John Shibuda na mgogoro wa Kauli ya kuisifia CCM; Kauli za wana CHADEMA

Chadema wanamlea sana. Wahangaike na wanaccm halafu wahainge na shibuda?
Naamini CHADEMA wako radhi kumfukuza, ila hata wakimwondoa kupitia vikao halali vya chama; itaishia kuwa kama issue za akina Kafulira na Hamad Rashid. Haitaleta tija.
 
Mtu wa Pwani, asubirie utawala wa CCM uridhie officially hoja ya mgombea binafsi 2015; ili kufahamu iwapo Wanamaswa walimchagua kwa utashi wa CCM, Chadema au yeye binafsi kama Shibuda!!

Mbona hoja iko wazi?. Shibuda katamka wazi kuwa haoni chama kingine zaidi ya CCM kinachoweza kushika uongozi wa Taifa. Ina maana hata ateuliwa na CDM kugombea uraisi hakusudii kuishinda CCM bali kuisaiharakishia ushindi kwa kuuhujumu CDM. Nia pekee ni kujijengea umaarufu binafsi. Kimsingi Shibuda kajivua mwenyewe uanachama.
 
Last edited by a moderator:
Mpaka hapa nadhani sababu za kumfukuza Shibuda ziko wazi

@ Kukidharirisha chama
@ kuwadharirisha viongozi
@ kuvunja katiba ya chama
@ Kutishia kukiangusha chama.

Hizi sababu ukizichambua kwa ubongo ulio timamu zinatosha kumuondoa Shibuda!! Asituletee ulimbukeni wake!!

Please cabinet ya chama tuondoleeni huyu Gamba kungali mapema asijetuvuruga baadae!!
 
kosa la shibuda ni lipi..??? kutangaza nia...?! ndio mwataka afukuzwe uanachama ..?! je kuna mtu CDM wameshapanga aje kugombea..!?


ooh no; tatizo siyo kutangaza nia. Sidhani kama hilo ni tatizo. Soma vizuri utaona tatizo hasa nini. Uzuri ni kuwa utaona wana CCM ndio wanamtetea Shibuda na mambo yake kwamba asionewe. Adui yako anapomtetea msaliti wako na wewe ukimsikiliza atakucheka!
 
Chadema wanamlea sana. Wahangaike na wanaccm halafu wahainge na shibuda?

...Mkuu Mkjj niliwahi kuandika hapa kwamba huyu Shibuda ni pandikizi la magamba ndani ya CDM ili kujaribu kukisambaratisha chama hicho na pia wengi waliandika kwamba huyu afukuzwe mara moja lakini wakamdekeza, labda sasa ndiyo kaanza kazi yake rasmi ya kuongea pumba zake dhidi ya CDM. Natumai Viongozi wa juu wa CDM watatoa tamko hivi karibuni kuhusu huyu mganga njaa...kama kumfukuza CDM kutasababisha kupoteza jimbo ni bora iwe hivyo mara milioni kuliko kuendelea kumlea/kumdekeza huyu adui mkubwa wa CDM.
 
Tuliosoma shule za kata tunasema -senkiyu veri mach! Ila iwe hivyo mpaka milele.
 
We are fed up with him, Shibuda alikuja cdm kwa kazi maalumu na sasa ndo ameanza kutekeleza kazi iliyomleta chadema, Hivi mnakumbuka nguvu za NCCR Mageuzi zilipoteaje? Ni katika kulea virusi kama hivi.
Chama kilimuokota shibuda kwenye jalala la kisiasa kikampa nafasi ya ugombea ubunge, akashinda na hivi ndo anavyokidhalilisha kichaka kilichomhifadhi? Kweli Kurumbizi ni ndege asiye na shukrani.
My take: Viongozi wa cdm taifa twhitaji kusikia kauli yenu juu ya huu upuuzi wa huyu jamaa, failure ya kumwajibisha huyu kurumbizi itazalisha vibuda wengine ndani ya chama na mwisho malengo ya chama yatakuwa ni ndoto isiyotekelezeka tena, Mh Mbowe ulipopewa chama kama Mwenyekiti ulikuja udsm 2005 ukiwa na vision nzuri ya kujenga chama kupitia vijana na hakika tukakuunga mkono, wataka niambia kuwa kile ulichopambana kukijenga kwa miaka yote hii unaacha kiathiriwe na kirusi kinachoweza kuteketezwa as soon as possible, please think abt it kwa faida ya chama chetu.
 
