John Shibuda na mgogoro wa Kauli ya kuisifia CCM; Kauli za wana CHADEMA

SHIBUDA ana siri nzito sana ataisema muda ukifika.
CDM kuwa makini sana, kasi yenu inaelekea kupunguzwa sasa.
 
Shibuda, ana uelewa kiasi gani wa siasa za nyakati hizi zinavyokwenda? Au sababu ya kukaa sana Zanzibar akaanza kupractise urais kabisa?
 
Bavicha musimpe credit za kisiasa anazotafuta,hana lolote amejiona alivyochuja kama mchuzi usio na nyanya,nyie itisheni kikao pelekeni mapendekezo kwenye chama chenu endeleeni na vua Gamba vaa gwanda hiyo mbinu imekuwa set na usalama wa taifa na CCM kunuetralise ukweli kwamba serikali imefirisika hilo limewauma sana ,pia nguvu ya wana CCM wanavyohamia Chadema mumeshamuumbua inatosha ngojeni baada ya siku tatu aseme anachotaka kusema hana popularity yeyote hata huko Maswa

APRM mbona hajawahi kutoa taarifa kwa general public wala Chadema kwa nini taarifa akaitolee kwa CC ya CCM,alialikwa au alijialika na kama alijialika kwa nini
Mad man mwacheni amejikaanga
 
CHADEMA nao wanatakiwa kuwafunda kina Heche. Shibuda hatakiwi kuwa engaged kwenye majukwaa ya siasa. Wamwache afanye analotaka kufanya. Shibuda yupo kwenye suicide mission aliyotumwa na CCM, yaani kujilipua ili aondoke na credibility ya CDM. Njia pekee ya kushinda mission hiyo ni kumwacha Shibuda abwabwaje na 2015 akiomba kugombea jimbo la maswa kwa ticket ya CDM wampatie nafasi vilevile, kama akisema arudia kuvaa gamba basi wamwache.
CDM wakianza kufuata jinsi Shibuda alivyoenda rogue na kutaka kumdhibiti, itakuwa ni furaha kwa CCM. CCM waliisha mwita huyu jamaa na kumtaka radhi kwa kumtosa 2010 na kumuahidi makubwa kama atawasaidi kuiingiza CDM katika migogoro. Ukweli ni kwamba Shibuda hawezi kuiingiza CDM kwenye migogoro kwani si kiongozi hivyo ni wa kumpuuza tu. Mheshimiwa kamanda Mbowe tumia busara zako kwenye hili waambie CDM na vijana wote kuwa Shibuda ni mtu huru wamwache aongee anavyojisikia na wala wasimjibu. CDM you are winning the battle against CCM msikubali kuondolewa mawazo yenu kwenye trigger kwa kupitishiwa binti asiyekuwa na nguo.

Hofstede...Ninakubaliana na wewe, kabisa mission yake ya kuivuruga CDM (hataweza kamwe) imeshindikana, sasa anatafuta njia ya nguvu kuwachanganya CDM (ambao wanatakiwa kutulia na kumsoma njia zake), ila nashauri wala wasimfukuze ila kitaeleweka 2015, ila nashauri CDM ianze kuandaa kada mwingine kwa ajili ya kuteuliwa kugombea kwenye Jimbo lake
 
na Danson Kaijage, Dodoma

MBUNGE wa Maswa Magharibu, John Shibuda (CHADEMA), ametishia kutoboa kile alichokiita siri za chama hicho kwa madai kuwa ameishazijua zote.

Aidha Shibuda amemtaka Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA), John Heche, amwombe radhi ndani ya siku tatu tangu leo (jana) kutokana na kauli za kumdhalilisha katika vyombo vya habari juu ya kutangaza nia yake ya kugombea urais 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, mbunge huyo alidai kuwa iwapo BAVICHA hawatamwomba radhi ndani ya siku tatu atatoa siri kubwa za vijana hao zilizofichika nyuma ya pazia.

"Niliingia CHADEMA ili kuelewa mfumo na kanuni za chama, sasa nimeisha zijua siri zao hivyo naweza kufanya jambo kwa wananchi wangu na Watanzania kwa ujumla. Lazima Heche anieleze ni kwa nini ametoa matamko katika vyomba vya habari ambayo yanalenga kunidhalilisha kwa wapiga kura wangu," alisema.


"Sijui kama ni kauli ya vijana au yake mwenyewe na kama Heche ni kiongozi au mlinda masilahi ya viongozi ndani ya chama wenye fikra za ugandamizaji na ukabila ndani ya chama."


Alisema kuwa mwenyekiti huyo anatakiwa kueleza anaendesha baraza hilo kwa mawazo ya wajumbe au anatumia cheo chake vibaya kwa lengo la kulida maslahi ya watu ambao ni wachache wenye fikra hasi.


