John Mnyika: Sikuunga mkono Lowassa kuwa Mgombea wa Urais 2015 kupitia CHADEMA

Kumpokea Lowassa na kumpa Bendera aipeperushe ilikuwa ni Best Strategy na kama TUME ingekuwa ni HURU na sio hii ya KITAPELI CHADEMA ilikuwa iingie Ikulu.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amesema hakuunga mkono Hayati Edward Lowassa kuwa mgombea wa urais kwenye chama hicho, bali alitaka akijiunga CHADEMA awe mwanachama wa kawaida.

View attachment 2903024
Mbona hilo linafahamika maana ulisusa kwa karibu miaka minne. Ila nakupongeza ulijitahidi kukaa kimya kuepusha mgogoro na baadae ikarudi. Zaidi ya hapo licha ya kutakiwa CCM ukabaki CDM.
 
..Lowassa alizingua.

..Cdm hawakufanya utafiti wa kutosha kuhusu afya ya Lowassa, na kama anaweza kuhimili mikikimikiki ya kampeni.

..Lowassa alikuwa hawezi kukampeni.

..kura na hamasa kwa kampeni yake zilipungua kadiri muda ulivyokuwa unakwenda.
Kwa kigezo cha utafiti wa afya za wagombea vyama vyote vyenye ushawishi vingechana mikeka.
Kama CCM zile top 5 zote ndio kama ulivyoona.
 
..Lowassa alizingua.

..Cdm hawakufanya utafiti wa kutosha kuhusu afya ya Lowassa, na kama anaweza kuhimili mikikimikiki ya kampeni.

..Lowassa alikuwa hawezi kukampeni.

..kura na hamasa kwa kampeni yake zilipungua kadiri muda ulivyokuwa unakwenda.
Ila kura alizopata za Urais ziliweka rekodi ambayo hamkuitegemea na bado mlivuna wabunge wengi mno na hata kuongoza halmashauri kadhaa nchini.

Nyota ya Lowassa iliwanufaisha sana

Tindo zitto junior
 
Bora yeye aliendelea kubaki huko Chadema

Binafsi nafsi ilinisuta

Mtu tuliyeitangazia dunia kwamba, ni fisadi la mafisadi na hastahili popote, aje kuwa mgombea wetu? Nilishindwa kujaribu kulamba matapishi

Inaonesha ni jinsi gani mnavyoweza kula matapishi yenu.
 
Kwanini nisionekane ? iko hivi , kwenye jambo la wengi huamui tu utakavyo wewe , bali wengi wakisema ndio huwezi kukataa , utachagua kuwaunga mkono au kunyamaza , mimi nilimpinga mno Lowassa , lakini wengi walipomkubali ndani ya chama chetu , nikaamua kuwaunga mkono kwa Maslahi ya chama , huo ndio ukomavu
Lowassa aliletwa Chadema na Mbowe, iweje useme ni maamuzi ya watu wengi kwenye chama chako.?
 
Hakuwa na nguvu yakupambania kura zake maskini... hata huko CCM asingekuwepo wa kumkata Lowassa kama angekua ngangari vile.
Nafikiri Richmond haikumwacha Lowasa salama, shida zote za koafya hienda chimbuko lake ni Richmond
 
Kumpokea Lowassa na kumpa Bendera aipeperushe ilikuwa ni Best Strategy.
No. It was a fatal mistake!
1. Ilichafua taswira ya Chadema. Chama cha Upinzani kina Mgombea ana kashfa zaidi ya Mgombea wa Chama Tawala.

2. Lowasa alikosa sifa muhimu ya any genuine opposition candidate-MILITANT PERSON DHIDI YA DHULMA ZA CHAMA TAWALA. Hivi, kwenye mfumo ambao chama tawala ni wezi wa chaguzi, unawaambia wafuasi wako wakakae majumbani baada ya voting, halafu baada ya kuibiwa kura, huitishi public action. Hakuna wakati umma wa tanzania ulikua Umeiva kwa mabadiliko kama 2015. Mgombea wa upinzani, angekiwasha tu, nchi ingeitika, so CCM walihitaji Soft Inaction opposition candidate and yes, EL served the purpose.

3. Effect ya EL kurudi CCM, ili-demoralize wafuasi wa Upinzani hadi leo.

EL angeingia CDM na kuwa mfadhili, Silaa akasimama, nakuhakikishia JPM angekua Rais, lakini UKAWA wangejumuishwa kwenye Serikali.
 
Kajinga sana haka kajamaa.

Sasa inasaidia nini sasa hivi wakati Lowasa alishagombea na sasa ni marehemu.

