John Mnyika: Napinga ongezeko la bei ya umeme 8.5% kwa kuwa ni mzigo kwa wananchi

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,380
2,000
Anaandika Comred John Mnyika
Napinga ongezeko la bei ya umeme 8.5% lililotangazwa na EWURA kwa kuwa ni mzigo kwa wananchi na uchumi wa nchi na sababu zilizotolewa hazina msingi.

Namtaka Waziri Muhongo atengue uamuzi huo mbovu kama alivyoahidi kwamba hatarusu bei ya umeme kupanda.

Natoa mwito kwa Rais Magufuli naye katika hotuba yake kwa taifa leo au kesho azungumzie ongezeko hilo.

Iwapo Waziri au Rais hawatatoa kauli nitalifikisha suala hilo bungeni kwa hatua zaidi.

John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini
 
Capt Tamar

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
10,018
2,000
Slogan ya mwanzo kabisa ya Muhongo awamu hii ilikuwa ni kushusha bei ya umeme hasa baada ya kuanza kutumia nishati ya gas!! Lakini amegeuka!! Na ujue kuwa hii mijamaa haijawahi kuwa na chembe ya Huruma kwetu ni pale tulipoanza tu kulalamika tozo ya service charge ndipo nao walipoanza kupigania nyongeza ya bei ya umeme! Yaani ni kama tu wame shift kutoka service charge,kuiongeza tena kidogo,na Kisha kuichomeka kwenye bei Rasmi!! Wizi tu
 
Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,248
2,000
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UKAWA Yalaani Ongezeko Bei ya Umeme.

Napinga ongezeko la bei ya umeme 8.5% lililotangazwa na EWURA kwa kuwa ni mzigo kwa wananchi na uchumi wa nchi na sababu zilizotolewa hazina msingi.

Namtaka Waziri Muhongo atengue uamuzi huo mbovu kama alivyoahidi kwamba hatarusu bei ya umeme kupanda.

Natoa mwito kwa Rais Magufuli naye katika hotuba yake kwa taifa leo au kesho azungumzie ongezeko hilo.

Iwapo Waziri au Rais hawatatoa kauli nitalifikisha suala hilo bungeni kwa hatua zaidi.

John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini (CHADEMA-UKAWA)
 
Meatu01

Senior Member
Dec 20, 2016
175
225
huyu kamanda kaona aibukie na kiki ya kupanda kwa umeme dah!! by the way atoe na msimamo wake kuhusu Lowasa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom