Jordan na Misri zimeonesha nguvu zao kushinda silaha zote za Marekani na Israel

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,204
10,952
Mafanikio makubwa yamepatikana siku ya Ijumaa ya juzi ikiwa umebaki muda mfupi wapalestina wa Gaza waanze kufa kwa njaa na kiu. Siku hiyo ilitanguliwa na kikao cha pamoja kati ya viongozi wa nchi za Jordan,Saudi Arabia na Umoja wa falme za kiarabu.

Ni siku hiyo hiyo ambayo katibu mkuu wa umoja wa mataifa,Antonie Guteres aliitembelea Misri na kujionea hali ya mpaka wa Rafah unaoitenganisha Misri na Gaza.

Kwa amri ya raisi Abde Fattah Elsisi maandamano yaliyodhibitiwa yaliitishwa kuelekea mpaka kwenye mpaka huo kusuhubiana na ziara ya katibu mkuu huyo wa umoja wa mataifa. Kitu kama hicho kilifanyika kwenye kizuizi cha mto Jordan unaotenganisha nchi ya Jordan na eneo la Jerusalem.

Watu wapatao 500 waliruhusiwa kuandamana mpaka eneo hilo na baadae kutawanywa ili wasivuke mto huo.Hata hivyo ujumbe wa maandamano madogo hayo ilikuwa ni ujumbe tosha kuwa Jordan inafungwa na mkataba waliouingia na Israel mwaka 1994.

Kinyume na hivyo wanao uwezo pia wa kuwaachia wapalestina wanaounda asilimia 80 ya raia wake kuvuka mpaka huo ambapo mabomu kutoka angani hayatowazuia kuingia mitaa ya Jerusalem na kuwaondoa walowezi wa kiyahudi kwenye ardhi zao.

Salamu hizo zilionekana kuifikia Israel kikamilifu kwani kinyume na hasira zao baada ya kupigwa kidogo na Hamas ambapo walisema wanaweka total blockade ili kuwamaliza Hamas,na ilionekana mwanzoni hawataki mjadala kuhusiana na hilo.

Matendo ya Jordan na Misri yalikuwa na maana ya kujibu jaribio la Israel kutaka kuwatoa watu wa Gaza ili kujimilikisha eneo hilo kitu ambacho wamekifanya maeneo mengi ya Palestina miaka yote ya mzozo huo.Hii ilikuwa na maana badala ya kuwatoa watu kutoka Gaza wao wangeruhusu wapalestina waingie ndani yao badala yake.

Mbinu kama hiyo ya kutumia jeshi la watu peku peku walilifanya kwa mafanikio nchi ya Morocco mwaka jana walipokuwa na mzozo na nchi ya Spain pale kwenye eneo la Melilla ambapo Morocco waliwafumbia macho wazamiaji kutoka mataifa ya Afrika wanaotaka kuingia Ulaya kupitia lango hilo.

1698039583153.png
 
wangekuwa na uwezo huo, wangeshawaachia kitambo.
Wamepeleka salamu kuwa iwapo hamtafungua mpaka na kuacha mashambulizi hiki tunaweza tukakifanya.Sio sisi tu tuheshimu mikataba inayolalamikiwa na watu wetu lakini nyinyi hamtaki kutuheshimu na sisi.
 
Mafanikio makubwa yamepatikana siku ya Ijumaa ya juzi ikiwa umebaki muda mfupi wapalestina wa Gaza waanze kufa kwa njaa na kiu. Siku hiyo ilitanguliwa na kikao cha pamoja kati ya viongozi wa nchi za Jordan,Saudi Arabia na Umoja wa falme za kiarabu.

Ni siku hiyo hiyo ambayo katibu mkuu wa umoja wa mataifa,Antonie Guteres aliitembelea Misri na kujionea hali ya mpaka wa Rafah unaoitenganisha Misri na Gaza.

Kwa amri ya raisi Abde Fattah Elsisi maandamano yaliyodhibitiwa yaliitishwa kuelekea mpaka kwenye mpaka huo kusuhubiana na ziara ya katibu mkuu huyo wa umoja wa mataifa. Kitu kama hicho kilifanyika kwenye kizuizi cha mto Jordan unaotenganisha nchi ya Jordan na eneo la Jerusalem.

Watu wapatao 500 waliruhusiwa kuandamana mpaka eneo hilo na baadae kutawanywa ili wasivuke mto huo.Hata hivyo ujumbe wa maandamano madogo hayo ilikuwa ni ujumbe tosha kuwa Jordan inafungwa na mkataba waliouingia na Israel mwaka 1994.

Kinyume na hivyo wanao uwezo pia wa kuwaachia wapalestina wanaounda asilimia 80 ya raia wake kuvuka mpaka huo ambapo mabomu kutoka angani hayatowazuia kuingia mitaa ya Jerusalem na kuwaondoa walowezi wa kiyahudi kwenye ardhi zao.

Salamu hizo zilionekana kuifikia Israel kikamilifu kwani kinyume na hasira zao baada ya kupigwa kidogo na Hamas ambapo walisema wanaweka total blockade ili kuwamaliza Hamas,na ilionekana mwanzoni hawataki mjadala kuhusiana na hilo.

Matendo ya Jordan na Misri yalikuwa na maana ya kujibu jaribio la Israel kutaka kuwatoa watu wa Gaza ili kujimilikisha eneo hilo kitu ambacho wamekifanya maeneo mengi ya Palestina miaka yote ya mzozo huo.Hii ilikuwa na maana badala ya kuwatoa watu kutoka Gaza wao wangeruhusu wapalestina waingie ndani yao badala yake.

Mbinu kama hiyo ya kutumia jeshi la watu peku peku walilifanya kwa mafanikio nchi ya Morocco mwaka jana walipokuwa na mzozo na nchi ya Spain pale kwenye eneo la Melilla ambapo Morocco waliwafumbia macho wazamiaji kutoka mataifa ya Afrika wanaotaka kuingia Ulaya kupitia lango hilo.

View attachment 2789954
Ndo maana wakawa wanasheherekea?

View: https://youtube.com/shorts/j3PjJ6nhQGo?si=lI1AdaVxAHZNsh8O

Lucha
 
Back
Top Bottom