John Mnyika John, Mbatizaji anayetuhumiwa

John Mnyika John, Mbatizaji anayetuhumiwa

Nadhani hakukimbia jimbo ila CCM walitaka kuwagawanya wananchi wa UBUNGO wawatawale wakampeleka mwenye PHD sio huyu anayesema anasomea la hasha aliyekwisha maliza na kuifanyia kazi taaluma yake ila wananchi wakakataa hila chafu na tukamchagua Mnyika not otherwise

Lakini sijui ni lini mnyika ataacha tabia ya kukimbia majimbo..
 
CCM imebeba majitu yasiyojiweza, sasa mleta mada anatofauti gani na yule mbunge wa Kutaka kulia? Na yule wa sanamu la diamond au yule wa kilimo cha bhangi? CCM inajiua yenyewe kwa kushindwa kutengeneza wabunge na viongozi wanaoweza kujenga hoja na kuchambua mambo kwa kina matokeo ndio watu kama hawa nao ni wabunge! Huyu unategemea ataweza kujenga hoja dhidi ya watu kama kina lucy, ruth, anatropia, bulaya, mdee and co!!!
 
Don't confuse John, the Baptist with John, the Disciple! Yohana Mbatizaji wala hakuishi na Bw. Yesu kwa kipindi kirefu; sana sana baada ya kumbatiza Yesu haukupita muda akakatwa kichwa na Herodi kwa raha za Herodia yule mwanamke, ashakum sio matusi, "malaya". John, au yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu ni John yule mdogo, mtume, na ambaye miongoni mwa mengi wasifu wake ni huu:-
  1. Aliandika 1 Yoh na 2 Yoh.
  2. Aliandika Ufunuo akiwa huko kisiwani Patmo - Ugiriki ya leo.
  3. Ndiye mtume wa mwisho wa Bw. Yesu kufariki na alifariki kwa uzee - hakuuwawa kama wengine akina Stefano, n.k.
Nimeona niweke tu rekodi sawa maana Shetani hutenda kazi zake kwa hila sana kwa lengo la kupotosha; hatakiwi kuachiwa nafasi pale anapojaribu kupotosha maandiko.
Asante ndugu.kwa kuongezea ndiyo mwanafunzi pekee alikuwepo na Yesu hadi wakati wa kifo msalabani.na Yesu akamwambia mama tazama mwanao na akamwambia mwanafunzi tazama mama.mara nyingi ametajwa kwa sifa hii Mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda.yohana 19:25-27. Yohana mbatizaji hakuwa mwanafunzi wa Yesu.
 
Samahani,hivi hauna mazuri yoyote ya ccm utuwekee hapa tujadili,maana kila ukija hapa ni CHADEMA, CHADEMA, CHADEMA, we si Uko CHADEMA
 
Asante ndugu.kwa kuongezea ndiyo mwanafunzi pekee alikuwepo na Yesu hadi wakati wa kifo msalabani.na Yesu akamwambia mama tazama mwanao na akamwambia mwanafunzi tazama mama.mara nyingi ametajwa kwa sifa hii Mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda.yohana 19:25-27. Yohana mbatizaji hakuwa mwanafunzi wa Yesu.
Sawa umeeleweka, kuna ziada au ulikuja kumuunga mkono huyo ndugu juu ya hilo tu..?
 
Siku zote nimekuwa nikimuita Mbatizaji,

Ni mtu mwenye maarifa mengi, asiyejikweza na mwenye ustahamilivu wa kipekee, kwa sifa zake hizo alifanya watu wengi wampende, walio ndani ya CHADEMA hata nje ya CHADEMA, mimi ni miongoni mwao.

Katika Biblia ipo habari ya Mhubiri aliyependwa na YESU, pengine habari hiyo inawashangaza watu wengi kwani mhubiri huyo hakuwa mmoja wa madhehebu yetu maarufu, hakuwa Mluteri, wala mmedhodisti, wala mpentekoste, wala mwanglikana bali alikuwa MBATISTI. Aliitwa YOHANA MBATIZAJI, akibatiza watu kwa maji.

MBATIZAJI ninayetaka kumzungumzia leo anaitwa JOHN MNYIKA JOHN DALALI, Mbunge na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA…nitamzungumza ninavyomfahamu mimi na kuoanisha ufahamu huo na masaibu yanayomkuta hivi sasa.

