PreGE2025 John Mrema avuliwa uanachama wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia Tawi lake la Bonyokwa mkoani Dar es Salaam, kimemvua rasmi uanachama, John Mrema, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu, dharau kwa mamlaka halali za chama, na kukaidi misingi na maadili ya chama.

Kwa mujibu wa barua rasmi iliyoandikwa na kusainiwa Aprili 30, 2025 na Katibu wa Tawi, Solomini Kagaruki, ambayo Jambo TV tumepata kuiona, na ambayo ilitolewa na tawi hilo, Kamati Tendaji ya tawi hilo ilikutana Aprili 29, 2025 na kupitia tuhuma dhidi ya Mrema, kisha kufikia uamuzi wa pamoja wa kumvua uanachama wake kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006, toleo la 2019, ibara ya 5.4.3.

Miongoni mwa tuhuma zilizomkabili Mrema, aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho, ni pamoja na dharau dhidi ya mamlaka za chama ambapo imeelezwa kuwa alisambaza barua ya wito ya kufika mbele ya kamati ya nidhamu kwenye mitandao ya kijamii badala ya kuitikia kwa utaratibu wa chama, jambo lililotafsiriwa kuwa ni dharau kwa mamlaka husika.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Tuhuma nyingine ni kukaidi maadili na misingi ya chama, ikielezwa kuwa akiwa bado katika mchakato wa kujieleza, alifanya mkutano na waandishi wa habari Aprili 22, 2025 na kutoa tuhuma hadharani dhidi ya chama chake, akibeza misimamo na programu za CHADEMA kinyume cha utaratibu wa ndani wa chama.

Barua hiyo imeeleza kuwa, kutokana na mienendo hiyo, Mrema amepoteza sifa za kuendelea kuwa mwanachama wa CHADEMA kuanzia tarehe 30 Aprili, 2025. Hata hivyo, amepewa haki ya kukata rufaa kwa ngazi ya juu endapo hataridhika na uamuzi huo.

View attachment 3320871

Source: Jambo TV
That's how conflicts are resolved...

Akiona ameonewa, akate rufaa ngazi inayofuata...
 
cHADEMA ASILIA hatukubali. hakyanani Patachimbika! Mrema kalelewa na Mhe. Mbowe tangu ujana wake anakitumikia chama hadi anazeekea kwenye chama?!
Subirini, JOhn Henche, John Mnyika na Lissu wameamua kuwaondoa kanda ya kaskazini.
 
1746029902525.png
 
Hapa ndio tutajua wanafanyaga siasa kama kazi ( kuondoa njaa) au kuwatumikia watu
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia Tawi lake la Bonyokwa mkoani Dar es Salaam, kimemvua rasmi uanachama, John Mrema, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu, dharau kwa mamlaka halali za chama, na kukaidi misingi na maadili ya chama.

Kwa mujibu wa barua rasmi iliyoandikwa na kusainiwa Aprili 30, 2025 na Katibu wa Tawi, Solomini Kagaruki, ambayo Jambo TV tumepata kuiona, na ambayo ilitolewa na tawi hilo, Kamati Tendaji ya tawi hilo ilikutana Aprili 29, 2025 na kupitia tuhuma dhidi ya Mrema, kisha kufikia uamuzi wa pamoja wa kumvua uanachama wake kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006, toleo la 2019, ibara ya 5.4.3.

Miongoni mwa tuhuma zilizomkabili Mrema, aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho, ni pamoja na dharau dhidi ya mamlaka za chama ambapo imeelezwa kuwa alisambaza barua ya wito ya kufika mbele ya kamati ya nidhamu kwenye mitandao ya kijamii badala ya kuitikia kwa utaratibu wa chama, jambo lililotafsiriwa kuwa ni dharau kwa mamlaka husika.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Tuhuma nyingine ni kukaidi maadili na misingi ya chama, ikielezwa kuwa akiwa bado katika mchakato wa kujieleza, alifanya mkutano na waandishi wa habari Aprili 22, 2025 na kutoa tuhuma hadharani dhidi ya chama chake, akibeza misimamo na programu za CHADEMA kinyume cha utaratibu wa ndani wa chama.