"Kwani kuna nini mimi Msukuma wa watu nikigombea urais au hao Bavicha wana siri gani na wanamtaka nani awe Rais?" alisema na kudai anatangaza rasmi kwamba atagombea nafasi hiyo na kama atapitishwa na CHADEMA, atamteua Dk. Slaa kuwa meneja wake wa kampeni.


Mbunge huyo alidai kuwa hawezi kutoka CHADEMA, badala yake atapambana na kukabiliana na changamoto zote ndani ya chama hicho.


"Mimi sihami ndani ya chama lakini kama chama kitanikataa basi nitapeleka mashtaka yangu kwa wananchi ili niweze kuwaeleza kile kilichojificha nyuma ya pazia kwa Watanzania.


"Nilitoka CCM kwa lengo la kukataa kunyanyaswa; nikategemea kuwa huku hakuna mambo kama hayo, hivyo hata huku siwezi kukubali kuburuzwa kwa ajili ya maslahi ya watu wengine, na niliishamwambia Dk. Slaa kuwa siwezi kuburuzwa na kukubali dhuluma kwa ajili ya watu wachache badala ya kuwatetea Watanzania," alisema.


Alidai kushangazwa na kauli ya Heche kutaka afukuzwe, akihoji itasaidia kuongeza matawi mangapi ya CHADEMA nchini, akidai alikataa kukubali fikra hasi hata alipokuwa CCM, hivyo hatakubali kufungwa mdomo kwa ajili ya watu wenye dhuluma, na wanaoendekeza ukabila na ukanda ndani ya chama.


Aidha alisema alipoulizwa ni kwa nini amekuwa akipingana na viongozi wenzake kwa mambo mengi, na hivyo kuzua migogoro, alisema hana mgogoro wowote ndani ya chama na kutaka kama ipo iwekwe wazi.
 
Huyu Jamaa ataipa shida CHADEMA he's 2 faces; Chadema itabidi watumie hekima ya hali ya juu kumzimisha huyu

Shibunda kwasababu anawatishia sasa, kwa kujua siri za Chama.
 
Chadema huyu mtu si wa kumfanyia masihara ni kumtafutia timing na kumfukuza tu ni bora kupoteza mbunge mmoja kama shibuda kuliko kuendelea kumwacha ndani ya chama. Amekuja kwa shughuli maalumu na anataka kuikamilisha ni bora kumtimua hasiaribu mambo huko mbele ya safari
 
kosa la shibuda ni lipi..??? kutangaza nia...?! ndio mwataka afukuzwe uanachama ..?! je kuna mtu CDM wameshapanga aje kugombea..!?
 
Chadema wanamlea sana. Wahangaike na wanaccm halafu wahainge na shibuda?

Mwanakijiji mbona umekuja na jibu la mkato? Tuelezeni kuna agenda gani ya siri kwenye uraisi ndani ya Chadema? Mlianza kumtuhumu Zitto; basi kila atakayesema azma yake kuwania uraisi ni msaliti?

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Kwa kweli inaonekana watu hawajamfahamu Shibuda vizuri, au wana ajenda zao za siri kama anavyohisi. Chadema kinasimamia Demokrasia ya kujieleza na kusema unachokiamini alimradi huvunji sheria za chama. Kutangaza nia kuwa anautaka urais ni haki ya kila mwana Chadema, cha msingi mwisho kila mtaka kugombea urais atapa

Suala ni kufata taratibu za chama na chama kitachagua nani awe mgombea wake. Awe Zitto, Lema, Dr Slaa au mwenginewe. Chadema msiwe kama vyama vingine kuwa na umungu mtu ndani ya chama.
 
unajua kuzungumza bila ya kuonesha wapi amekosea ni ujinga, kutangaza nia ndio kosa ?jee amevunja sheria za chadema ? au kosa kutangaza nia kwenye kamati yaCCM,? au kumuomba JK awe kampeni manager wake?(kitu ambacho hakihitaji elimu hata ndogo kuamini kuwa ni utani wa kisiasa baina ya JK na Shivuda ambaye hata alipokuwa CCM aliwahi kusema JK ni mtani wake)

inaonekana Shibuda kagundua udhaifu wa CHADEMA, kuwa si watu wenye kufata taratibu za chama na ndio anawachachafya, na inakuwa tabu kumshughulikia maana anafata taratibu na sheria na anachokisema japo huwa kichungu kwa wengine lkn kwa vile anajua sheria zikoje zinampa kiburi cha kujiamini. kwa hio cha msingi wanachadema kufata misingi ya chama chao na kuheshimu uhuru wa kujieleza
 