Naomba nianze kwa kuelezea ninavyofahamu mchango wa MNYIKA ndani ya CHADEMA kwa ufupi kama ifuatavyo;

Katika mchakato wa Uandishi wa Katiba ya sasa ya CHADEMA mwaka 2006, uliwekwa utaratibu wa kuipitia Katiba ile ya 2004 kuona kama vipo vipengele vya kuvitumia kwenye Katiba mpya na baadae ukawekwa utaratibu wa waraka kwa wanachama kutoa maoni na kuyawasilisha makao makuu. Baada ya maoni hayo kuliundwa timu tatu (3) Timu moja ilihusu kuandika falsafa na itikadi ya chama ambayo Mwenyekiti alikuwa Prof Baregu na Katibu wake alikuwa Ndg John Mnyika.

Kuhusu falsafa ilinukuliwa kwa kiasi kikubwa kutoka kwenye Katiba ya 2004 na sehemu ya ITIKADI kwa mara ya kwanza ikaingizwa kwenye Katiba, hapo awali hakukuwa na kitu kinachojulikana kama itikadi ya CHADEMA.

Nimeanza na utangulizi huo kuwakumbusha Vijana wa CHADEMA ambao wanadhani ndio wameshiba itikadi ya CHADEMA kuliko MNYIKA kuwa hiyo inayoitwa ITIKADI yenyewe, imebuniwa na kuaririwa na MNYIKA.

Nguvu, uwezo, maarifa na mchango wa JOHN katika ujenzi wa CHADEMA ni wa kipekee, hakuna namna nitaelezea hatua za ukuaji na kuimarika kwa CHADEMA ikawa katika maelezo yangu hakuna jina la MNYIKA. Kwa ufupi hivyo ndivyo ninavyomfahamu Mnyika.

Nimeshtushwa na baadhi ya kadhia zinazomfika Kaka yangu huyu, nitaeleza baadhi;

1) Nadhani wengi wenu mtakumbuka kuwa Kaka yangu huyu amekuwa kimya kwa muda mrefu, ukimya wake ukapewa tafsiri kadha wa kadha kwa watu waliomzunguka. Ukimya wa MNYIKA ulianza pale tu MHE LOWASSA alipojiunga na CHADEMA, baada ya kuhama kwa Dr Slaa kulikotokana na ujio huo wa LOWASSA na kushambuliwa na GWAJIMA, na baadae andiko la Ndg Petro E. Mselewa Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA ambalo lilihusishwa na Mnyika, alituhumiwa kuwa anampinga LOWASSA na hivyo anapinga MABADILIKO. Ni kweli Dr Slaa ni Political Godfather wa Mnyika, na ni ukweli kuwa hasingelipenda kuona akina GWAJIMA wakimtukana hadharani ama kuungana nao kumkashifu kwa kila aina ya kashfa. Lakini kutokuwa tayari kuungana na akina Tundu Lissu, Mbowe na Gwajima kumshambulia Dr Slaa sio lazima kutafsiriwe kuwa ni UASI kwa Chama.

2) Tarehe 25th September, 2015 Mpambe mmoja wa wakubwa wa CHADEMA akaandika hapa JF John Mnyika, aidha ungana na wenzio au kubali kushindwa Kibamba Anatumia i.d ya Mpululu {alifunguliwa January 3, 2013 wakati wa sakata langu, ilikuwa ikinishambulia asubuhi na jioni} baadae nilifanikiwa kumjua mwenye i.d hiyo, ni mtu wa Kanda ya Juu Kusini, mzaliwa wa Njombe, Mpambe wa wakubwa, Cybercrime inamlinda. Mtu huyo akaandika akimtabiria Mnyika kushindwa jimbo la Kibamba, na kumshambulia kuwa anajitenga na UKAWA na Mhe Lowassa. Mnyika Hakujibu.

4) Baaada ya Lowassa na Sumaye kupitishwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu, kuna waraka ulitembea mitandaoni ukieleza kuwa MNYIKA hajaridhika na hatua hiyo na kwamba anataka kujiengua CHADEMA, akatuhumiwa kwa mara nyingine. Mara hii, Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi akampigia simu kutaka uhakika wa jambo hilo, na hatimae Mwananchi la tarehe 10 July,2016 likaandika “SINA MPANGO WA KUHAMA CHADEMA” lakini wale wa kazi maalum ambao wanamuona MNYIKA kuwa ni kirusi waliendelea kumshambulia kuwa kwanini iwe kwa simu, kwanini asifanye Press.

