you guys..long time. Kuna kitabu nlikisoma nliazima library ya arusha mkoa, kinaitwa MBIO ZA JASUSI..dah kilikua nooma. those days..
wote wamekufa na kazi zao zimekufa, Hamie Rajabu nae maskini
Yeah ni njama. sasa wakati anaelezea ford mustang gari mimi kijijini hata sijui linaonekanaje maana gari pekee tulikuwa tunaona ni isuzu injection za halmashauri ya wilaya zikileta walimu ama bwana mganga! sasa fikiri nilikuwa na amini ni gari sampli hiyo ndilo msichana kahongwa!!!!!Hivi mrembo Zabibu alikuwepo katika simulizi ya kitabu gani...? nadhani ni Njama kama sikosei (nisahihishwe tafadhali). Willy Gamba alipojibarizi naye...alimsifia sana na kumwambia "Yaani, wewe kweli ni mtamu kama zabibu"
Willy Gamba bana mara nyingi akiwa ndio kwanza yuko likizo akila raha na mrembo ndio anapigiwa simu ya kuitwa ghafla Dar! Hapo anajua kimeshanuka,akifika Dar anapokelewa na namba 4 wanaelekea hadi ofisini na kumkuta bosi mkuu amefura kwa hasira kuashiria hali ni tete na ile bosi kumuona tu anamuita "namba moja umefika?" na bosi wake anapomuita kwa namba badala ya jina lake la Willy Gamba ujue kuna jambo zito!!
RIP ELVIS MUSIBA.... Ulikuwa mtu mwingine kwenye uandishi na kutufanya tujisikie salama na kuipenda nchi yetu kwani enzi hizo tuliamini Willy Gamba yupo kweli hivyo hakuna atakayeiweza Tanzania.
Watabaki kuwa watu muhimu katika uandishi hapa duniani. Mungu awarehemu
msimsahau mzee Zahir Ally Zoro baba yake banana kwenya Mafia Mob
hapa unapoongea narudia 24hrs kwa mara ya sita!!!!
Ulikuwa unajisikiaje unapomuona mwenzako ameshika KUFA NA KUPONA, NJAMA, KIKOSI CHA KISASI, KIKOMO ama SALAMU TOKA KUZIMU, TUTARUDI NA ROHO ZETU?, LAZIMA UFE JORAM, MIKONONI MWA NUNDA, NAJISIKIA KUUA TENA!!!HEBU KUMBUKA ULIPOKUWA UNASUBURI ZAMU YAKO NA WEWE UAZIME!!!
Nimeshangazwa kujua kwamba karibia kila mwandishi bora wa nyakati hizi amefariki. Nataka tuwakumbuke na kuwaombea. Lakini ni lazima nimpongeze mwandishi bora wa nyakati hizi HUSSEIN TUWA. kwa kweli ni mkali sana hebu kwa wale wapenzi wa riwaya tutafute riwaya zake MKIMBIZI, UTATA WA 9/12 NA MDUNGUAJU
hiyo muvi uwa haichoshi, hata ukiangalia mara mia, hivi haikuendelea season 12? maana niliishia 11, kitu cha jack baur federal agent from ctu, ethan, madam president. ila tafuta nyingine ya kikorea IRIS nalo bonge 1 la muvi. wacha hao wazamani waadithiane kwa vitabu, sisi kwa muvi.
Mimi pia ni wazamani. Combination ya kutoka analog mpaka digital ni kali kuliko digital pekeyake. Mimi nimeanzia vitabu na hiyo IRIS nasubiri season 5. Kuna city hunter,Athena, swallow the sun na sasa namalizia A man called God hapa nasubiri wakorea watakuja na nini tena. Umeona kijana wa kidijitali?hiyo muvi uwa haichoshi, hata ukiangalia mara mia, hivi haikuendelea season 12? maana niliishia 11, kitu cha jack baur federal agent from ctu, ethan, madam president. ila tafuta nyingine ya kikorea IRIS nalo bonge 1 la muvi. wacha hao wazamani waadithiane kwa vitabu, sisi kwa muvi.
Huku wakichombeza kwa lugha ya kiitaliano
"cappi de tutti cappi" boss of the boss
"Cossa nostra"
Mimi pia ni wazamani. Combination ya kutoka analog mpaka digital ni kali kuliko digital pekeyake. Mimi nimeanzia vitabu na hiyo IRIS nasubiri season 5. Kuna city hunter,Athena, swallow the sun na sasa namalizia A man called God hapa nasubiri wakorea watakuja na nini tena. Umeona kijana wa kidijitali?