Joram Kihango vs Willy Gamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Joram Kihango vs Willy Gamba

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Bujibuji, Sep 23, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,186
  Trophy Points: 280
  Ulikuwa unavutiwa zaidi na yupi kati ya wakali hao?
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,186
  Trophy Points: 280
  Joram Kihango, yaani nikisoma kitabu kama SALAMU KUTOKA KUZIMU, nilikuwa nasisimka mwikli mzima, nywele zikinisimama na vipele kunitoka mwili mzima.
   
 3. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  WILLY GAMBA mkuu, sijui waandishi wa enzi zile wamepotelea wapi!
   
 4. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Nilivutiwa zaidi na Willy Gamba, yaani nilikuwa nikisoma hadithi zake nilikuwa najisikia mzalendo halisi na nilitamani niwe kama yeye yaani niwe tayari wakati wote kuipigania Afrika, nakumbuka harakati za WG katika vitabu kama NJAMA, HOFU, KK (KIKOSI CHA KISASI), na kile cha wizi wa almasi mwadui. Huwa najiuliza kama mzee Aristablus Elvis Musiba angeendelea kuandika vitabu hivi, sijui angeandika nini juu ya Willy Gamba na mapambano yake na wahujumu kama wa EPA na RICHMOND! yaani Willy Gamba alinifanya nivutiwe sana kusoma riwaya za upelelezi kama zile za mtunzi James Hadley Chase!
   
 5. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  umenikumbusha willy Gamba,alikua anafurahisha sana!
   
 6. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ninavyofahamu mimi willy Gamba hakuwa mwandishi wa vitabu vya hadithi isipokuwa ni jina lililotumiwa na mwandishi wa vitabu maarufu wakati huo ambaye sasa ni mfanyabiashara maarufu vilevile anayeitwa A.MUSIBA. Nakumbuka KITABU CHAKE CHENYE HADITHI YA KUSISIMUA YA KIPELELEZI KATIKA JIJILA KINSHASA ( KUFA NA KUPONA )cha A.MUSIBA aliyetumia jina la Wily Gamba Kama Muhusika mkuu.
   
 7. Mchizi

  Mchizi JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2010
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 677
  Likes Received: 848
  Trophy Points: 180
  Kwa kweli umenikumbusha mbali enzi hizo kusoma vitabu vya hadithi ilikuwa ni mojawapo ya starehe kama si kwenda cinema.Nimesoma karibu vitabu vyote vya willy gamba,kuanzia kikomo,kikosi cha kisasi,hofu,njama,tutarudi na roho zetu,na vile vile vya joram kiango kama najisikia kuua tena,pesa zako zinanuka,dar es salaam usiku na vingine.Naweza kusema kila mmoja alikuwa na uzuri wake ila pointi nyingi atachukua willy gamba ambaye alikuwa anacheza kama mtu wa usalama wa taifa tofauti na joram kiango ambaye alikuwa anacheza kama mpelelezi wa kujitegemea.
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Joram Kiango malaika wa Shetani..lakini wote kwa ujumla Riwaya zao zilikuwa nzuri sana .
  Hivi mbona sasa hazipatikani?anayejua zunzuzwa waoi tafadhari tuwasiliane

  Zawadi ya ushindi mtunzi alikuwa nani nimesahau?
   
 9. A

  Akiri JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,447
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  du nilivutiwa sana na willy gamba hasa vitabu vya njama na kikosi cha kisasi. na mwandishi wa hivi vitabu yupo hapa mikocheni naona kajikita zaidi kwenye biashara zake. naona aliamua kuajipumzisha na fasihi andishi kwa heshima. yaani ameacha kuandika huku jamii ikiwa bado inapenda kazi zake. anaitwa mzee elivis musiba kwa sasa ni mwenyekiti wa CTI but sina hakika kama bado anaendelea au muda wake umeisha
   
 10. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  FL1 umekumbusha mbali kidogo na Mambo ya Sikamona! Mtunzi wa kitabu hiki ni Ben R. Mtobwa ambaye ndiye aliyekuwa anaandika Riwaya za Kusisimua za Joram Kiango. Nilipokuwa nasoma hizi riwaya nilikuwa nafanya imagination kumhusu Joram Kiango! Nilikuwa napata picha eti ni kweli Joram Kiango ni mtu kweli, Mwembamba, Mrefu amenyoa panki Ha ha ha
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,186
  Trophy Points: 280
  Kuna haja ya kuzitafuta hizi riwaya na kuziweka kwenye mtandao, maana hata kwenye book shops za hapa mjini vitabu hivyo havipatikani.
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Tena Musiba aliandika vitabu vyote hivyo kipindi alichokuwa anatumikia kifungo kirefu jela. Baada ya kifungo, alirudi uraiani, biashara imemchanganyia uandishi ndio basi tena.
   
 13. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu hapo kwenye red muhusika mkuu hakuwa Willy Gamba alikuwa Joram Kiango
   
 14. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #14
  Sep 23, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,186
  Trophy Points: 280
  Kumbe jamaa alitupwa lupango, nini ilikuwa sababu hasa ya kifungo hicho kirefu?
   
 15. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama anaitwa Joram KIHANGO......................... Mimi mkali wangu ni Ben R. Mtobwa na baadhi ya vitabu vyake ni Dar es salaam usiku, tutarudi na roho zetu, hiba ya wivu, najisikia kuua tena,zawadi ya ushindi, kipofu mwenye miwani mweusi,malaika wa shetani, roho ya paka, salamu kutoka kuzimu, mwalimu mwenye mkono wa bandia, nyuma ya pazia na bila kusahau, Kikwete:Safari ya Ikulu.....

  RIP Ben
   
 16. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Na mtunzi alikuwa Ben R Mtobwa jamaa ukisoma riwaya zake utadhani unaangalia senema.
   
 17. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #17
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,753
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Enzi za Nyerere, sometime hata bila sababu, mtu anakunywa mvua nyingi tuu hata bila sababu ya msingi. Hata mimi Mzee wangu ni mhanga wa enzi hizo na walikuwa wote huko.
   
 19. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #19
  Sep 23, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  WILLY GAMBA alikuwa kiboko.
   
 20. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #20
  Sep 23, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Mtunzi wa Vitabu hivyo (vinavyomhusu Willy Gamba) anaitwa, ARISTABLUS ELVIS MUSIBA

  Huyo Elvis Musiba nadhani ni baba yake mzazi na Aristablus, mwenye kuwafahamu vizuri watu hawa naomba atujuze tafzali.
   
Loading...