Huyu Shibuda asifukuzwe wala nini, aachwe tu hivyovyo. Atajifukuza mwenyewe au tuseme kaisha jifukuza. Huyu ata-expire tu believe or not. We undhani wananchi wanajali kauli zake...? Ndo kwanza anaendelea kupoteza mvuto hadi atachuja. Kwa mtazamo wangu kupitia jicho la 3, Shibuda anakiimarisha CDM on backgroud. We need the likes of Shibuda and so, to keep going. Mwacheni abwabwaje tu huku tukisonga mbele, yeye atainekana kama katumwa na maganba kusambaratisha magwanda, na Kwa njia hiyo watu eataendelea kuwachukia magamba huku nyota ikingara Kwa magwanda... Muhimu nikumpa kile aonacho siri huku siri yenyewe iko chini ya kapeti.
 
Shibuda afukuzwe hana jipya, najua hatakua na siri yoyote zaidi ya kubwabwaja na ukanda na ukabile vitu ambavyo vimekua ni wimbo usio na ukweli wowote, plz uongoz wa juu cdm fukuza hili gamba.
 
Mtu wa Pwani, asubirie utawala wa CCM uridhie officially hoja ya mgombea binafsi 2015; ili kufahamu iwapo Wanamaswa walimchagua kwa utashi wa CCM, Chadema au yeye binafsi kama Shibuda!!

Hata afanyeje,shibuda is no Presidential material. Sasa asubiri mikakati ya kung'olewa Cdm at any price. Yeye ni gamba. Ameprove failure ndani ya magamba,asituletee upuuzi wake huku
 
Last edited by a moderator:
Chadema wanamlea sana. Wahangaike na wanaccm halafu wahainge na shibuda?

Mzee mwanakijiji Shibuda ni mwana CCM ndio maana anahudhuria vikao vya NEC na CC ya CCM na kutangaza nia ya kugombea urais ndani ya vikao hivo na kumuomba mwenyekiti wa ccm ampigie kampeni?pia anasema hakuna chama kinaweza kushinda urais ila ccm ukifanya simple correlation analysis unapata jibu gani hapo??
 
kiukweli uongozi wa CDM wanapaswa kumfukuza huyu mbunge.Amekidhalilisha cham,hafai kuwa mwanaCDM huyu.
 
Huyu Shibuda ni sawa na Mrema alivyoiua NCCR then TLP...ni mpinzani wa wapinzani
na Danson Kaijage, Dodoma

MBUNGE wa Maswa Magharibu, John Shibuda (CHADEMA), ametishia kutoboa kile alichokiita siri za chama hicho kwa madai kuwa ameishazijua zote.

Aidha Shibuda amemtaka Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA), John Heche, amwombe radhi ndani ya siku tatu tangu leo (jana) kutokana na kauli za kumdhalilisha katika vyombo vya habari juu ya kutangaza nia yake ya kugombea urais 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, mbunge huyo alidai kuwa iwapo BAVICHA hawatamwomba radhi ndani ya siku tatu atatoa siri kubwa za vijana hao zilizofichika nyuma ya pazia.

“Niliingia CHADEMA ili kuelewa mfumo na kanuni za chama, sasa nimeisha zijua siri zao hivyo naweza kufanya jambo kwa wananchi wangu na Watanzania kwa ujumla. Lazima Heche anieleze ni kwa nini ametoa matamko katika vyomba vya habari ambayo yanalenga kunidhalilisha kwa wapiga kura wangu,” alisema.


