Heparin
Senior Member
- Sep 24, 2021
- 127
- 420
Kupunguza bei ya bidhaa muhimu ikiwemo madawa na vifaa tiba kunahitaji Mkakati wa Dharura, haraka na makusudi utakaokuwa mtambuka na kutazama picha pana kwenye sekta kuu za kiuchumi kwa umma na kwa binafsi. Mkakati wa kisera, kikodi, kiutendaji na kimatumizi. Rais pitia ripoti iliyoko mezani kwako ya ufisadi na matumizi mabaya NHIF itakuongoza kufanya maamuzi sahihi. Nakiona kitanzi kwa bima ya afya kwa wote kabla hata hatujafika mbali. Narudia rai yetu ya kutaka mjadala juu ya huduma bora na nafuu za afya kwa wote.
John Mnyika
Mtandao wa X