John Shibuda na mgogoro wa Kauli ya kuisifia CCM; Kauli za wana CHADEMA

Uhuru wa maoni na demokrasia huru ni sawa, lakini hata uhuru na demokrasia hiyo pia ina mipaka yake. Shibuda amesha itumia demokrasia na uhuru wake vibaya, anapaswa kuwajibishwa.

Viongozi wa chadema wameshiriki kukijenga chama kwa nguvu lakini haohao wanashiriki kulea nyufa kwa nguvunguvu hizohizo walizo tumia kukijenga chama. Kuendelea kumlea Shibuda kunatokana mapenzi ya kumuacha achafue chama na kuongeza nyufa.

Mimi naona chadema ni sawa na mwenye nyumba anae ziba mashimo ya panya wanao msumbua kwa vipande vya mikate. Dawa ni kuweka sumu ili watoweke kabisa!

Chadema inavyozidi kumlea shibuda ndio inavyozidi kuzalisha Vibuda.
 
eti ametishia kutoa siri za chama, cdm hatuuz unga, pmb za tembo wala magendo ya aina ya yoyote, kaz yetu kulinda maslai ya umma, huyu hana siri yoyote fukuza huyu mchumia tumbo. After miez michache atakue amesaulika.
Wamwache tu hakuna anayejali kauli za gamba hili!
 
madiwani wasaliti wa chadema walishughulikiwa bila chama kutetereka.
Ni muda wa kumuondoa shibuda.
 
CDM siyo chama kinachopaswa kupewa dola,wamejaa ubaguzi,udini na ukabila.Mara elfu ccm waendelee kuongoza hata kama ni mafisadi,kuliko hawa wabaguzi watakao poteza amani ya nchi na kusababisha hata watu wakashindwa kwenda makazini,so msiishabikie cdm kwa kua bendera fata upepo.
 
Yani namchukia huyu mzee! mdomo wake siku zote umejaa maneno uropokaji,anakera sana.
 
Shibuda..... mpotezeeni.... hana nguvu politically...
Domo kaya anapiga kelele.... CDM kaeni kimya... Akiendelea PIGA CHINI FASTAAAA
 
ooh no; tatizo siyo kutangaza nia. Sidhani kama hilo ni tatizo. Soma vizuri utaona tatizo hasa nini. Uzuri ni kuwa utaona wana CCM ndio wanamtetea Shibuda na mambo yake kwamba asionewe. Adui yako anapomtetea msaliti wako na wewe ukimsikiliza atakucheka!
Kweli umesema vizuri sana mzee,ni kama lowassa anavyotetewaga na wapinzani wa ccm nw engine humu humu wakienda mbali zaidi kwa kudai hakuna mgombea bora wa urais ccm kama lowassa!yani wanaomteteaga lowassa humu ndani wengi ni cdm
 
CDM huyu shibuda ni mpuuzi hadi anatia hasira, wala huyu si wa kuachiwa kijinga jinga hivi eti anasema atatoa siri za chama! Gosh......, BAVICHA hakuna kumwomba msamaha mpaka tuone hizo siri anazodai atazitoa.

SHORT LIVE SHIBUDA.
 
Mpaka sasa hivi sijajua kwa nini Heche anataka Shibuda afukuzwe chama...kumbe ndani ya Chadema ni kosa la jinai ukitangaza nia ya kugombea urais, tumeona kwa Zitto, leo tena tumeona kwa Shibuda.
 
Mimi mwana cdm kutoka kagera-karagwe kwa wale wanaosema kuwa CHADEMA ni ya ukanda niwaongo tu. Kwetu hatulali mpaka kieleweke kamati kuu tunaomba mtupilie mbali Chibuda hana lolote la kututishia ktk chama haondoke zake huyo kibaraka wa ccm tu, bora tumefahamu nia yake mapema. Viva dr Slaa.
 
Hapa inabidi viongozi wa CHADEMA wapate fundisho.Hata hawa kina Milya wanaojifanya kondoo,itafika mahali watageuka mbwa mwitu na kuteketeza ng'ombe,kondoo na mbuzi wote zizini.Hizi kauli za Shibuda zinadhihirisha jinsi alivyo egemea upande mwingine wa shilingi. Viongozi wa chama wawe makini.
 
Huyu Shibuda nahisi ni mzigo mpaka kwa familia yake!kifupi ni K.J, hv kwa akili zake anafikiria kuna Mtanzania gani mpenda mageuzi na mpenda maendeleo atakaemuamini tena mtu ****** kama yeye?eti linajifanya mtetea maslahi ya Watanzania,labda anatetea tumbo lake,mkewe na watoto wake!!CDM please muondoeni huyu mtu haraka iwezekanavyo,hathari za huyu mtu kubaki ndani ya chama ni kubwa kuliko kwenda kupga porojo zake akiwa nje ya chama!ni bora aendelee kua mbunge wa Maswa kupitia mahakama kuu,na naamini hii ndio safari yake ya mwisho kisiasa!
 
Back
Top Bottom