Joseph Mbilinyi 'Sugu' amlipua Zitto Kabwe

Joseph Mbilinyi 'Sugu' amlipua Zitto Kabwe

[h=2][/h]
:blabla: Msanii Msanii Tu Hata Iweje atabaki Kuwa Msanii ...!




 
Prof Ngongo

Kabla haujatoa maamuzi ya kumuweka Zitto kwenye kundi la mafisadi ungevuta subra kiduchu usikie na upande wa pili wa Zitto.

Hawa wanasiasa wetu wengi wao ni maghumashi.

Ahsanta.

Naona siku hizi unajifanya mjanja wa JF, teh teh teh kauzu kweli wewe.

Katika mambo yanayo niudhi ni hili la wapinzani wao wenyewe kushambuliana badala ya kunoa mapanga kupambana na Liccm ninyi mnapambana wenyewe nini malengo yenu sasa

Hivi hizi Milioni mia ninyingi kuliko bil 200 zilizochotwa na viongozi wa serikali na chama kwanini msiunganishe nguvu kutusemea wanyonge ili mapesa haya yarudi kama zilivyorudi pesa za rada jamani upinzani nani kawaroga kiasi cha kuanza kuumbuana hadharani kiasi hiki??!!!!!!!

BACK TANGANYIKA

Hivi mnajua kama Zitto bado ni mwanachama wa chadema?
Kwa sasa huwezi kutenganisha 'ufisadi' wa Zitto na Chadema.

Wapiga kura ambao wengi sio wanachama wa JF wal wa Face book, kwasasa hawawezi kumtenganisha zitto na Chadema.
Hivyo mnavyomchafua Zitto, mnaichafua chadema.

Chadema ingehakikisha kwanza Zitto anaondolewa kabisa kwenye chama officialy kisha ndio waanze kumlipua.

Unawataka UKAWA wachangue uchafu wa kufagia, yaani watoe mchanga tu,vumbi waliache kisa?

Nilikuwa sifahamu kumbe TANAPA wanakopesha siku hizi???

Zile za makada wa Chama chenu yakiwemo mabilion ya Mzindakaya ya Guarantee Scheme mmesharejesha?

CHADEMA waache chuki binafsi za kumshambulia mtu kisa tu hataki kufuata mkumbo wao.

Ni sawa sawa tuu na kutoboa jahazi mlilopanda wote tena mpo katikati ya bahari.

Hatuichukii serikali ya CCM kwasababu tu kuna watu wanaiba fedha za umma au kujinufaisha na madaraka kwa kuhujumu uchumi la hasha, tunaichukia kwasababu haichukui hatua kuwawajibisha na kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria haki itendeke.

Vyama vya upinzani havina malaika au miungu vina binadamu ambao wasipobanwa na sheria wanaweza kuwa mbwa mwitu. Chadema inaonyesha wazi kila mwenye kukiuka maadili, na kushindwa kutekeleza kazi yake kwa mujibu wa sheria za nchi, kanuni, na taratibu ni mhalifu tu kama wahalifu wengine wote.

Hapa swala sio Zito tu hata akiwa nani ikionekana anatenda ndivyo sivyo atawajibishwa. Kelele tunazompigia JK ni kushindwa kuwawajibisha watu wake. Kila mwenye kosa lazima awajibishwe ikithibitika bila kujali chama, au wadhifa.

Hakuna chuki binafsi hapa, hoja ijibiwe kwa hoja. Je huu sio mgonngano wa kimasilahi? Kweli tutaweza kukagua Tanapa na NSSF?
 
Hivi mnajua kama Zitto bado ni mwanachama wa chadema?
Kwa sasa huwezi kutenganisha 'ufisadi' wa Zitto na Chadema.

Wapiga kura ambao wengi sio wanachama wa JF wal wa Face book, kwasasa hawawezi kumtenganisha zitto na Chadema.
Hivyo mnavyomchafua Zitto, mnaichafua chadema.

Chadema ingehakikisha kwanza Zitto anaondolewa kabisa kwenye chama officialy kisha ndio waanze kumlipua.

"Makalio ya sufuria hayaogopi moto"
 
Zitto ni fisadi papa! Amezoea kuishi kiujanja ujanja na hadaa kwa Watanzania. Kumbe ndo anapiga dili chafu hivi huyu mpuuzi! Ninahasira naye kwa hili alilolifanya huyu? Hapo tutarajie kilio cha kutafuta huruma kuwa nafuatwafuatwa wakati nipo ktk kipindi kigumu cha kuuguza mama mzazi! Pole kweli kwa kuuguza ila ktk hili sina huruma na wewe!
 