Kuna wanasiasa ni wapumbavu sana wanafikiri tunataka kusikia ujinga wao kila mara.
 
Ila kura alizopata za Urais ziliweka rekodi ambayo hamkuitegemea na bado mlivuna wabunge wengi mno na hata kuongoza halmashauri kadhaa nchini.

Nyota ya Lowassa iliwanufaisha sana

Tindo zitto junior

Narudia tena, cdm walichopata ni kama kilipungua kwa ujio wa Lowassa. Cdm ndio chama kilichofanya kazi na hamasa ya kisiasa kuliko chama chochote kuanzia 2011-2015. Ndio chama kilichowafikia wananchi wengi huku wakiwa na hamasa ya kiwango Cha juu. Hata vitambulisho vya kura watu waliviita kichinjio Ili kumkata huyo Lowassa, watu wakijua ndio atakuwa chaguo la ccm.

Kama Lowassa ndio alileta ushindi ule akiwa na miezi miwili tu, je alileta viti vingapi akiwa na miaka miwili? Msitake kutuona hatujui ukweli kwa huo upotoshaji wenu usio na tija. Lowassa angepata kura zile kama angeenda TLP hapo ungekuwa na hoja. Sana sana Lowassa alirukia gari la mabadiliko, na akafaidika na hamasa iliyokuwa ndani ya cdm. Update kura 6m+ kwa kusema "elimu, elimu, elimu" tena ndani ya miezi miwili? Hata viongozi kadhaa wa cdm huwa wanakalia kimya huo upotoshaji, kama sehemu ya kufunika blunder ya kumpokea Lowassa.

Narudia tena, alaaniwe Mbowe na genge lake kwa kumpokea Lowassa na kumpa nafasi adhimu ya kugombea urais kwa maslahi Yao binafsi, akiwa hastahili, bali allitumia cdm kutimiza haja yake ya kuwa rais. Na kwa kukusaidia tu, Lowassa alikuwa haipendi cdm, na asingekaa aipende. Ninahisi hata akifufuka Leo hii ataendelea na ccm yake.
 
Nafikiri Richmond haikumwacha Lowasa salama, shida zote za koafya hienda chimbuko lake ni Richmond
Kikwete na Lowassa kuelekea 2005 walicheza rafu nyingi sana za hatari ambazo zimewagharimu/zitawagharimu. Kingunge kang'atwa na mbwa kama, Lowassa kateseka sana na zamu ya kikwete inakuja.
 
No. It was a fatal mistake!
1. Ilichafua taswira ya Chadema. Chama cha Upinzani kina Mgombea ana kashfa zaidi ya Mgombea wa Chama Tawala.

2. Lowasa alikosa sifa muhimu ya any genuine opposition candidate-MILITANT PERSON DHIDI YA DHULMA ZA CHAMA TAWALA. Hivi, kwenye mfumo ambao chama tawala ni wezi wa chaguzi, unawaambia wafuasi wako wakakae majumbani baada ya voting, halafu baada ya kuibiwa kura, huitishi public action. Hakuna wakati umma wa tanzania ulikua Umeiva kwa mabadiliko kama 2015. Mgombea wa upinzani, angekiwasha tu, nchi ingeitika, so CCM walihitaji Soft Inaction opposition candidate and yes, EL served the purpose.

3. Effect ya EL kurudi CCM, ili-demoralize wafuasi wa Upinzani hadi leo.

EL angeingia CDM na kuwa mfadhili, Silaa akasimama, nakuhakikishia JPM angekua Rais, lakini UKAWA wangejumuishwa kwenye Serikali.

Uko sahihi kwa zaidi ya 100%, Kuna watu wanapotosha kuwa kura walizopata cdm zililetwa na Lowassa! Hakuna chochote Cha maana cdm walipata ambacho wangekikosa iwapo Lowassa asingekuja, Sana Sana cdm iliishia kuharibu haiba yake na misimamo yake. Leo hii wenye mitazamo ya kipinzani na wataka mabadiliko, hawaitaki ccm, na Wala hawawaamini wapinzani ambao ni cdm.

Msimamo wangu umeendelea kubaki kuwa kumpokea Lowassa ilikuwa ni hasara kwa cdm, wakati ule, na zaidi zaidi sasa. Na ninaendelea kusisitiza ili cdm ipate hamasa mpya, ni Mbowe kutokuwa mwenyekiti wa cdm, na uenyekiti wa cdm apewe Tundu Lisu, katibu mkuu awe Heche. Mbowe kagota tusitegemee jipya toka kwake zaidi ya maridhiano ya kitapeli.
 
Back
Top Bottom