hii hatari. Kungekuwa na willingness, chama kingesha wa-screen na kuwaandaa members potential. Haiingii akilini kwamba hakuna mrithi sahihi. Utakua ni uzembe wa hali ya juu sana tena kwenye nyakati fragile kama hizi.
 
Jiwe jana kasema haoni mtu wa "kujenga madaraja, SGR na Stigla," hiv kweli hata kibajaj akipewa urais akaamua kubambikizia watu kesi alafu baadae akawaita mezani wajadiliane ili watoke atashindwa kujenga hayo madaraja na barabara?
 
Takataka za Mbowe zitakuja hapa na kutetea kwamba bila Mbowe chadema itakufa!

Yani watanzania sasa mnapaswa kujua kwamba siku Mungu akimchukua Mbowe chadema hakuna.
Hata mwewe akimchukua CHADEMA hakuana
 
Back
Top Bottom