PreGE2025 John Mrema avuliwa uanachama wa CHADEMA

PreGE2025 John Mrema avuliwa uanachama wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia Tawi lake la Bonyokwa mkoani Dar es Salaam, kimemvua rasmi uanachama, John Mrema, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu, dharau kwa mamlaka halali za chama, na kukaidi misingi na maadili ya chama.

Kwa mujibu wa barua rasmi iliyoandikwa na kusainiwa Aprili 30, 2025 na Katibu wa Tawi, Solomini Kagaruki, ambayo Jambo TV tumepata kuiona, na ambayo ilitolewa na tawi hilo, Kamati Tendaji ya tawi hilo ilikutana Aprili 29, 2025 na kupitia tuhuma dhidi ya Mrema, kisha kufikia uamuzi wa pamoja wa kumvua uanachama wake kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006, toleo la 2019, ibara ya 5.4.3.

Miongoni mwa tuhuma zilizomkabili Mrema, aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho, ni pamoja na dharau dhidi ya mamlaka za chama ambapo imeelezwa kuwa alisambaza barua ya wito ya kufika mbele ya kamati ya nidhamu kwenye mitandao ya kijamii badala ya kuitikia kwa utaratibu wa chama, jambo lililotafsiriwa kuwa ni dharau kwa mamlaka husika.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Tuhuma nyingine ni kukaidi maadili na misingi ya chama, ikielezwa kuwa akiwa bado katika mchakato wa kujieleza, alifanya mkutano na waandishi wa habari Aprili 22, 2025 na kutoa tuhuma hadharani dhidi ya chama chake, akibeza misimamo na programu za CHADEMA kinyume cha utaratibu wa ndani wa chama.

Barua hiyo imeeleza kuwa, kutokana na mienendo hiyo, Mrema amepoteza sifa za kuendelea kuwa mwanachama wa CHADEMA kuanzia tarehe 30 Aprili, 2025. Hata hivyo, amepewa haki ya kukata rufaa kwa ngazi ya juu endapo hataridhika na uamuzi huo.

View attachment 3320972

View attachment 3320871


Source: Jambo TV
Hili ni jambo jema sana. Binafsi ninataka wooooooote wavuliwe uwanachama abaki Lissu, Heche, Mnyika, Erythrocyte, Tindo na Lema tu! Hao wengine wote FUKUZA!

Peoplessssss, Power!!!!!!!
 
Huku nje wanasisitiza uhuru wa kutoa maoni wakati ndani ya chama ni madikteta mtu akitoa maoni mbadala anafukuzwa chama, tukiwapa nchi tutaweza kuwakosoa kweli nyie madikteta uchwara?
Umemsahau yule dokta aliyepinga namna samia alivyopitishwa kugombea urais alivyovuliwa uanachama huko kijani!
 
Sasa ajiunge na ccm anayoipigania , Sema sasa ukishatolewa Chadema na bei yako imeshuka
Wapi ameipigania CCM? Kuweni na aibu kidogo. Mna tofauti gani na CCM kama hamtaki uongozi wenu ukosolewe? Halafu mnajiita Chama cha Demokrasia na Maendeleo? Mnakoelekea sio kuzuri.

Amandla...
 
Umemsahau yule dokta aliyepinga namna samia alivyopitishwa kugombea urais alivyovuliwa uanachama huko kijani!
Ndio maana Chadema ilipaswa kujitofautisha na CCM. Kama ilivyofanya katika uchaguzi wao.

Amandla...
 
Huyu dogo hakujua hata kupiga hesabu vizuri. Alitakiwa aondoke mapema. Sasa kukaa kaa kachelewa kwa sasa soko lake limeshuka ataenda kukaa tu na akina lucas mwashambwa ambao ni prof arse lickers.
Hivi mnaamini kwa kumfukuza ndio mtamnyamazisha? Na kwa kudai kuwa ni CCM ndio atanyamaza? Wakati rufaa yake inasikilizwa ataendelea kuwakosoa. Mwisho wa siku mtathibitisha tu kuwa CDM imekuwa chama cha kidikteta uchwara.

Amandla...
 
Back
Top Bottom