Kwa kweli inaonekana watu hawajamfahamu Shibuda vizuri, au wana ajenda zao za siri kama anavyohisi. Chadema kinasimamia Demokrasia ya kujieleza na kusema unachokiamini alimradi huvunji sheria za chama. Kutangaza nia kuwa anautaka urais ni haki ya kila mwana Chadema, cha msingi mwisho kila mtaka kugombea urais atapa

Suala ni kufata taratibu za chama na chama kitachagua nani awe mgombea wake. Awe Zitto, Lema, Dr Slaa au mwenginewe. Chadema msiwe kama vyama vingine kuwa na umungu mtu ndani ya chama.
Mtu wa Pwani, asubirie utawala wa CCM uridhie officially hoja ya mgombea binafsi 2015; ili kufahamu iwapo Wanamaswa walimchagua kwa utashi wa CCM, Chadema au yeye binafsi kama Shibuda!!
 
Last edited by a moderator:
Shibuda anapotosha umma kwa sababu yeye hajatumia taratibu za kichama kutangaza nia yake, kila chama kina taratibu zake, ktk tamko lile Mh. Heche amemshutumu huyu kwa kukiuka kanuni siyo usukuma wake. Huyu mzee ameonyesha udhaifu kwa kupotosha umma.

Pia mara Slaa mara Kikwete hatujui jibu ni lipi sasa. Kanuni zipo hata ktk ngazi ya familia. Mfano: Uwoya alienda kutangaza ktk media hampendi wala hajawai kumpenda Ndikumana, endapo Ndiku angemkemea angesema anamnyanyasa sababu ya uanamke wake au upumbavu wake? Hayo ni mambo ya family angepaswa kwenda kwa wazazi kueleza matatizo yake na siyo media za udaku, japo mfano haufanani ila mantiki ipo sawa, wale madiwani wa arusha walikua wasukuma?

Ktk Africa tunaamini ktk jambo lolote linalotaka busara basi wazee ndio kisima cha hekima na busara ila kama wazee wenyewe ndo hawa na kina mkapa na wassira basi wakizalisha vijana kama lusinde tusishangae, mi nilijua tuna ombwe la uongozi tu kumbe hata ombwe la wazee.
 
Huyu afukuzwe tu.Asilete usukuma kama kigezo cha kuvuruga chama.

Hata mimi ni Msukuma na 2015 naingia mjengoni kwa M4C ila natamka wazi kuwa SHIBUDA AFUKUZWE CDM HATUFAI. Arudi hukohuko CCM kwa vibaraka wenzie
 
Shibuda anapotosha umma kwa sababu yeye hajatumia taratibu za kichama kutangaza nia yake, kila chama kina taratibu zake, ktk tamko lile Mh. Heche amemshutumu huyu kwa kukiuka kanuni siyo usukuma wake. Huyu mzee ameonyesha udhaifu kwa kupotosha umma.

Pia mara Slaa mara Kikwete hatujui jibu ni lipi sasa. Kanuni zipo hata ktk ngazi ya familia. Mfano: Uwoya alienda kutangaza ktk media hampendi wala hajawai kumpenda Ndikumana, endapo Ndiku angemkemea angesema anamnyanyasa sababu ya uanamke wake au upumbavu wake? Hayo ni mambo ya family angepaswa kwenda kwa wazazi kueleza matatizo yake na siyo media za udaku, japo mfano haufanani ila mantiki ipo sawa, wale madiwani wa arusha walikua wasukuma?

Ktk Africa tunaamini ktk jambo lolote linalotaka busara basi wazee ndio kisima cha hekima na busara ila kama wazee wenyewe ndo hawa na kina mkapa na wassira basi wakizalisha vijana kama lusinde tusishangae, mi nilijua tuna ombwe la uongozi tu kumbe hata ombwe la wazee.
chadema wana vikao vyao, kama wanaona kweli SHIBUDA kakosea wamwite wamjadili na wamsikilize, ila kwa wanavyoenda ni rahisi kuamini kuwa kuna watu wamejiandaa kumuonea na kumzika kisiasa kwa njia za uonevu
 
kosa la shibuda ni lipi..??? kutangaza nia...?! ndio mwataka afukuzwe uanachama ..?! je kuna mtu CDM wameshapanga aje kugombea..!?
Sion kosa Shibuda kutangaza nia, lakini bado najiuliza, 1)kwanini alitangaza nia kupitia jukwaa la ccm huku akisisitiza jk ampigie debe ilhali akitarajia udhamini wa cdm?. 2)Hata kama Bavicha wamemkosea, kwanini atishie kutangaza siri za chama?. Anavoonekana, nikama vile anasubiri spark ndogo tu ili atimize lengo lake. Cdm must handle him with care, togather with other "Vibudas"
 
Back
Top Bottom