PreGE2025 John Mrema avuliwa uanachama wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia Tawi lake la Bonyokwa mkoani Dar es Salaam, kimemvua rasmi uanachama, John Mrema, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu, dharau kwa mamlaka halali za chama, na kukaidi misingi na maadili ya chama.

Kwa mujibu wa barua rasmi iliyoandikwa na kusainiwa Aprili 30, 2025 na Katibu wa Tawi, Solomini Kagaruki, ambayo Jambo TV tumepata kuiona, na ambayo ilitolewa na tawi hilo, Kamati Tendaji ya tawi hilo ilikutana Aprili 29, 2025 na kupitia tuhuma dhidi ya Mrema, kisha kufikia uamuzi wa pamoja wa kumvua uanachama wake kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006, toleo la 2019, ibara ya 5.4.3.

Miongoni mwa tuhuma zilizomkabili Mrema, aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho, ni pamoja na dharau dhidi ya mamlaka za chama ambapo imeelezwa kuwa alisambaza barua ya wito ya kufika mbele ya kamati ya nidhamu kwenye mitandao ya kijamii badala ya kuitikia kwa utaratibu wa chama, jambo lililotafsiriwa kuwa ni dharau kwa mamlaka husika.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Tuhuma nyingine ni kukaidi maadili na misingi ya chama, ikielezwa kuwa akiwa bado katika mchakato wa kujieleza, alifanya mkutano na waandishi wa habari Aprili 22, 2025 na kutoa tuhuma hadharani dhidi ya chama chake, akibeza misimamo na programu za CHADEMA kinyume cha utaratibu wa ndani wa chama.

Barua hiyo imeeleza kuwa, kutokana na mienendo hiyo, Mrema amepoteza sifa za kuendelea kuwa mwanachama wa CHADEMA kuanzia tarehe 30 Aprili, 2025. Hata hivyo, amepewa haki ya kukata rufaa kwa ngazi ya juu endapo hataridhika na uamuzi huo.

View attachment 3320871

Source: Jambo TV
Kuna watu wanapenda sana vyeo. Huyu jamaa tangu apoteze nafasi yake amekuwa mwendawazimu!
 
Kwamba aliehoji uteuzi wa rais kuwa mgombea hakufukuzwa uanachama? Mbona ccm walifanaya the same?
Kwahiyo unakubali madikteta wa chadema na majizi ya Ccm tofauti yenu hamna madaraka tu ila tabia zilezile
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia Tawi lake la Bonyokwa mkoani Dar es Salaam, kimemvua rasmi uanachama, John Mrema, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu, dharau kwa mamlaka halali za chama, na kukaidi misingi na maadili ya chama.

Kwa mujibu wa barua rasmi iliyoandikwa na kusainiwa Aprili 30, 2025 na Katibu wa Tawi, Solomini Kagaruki, ambayo Jambo TV tumepata kuiona, na ambayo ilitolewa na tawi hilo, Kamati Tendaji ya tawi hilo ilikutana Aprili 29, 2025 na kupitia tuhuma dhidi ya Mrema, kisha kufikia uamuzi wa pamoja wa kumvua uanachama wake kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006, toleo la 2019, ibara ya 5.4.3.

Miongoni mwa tuhuma zilizomkabili Mrema, aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho, ni pamoja na dharau dhidi ya mamlaka za chama ambapo imeelezwa kuwa alisambaza barua ya wito ya kufika mbele ya kamati ya nidhamu kwenye mitandao ya kijamii badala ya kuitikia kwa utaratibu wa chama, jambo lililotafsiriwa kuwa ni dharau kwa mamlaka husika.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Tuhuma nyingine ni kukaidi maadili na misingi ya chama, ikielezwa kuwa akiwa bado katika mchakato wa kujieleza, alifanya mkutano na waandishi wa habari Aprili 22, 2025 na kutoa tuhuma hadharani dhidi ya chama chake, akibeza misimamo na programu za CHADEMA kinyume cha utaratibu wa ndani wa chama.

Barua hiyo imeeleza kuwa, kutokana na mienendo hiyo, Mrema amepoteza sifa za kuendelea kuwa mwanachama wa CHADEMA kuanzia tarehe 30 Aprili, 2025. Hata hivyo, amepewa haki ya kukata rufaa kwa ngazi ya juu endapo hataridhika na uamuzi huo.

View attachment 3320871

Source: Jambo TV
Acha nyumbu wazikane wanyewe
 
Chadema ni wabaguzi, wabinafsi na wachoyo... Chama cha hovyo kuwahi kutokea. Sasa wanamalizana wenyewe kwa wenyewe..
 
cHADEMA ASILIA hatukubali. hakyanani Patachimbika! Mrema kalelewa na Mhe. Mbowe tangu ujana wake anakitumikia chama hadi anazeekea kwenye chama?!
Subirini, JOhn Henche, John Mnyika na Lissu wameamua kuwaondoa kanda ya kaskazini.
Ameshaiva kisiasa sasa mpaka ndani ya chama anataka kufungua chama chake wacha akafanye manuver huko
 
Ile ahadi aliyopewa inamtaka agombee kupitia CDM ili waliomtuma kazi yao waifanye vizuri.

Automatically anakuwa liability kwa wale jamaa waliomtuma, next move ya wale jamaa ni Mrema ajitoe ufahamu akubali kuwa juha ili akomae kubaki CDM na kukataa hayo maamuzi na kifuatacho ni kuleta mgogoro ambao hauwezi kuwa na madhara.

Pole sana Mrema ndio shida ukiamua kufanya kazi ya shetani, maana shetani anakugeuka chapu ukiwa huna faida, Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ndio angekuwa muaminifu kwako maana hata tukitenda dhambi bado anatusamehe na kuwa upande wetu na hata katikati ya dhambi hutulinda pia.
 
Hiki ndio chama cha demokrasia?
Kafutwa uanachama na kikao halali cha chama, tena cha tawi lake la mtaani...na bado ananafasi kukata rufaa vikao vya juu.
Maccm hamnaga hizo ni mwenyekt anakuja na kikaratasi mfukoni!
 
Back
Top Bottom