“Sijui kama ni kauli ya vijana au yake mwenyewe na kama Heche ni kiongozi au mlinda masilahi ya viongozi ndani ya chama wenye fikra za ugandamizaji na ukabila ndani ya chama.”


Alisema kuwa mwenyekiti huyo anatakiwa kueleza anaendesha baraza hilo kwa mawazo ya wajumbe au anatumia cheo chake vibaya kwa lengo la kulida maslahi ya watu ambao ni wachache wenye fikra hasi.


“Kwani kuna nini mimi Msukuma wa watu nikigombea urais au hao Bavicha wana siri gani na wanamtaka nani awe Rais?” alisema na kudai anatangaza rasmi kwamba atagombea nafasi hiyo na kama atapitishwa na CHADEMA, atamteua Dk. Slaa kuwa meneja wake wa kampeni.


Mbunge huyo alidai kuwa hawezi kutoka CHADEMA, badala yake atapambana na kukabiliana na changamoto zote ndani ya chama hicho.


“Mimi sihami ndani ya chama lakini kama chama kitanikataa basi nitapeleka mashtaka yangu kwa wananchi ili niweze kuwaeleza kile kilichojificha nyuma ya pazia kwa Watanzania.


“Nilitoka CCM kwa lengo la kukataa kunyanyaswa; nikategemea kuwa huku hakuna mambo kama hayo, hivyo hata huku siwezi kukubali kuburuzwa kwa ajili ya maslahi ya watu wengine, na niliishamwambia Dk. Slaa kuwa siwezi kuburuzwa na kukubali dhuluma kwa ajili ya watu wachache badala ya kuwatetea Watanzania,” alisema.


Alidai kushangazwa na kauli ya Heche kutaka afukuzwe, akihoji itasaidia kuongeza matawi mangapi ya CHADEMA nchini, akidai alikataa kukubali fikra hasi hata alipokuwa CCM, hivyo hatakubali kufungwa mdomo kwa ajili ya watu wenye dhuluma, na wanaoendekeza ukabila na ukanda ndani ya chama.


Aidha alisema alipoulizwa ni kwa nini amekuwa akipingana na viongozi wenzake kwa mambo mengi, na hivyo kuzua migogoro, alisema hana mgogoro wowote ndani ya chama na kutaka kama ipo iwekwe wazi.
 
eti ametishia kutoa siri za chama, cdm hatuuz unga, pmb za tembo wala magendo ya aina ya yoyote, kaz yetu kulinda maslai ya umma, huyu hana siri yoyote fukuza huyu mchumia tumbo. After miez michache atakue amesaulika.
 
Tunyoshe maelezo, kiukweli most of us CHADEMA tunamtaka Dr SLAA agombee upresident 2015, hatuna matatizo na Dr huyu! Huyu kirusi Shibuda nani atamchagua au kumpendekeza ndani ya Cdm?? Mimi naishi mbeya Ileje huku, yeye huo ukanda na ukabila anautoa wapi? Hatukutaki shibuda, endelewa hivyo! Kafilie mbali usitusumbue, tuache tuendelee kupambana na adui mmoja tu CCM!
 
jaman mbona ni kawaida yao kujisahau hata ndgu yake katika kazi ya kuua vyama pinzani mze wa inji hii alitangaza nia ya ubunge vunja akiwa kwenye mkutano wa nec pale dodoma.
 
Hivi Shibuda ameoa?
Mwanaume alieshaoa anaweza kurudishwa mkoleni? Manake haya mambo ya kutoa siri za ulipo hata kwenye unyago tunakatazwa!
 
Shibuda ana deserve kufukuzwa toka Chadema.
Bora awe mbunge wa mahakama kuliko kuendelea kubaki Chadema huku akiendelea kukidhalilisha chama na viongozi wake.
 
Back
Top Bottom