Barua hiyo imeeleza kuwa, kutokana na mienendo hiyo, Mrema amepoteza sifa za kuendelea kuwa mwanachama wa CHADEMA kuanzia tarehe 30 Aprili, 2025. Hata hivyo, amepewa haki ya kukata rufaa kwa ngazi ya juu endapo hataridhika na uamuzi huo.

View attachment 3320871

Source: Jambo TV
 
Bado Catherine Ruge naona sasa hivi ameongeza kasi ya unyenyekevu katika mambo ya chama😏
 
Huku nje wanasisitiza uhuru wa kutoa maoni wakati ndani ya chama ni madikteta mtu akitoa maoni mbadala anafukuzwa chama, tukiwapa nchi tutaweza kuwakosoa kweli nyie madikteta uchwara?
This is rubbish.

Alichokuwa anafanya Mrema ni attack kwa chama, hayakuwa maoni.

Kama ni maoni, alivyoandika barua, angetulia kusubiria maamuzi ya mamlaka za chama.

Unaita wanahabari kushambulia mamlaka za chama, halafu ichukuriwe ni maoni mbadala? Waliitwa kwenye kikao halali cha watia nia ili wakatoe hoja zao,wakagoma.

Huyu kiuhalisia alikwishajivua uwanachama, na kuamua kuwa adui wa CHADEMA.

Hongereni sana kamati tendaji ya tawi lake kuchukua hatua
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia Tawi lake la Bonyokwa mkoani Dar es Salaam, kimemvua rasmi uanachama, John Mrema, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu, dharau kwa mamlaka halali za chama, na kukaidi misingi na maadili ya chama.

Kwa mujibu wa barua rasmi iliyoandikwa na kusainiwa Aprili 30, 2025 na Katibu wa Tawi, Solomini Kagaruki, ambayo Jambo TV tumepata kuiona, na ambayo ilitolewa na tawi hilo, Kamati Tendaji ya tawi hilo ilikutana Aprili 29, 2025 na kupitia tuhuma dhidi ya Mrema, kisha kufikia uamuzi wa pamoja wa kumvua uanachama wake kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006, toleo la 2019, ibara ya 5.4.3.

Miongoni mwa tuhuma zilizomkabili Mrema, aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho, ni pamoja na dharau dhidi ya mamlaka za chama ambapo imeelezwa kuwa alisambaza barua ya wito ya kufika mbele ya kamati ya nidhamu kwenye mitandao ya kijamii badala ya kuitikia kwa utaratibu wa chama, jambo lililotafsiriwa kuwa ni dharau kwa mamlaka husika.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Tuhuma nyingine ni kukaidi maadili na misingi ya chama, ikielezwa kuwa akiwa bado katika mchakato wa kujieleza, alifanya mkutano na waandishi wa habari Aprili 22, 2025 na kutoa tuhuma hadharani dhidi ya chama chake, akibeza misimamo na programu za CHADEMA kinyume cha utaratibu wa ndani wa chama.

Barua hiyo imeeleza kuwa, kutokana na mienendo hiyo, Mrema amepoteza sifa za kuendelea kuwa mwanachama wa CHADEMA kuanzia tarehe 30 Aprili, 2025. Hata hivyo, amepewa haki ya kukata rufaa kwa ngazi ya juu endapo hataridhika na uamuzi huo.

View attachment 3320871

Source: Jambo TV
Tokea baada ya matokeo ya uchaguzi wa uongozi mpya ndani ya CDM ilikwisha onyesha kamanda John Mrema alikitegemea sana chama kuendesha maisha yake ya kila siku kutokana na cheo alichokuwa nacho pale makao makuu. Ukichunguza vyema malalamiko anayoyatoa kila uchwao kwenda kwa uongozi wa sasa wa CDM utatambua dhahiri ya kuwa yeye ni mtu ambaye amekosa fursa aliyokuwa akiitegemea mno kutengeneza fedha zake binafsi.

