Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,183
- 10,913
Mashirika kadhaa ya misaada na wanasiasa wamezibeza juhudi za Marekani na ufalme wa Jordan za kudondosha vyakula kwenye jimbo la Gaza kama ni mchezo usiopendeza kipindi hiki watu wanakufa njaa jimboni humo.
Seneta wa Marekani,Jeff Merkley ameuambia utawala wa raisi Biden ikiwa kweli wamekusudia kusaidia matatizo ya watu wa Gaza basi lazima misaada ipelekwe kwa njia ya ardhini na baharini.Akaongeza kwa kusema misaada lazima iende kulingana na ukubwa wa mahitaji na aina ya mahitaji hayo.
Hapo jana katika vifurushi vichache vilivyodondoshwa jimboni humo vilikuwa havikujumuisha maji wala madawa ambavyo kwa hali ya Gaza ni vya lazima.
Ndege ya mizigo ya kijeshi ya C-130 ilidondosha vifurushi 38,000 tu na vyote vikiwa havina maji wala dawa.
Ndege moja ya aina hiyo ina uwezo wa kubeba uzito sawa na lori moja tu wakati mahitaji ya kawaida ya Gaza kwa siku moja ni malori 500.
Eneo ambalo hupendelewa kudondoshwa mahitaji hayo ni ukanda wa bahari ambapo wiki iliyopita misaada kama hiyo mingi ilidondokea baharini.Michache tu kati yao iliweza kupatikana na wavuvi ikiwa na vitu ambavyo havikuwa na thamani ya uzito wa plastiki uliotumika kuvihifadhi.