Wewe MSALANI kila kitu unatetea na we2 ni uko wa panya ameiba ameiba,wewe ninani? katika nchi hii.

Huwa ninamshangaa sana utafikiri si mtanzania mwenye uchungu na nchi yake. Huenda ni mtoto wa fisadi. Angekuwa mtoto wa mkulima kama mimi angesimama kidete kupinga ufisadi.
 
Mkuu Ruttashobolwa , Sugu ni kifaranga tu aliyetumwa kumshambulia Zitto. Namfananisha na kifaranga Lema alivyotumwa na Mengi kumtukana Prof.Muhongo.
 
Last edited by a moderator:
Ngoja Tusubilie majibu ya Zitto mwenyewe bila shaka atajibu kwa mda muafaka na kwa majibu mujalabu
uzuri wa Zitto akijibu huwa anaanza kwanza na mama Kifaranga halafu anamalizia kwa vifaranga
Sugu mwenyewe haaminiki maana aliwaacha kwenye mataa Vinega wenzake akaingia makubaliano na Ruge bila kuwashirikisha Vinega
 
No tender advised, no work done, and still Zitto Daft Kabwe cashed the money.
 
Hapa swala sio Zito tu hata akiwa nani ikionekana anatenda ndivyo sivyo atawajibishwa.

Sasa inakuwaje mbowe awajivishwi kwa kujipa tenda na kufanya biashara na chama???
Vipi slaa mbona naye anapeta tu wakati anajikopesha hela ya chama??
 
Mkuu MSALANI ukitaka kujivua ujinga shabikia wanasiasa wa nchii hii bahati nzuri mimi sina mahaba na wanasiasa nina mahaba ya nchi yangu Tanzania.
Huu ni uzushi wa CHADEMA tu, katika harakati za kumchafua Mh.Zitto.
 
Last edited by a moderator:
Wewe MSALANI kila kitu unatetea na we2 ni uko wa panya ameiba ameiba,wewe ninani? katika nchi hii.
Mkuu tunachopinga hapa ni uzushi wa CHADEMA. Kila mtu anafahamu Viongozi wa CHADEMA na Zitto haziivi ndio maana wanamtumia SUGU asiyejitambua kumshambulia.
 
Mkuu Ruttashobolwa , Sugu ni kifaranga tu aliyetumwa kumshambulia Zitto. Namfananisha na kifaranga Lema alivyotumwa na Mengi kumtukana Prof.Muhongo.

Mkuu MSALANI hilo tunalijua kuwa chadema wana watumia vijana wasio jua mambo kama sugu nawengine kumchafua zitto.
Katika hili ndio utaamini Chadema hawana uwezo wa kupambana na Zitto.
Lazima awaumbua naona wameanza kucheza na moto tena lazima watafutane.
 
Last edited by a moderator:
Katika wanasiasa niliokuwa nawakubali basi ni Zitto...Ata wakati wanaanza kumuanika nikajua ni siasa chafu wanamuonea......Nilikuja kuchoka nilipokaa na kina Linex wanamuziki members wa Leka Tugite waliponiambia namna alivyokuwa anawatumia wasanii kupiga pesa.....Yani jamaa walikuwa wanaongea kwa uchungu uwezi kuamini ni Zitto uyu uyu ... rip leka tugigite

Duh........:der:
 
Huwa ninamshangaa sana utafikiri si mtanzania mwenye uchungu na nchi yake. Huenda ni mtoto wa fisadi. Angekuwa mtoto wa mkulima kama mimi angesimama kidete kupinga ufisadi.
Nyie wapinga ufisadi mbona tukisema Mbowe alipe fedha za UMMA alizokopeshwa hamtaki? Na Mbowe anaonyesha kila dalili ya kutaka "kurusha" deni hilo?
 
ngoja tusubilie majibu ya zitto mwenyewe bila shaka atajibu kwa mda muafaka na kwa majibu mujalabu
uzuri wa zitto akijibu huwa anaanza kwanza na mama kifaranga halafu anamalizia kwa vifaranga
sugu mwenyewe haaminiki maana aliwaacha kwenye mataa vinega wenzake akaingia makubaliano na ruge bila kuwashirikisha vinega

mkuu subiri uone watakavyo tafutana
 
Back
Top Bottom