Pia ukiangalia kwa jicho la tatu, utaona yeye ni aina ya mtu ambaye anataka kufaya "pre-emption" ili kuficha aibu yake ya kuondolewa katika sehemu aliyopiga fedha ndefu kwa muda mrefu. Anachokifanya hivi sasa ni kutafuta fursa mpya ya kupiga fedha dhidi ya uongozi wa sasa kupitia njia ya upinzani wa kificho akiwa ndani ya chama.

Anatambua kwa dhati kabisa jinsi uongozi uliopo unavyokubalika kwa wananchi waliokuwa wengi nchini kwa hivi sasa, pia anatambua mvuto waliokuwa nao viongozi waliopo pamoja na ajenda yao nzuri na yenye mashiko ya mabadiliko wanayoibeba. Ni dhahiri kabisa yeye na kundi lake wanatumika kama maadui waliopo ndani ya chama wakiungana na wale wa nje ili kutaka kudhoofisha mapambano ya kutaka mabadiliko yanayoendelea.

Si ajabu wao pamoja na baadhi ya viongozi fedhuli wa CCM na wa serikali pamoja na baadhi waliopo mahakamani, ndio ambao wanashirikiana na genge la maafisa wa vyombo vya dola ili kuendesha vitendo vya hujuma dhidi ya CDM kwa sasa. Si ajabu nyuma ya pazia anakutana na akina Mulilo ili kuleta drama ya kisiasa inayoendelea hivi sasa katika siasa ili kukipa unafuu chama tawala tuelekeapo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Manabii na wanajimu wamekwisha tabiri kuhusu hatima ya CCM tuelekeapo uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Wote wanatoa hitimisho moja,

MENE, MENE, TEKELI & PERESI (Rejea Danieli 5:25-28)

Ama kwa hakika NENO linakwenda kuthibitika,
MENE - Mungu ameuhesabu utawala wako batili na kuukomesha ....... X 2.
TEKELI - Utawala huu umepimwa katika mizani ya HAKI nao umeonekana kuwa umepungua.
PERESI - Utawala wao na umegawanyika, nao wanaenda kupewa wapinzani wa ndani na nje wa chama chao ili waje na utawala mpya na kuichukua nafasi yao.

Natambua kuanzi hivi sasa rangi yake halidi itaonekana. No Reforms No Election ni takwa la wakati. Na hakuna mtu ambaye ataweza kuzuia.. Time will tell, and Tundu Lissu will eventually have a tale to tell.
 
Saafi sana

Wote wenye urafiki na ccm hata wakipimwa akili, haziko sawa

Ni kawaida kwa yeyote yule akiwa ccm na au urafiki tu na ccm ama kula rushwa za duli, lazima akili haziwezi kuwa sawa
 
cHADEMA ASILIA hatukubali. hakyanani Patachimbika! Mrema kalelewa na Mhe. Mbowe tangu ujana wake anakitumikia chama hadi anazeekea kwenye chama?!
Subirini, JOhn Henche, John Mnyika na Lissu wameamua kuwaondoa kanda ya kaskazini.
Boya sana wewe, halafu mtafuteni kichaa wenu mmoja anajiita saigilomagema mumfundishe kujadiliana kwa hoja, mpumbavu sana yule trash!
 
This is rubbish.

Alichokuwa anafanya Mrema ni attack kwa chama, hayakuwa maoni.

Kama ni maoni, alivyoandika barua, angetulia kusubiria maamuzi ya mamlaka za chama.

Unaita wanahabari kushambulia mamlaka za chama, halafu ichukuriwe ni maoni mbadala? Waliitwa kwenye kikao halali cha watia nia ili wakatoe hoja zao,wakagoma.

Huyu kiuhalisia alikwishajivua uwanachama, na kuamua kuwa adui wa CHADEMA.

Hongereni sana kamati tendaji ya tawi lake kuchukua hatua

Ingekuwa jeshini angelambwa chuma! bahati yake ni kwenye chama.
 
Back
Top Bottom