Tendwa anasema vyama vya siasa vijadiliane na polisi? Wajadailine nini? Utamwambia nini mtu anayetaka kukuuwa, don't kill me?
Katika mazingira ya utawala bora, mtu akikumbwa na tatizo la kiusalama anakimbilia polisi, lakini kwa Tanzania kwa sasa wakiona polisi wanapatwa na hofu! Ukisikia ndugu yako kakamatwa na polisi unaanza kufikiria 'gharama' za mazishi. Daudi Mwangosi amekufa huku akiwa amezungukwa na mapolisi si chini ya 6! Leo Tendwa anataka watu wakae chini wajadiliane nini na hawa polisi? Hakuna sheria nchi hii?