5) Kadhia ya tano (5) na ya mwisho ni habari iliyoletwa na Ndugu yangu Frey Cosseny, kwa kuwa namfahamu Frey, nimebaki na butwaa, maana si rahisi kuwa habari hiyo ni uzushi wa kutungwa. Frey anaandika kuwa Mnyika kuondolea Naibu Katibu Mkuu Chadema Anayetajwa kumrithi ni Ruth Mollel, Mbunge mwenzangu wa Viti Maalum, najua ni msomi mzuri mwenye experience kubwa kwani ameshawahi kuwa Katibu Mkuu wizara mbalimbali pamoja na ofisi ya Waziri Mkuu lakini nikikumbuka Nguvu na Jitihada za Mnyika katika ujenzi wa CHADEMA na nafasi yake kupewa mtu aliyejiunga CHADEMA juzi tena baada ya LOWASSA kujiunga na CHADEMA, Napata mashaka makubwa kuwa uamuzi huo unaokuja ndani ya CHADEMA ni rational..? Naendelea kuona Ubeberu ukitawala ndani ya CHADEMA. Pamoja na yooote ambayo Mnyika amekuwa akihusishwa nayo, bado MNYIKA ni MTU ANAYEAMINIKA na litakuwa kosa lingine la kiufundi kwa CHADEMA kumng’oa mtu kama MNYIKA.

Najua watajitokeza watu watakaosema kuwa JULIANA hawezi kuitakia mema CHADEMA, na kwamba uamuzi huo ndio hasa wa kuushikilia, lakini mimi ni kama ilivyo kwa Mwalimu ambaye mpaka kufa kwake aliamini kuwa ili tuwe na CCM imara ni lazima tuwe na Upinzani makini. Mnyika ni Mpinzani makini, inawezekana kabisa ameacha harakati na kuamua kuwa mwanasiasa kamili lakini bado MNYIKA ni mtu hodari na mwenye mchango wa kipekee kwa siasa za nje yetu. Maana limeandika Gazeti la UMMA Tanzania la Julai 28 –Agosti 3, 2016 (mmiliki wake mnamjua) katika Ukurasa wake wa mbele “MNYIKA ATENGANISHA SIASA NA HARAKATI” na maelezo ya habari hiyo yakatolewa ukurasa wa tatu. Kwamba inaonekana harakati za akina TUNDU LISSU na akina KUBENEA ndio msingi wa siasa za Upinzani na kwamba kujitenga nazo ni UASI na USALITI. Jambo hili halikuwahi kuwa kweli na halitakuwa kweli.

Binafsi namjua MBATIZAJI, najua uwezo wake na umahiri wake kwenye siasa. Nimefanya nae mambo mengi katika ujenzi wa CHADEMA, alikuwa na wito na ailutimiza kwa bidii. Nitaumia na kuona kuwa ndoto zake haziji kuwa kweli. Na kwa wale wapambe wa wakubwa wanaotumwa kushambulia watu wasiokubalina na mabosi wao mitandaoni, ufike wakati mjipime na muweke mizania ya fikra zenu.

Nitaendelea kuwafunulia yale yaliyofunikwa maana mna viongozi mabingwa wa kufunika nanyi mmekuwa wafuasi msiohoji.
Kwa maelezo yote haya sijaona cha maana zaidi ya majungu na umbea tu. Kama unampenda Mnyika kamwambie huko sasa sisi yanatuhusu nini. Hivi hizi elimu na vyeti mnapataje? Maana ulichokiandika akiendani na elimu uliyonayo kabisa. PhD inakufundisha kuleta majungu humu, acha umbea Dada. Umeshapata ulaji wa ganda la dizi tulia ule sio kutuletea siasa taka hapa.

Chadema ndiyo iliyokulea mpaka kufika hapo alafu leo unatuletea pumba zako humu. Jifunze kufikiri kwanza kabla ya kuleta ujinga wako hapa.
 
Samahani,hivi hauna mazuri yoyote ya ccm utuwekee hapa tujadili,maana kila ukija hapa ni CHADEMA, CHADEMA, CHADEMA, we si Uko CHADEMA
Sijakuelewa..? Labda ujaribu kutuma tena ujumbe wako ukiwa umefanyiwa masahihisho.
 
Katika Biblia ipo habari ya Mhubiri aliyependwa na YESU, pengine habari hiyo inawashangaza watu wengi kwani mhubiri huyo hakuwa mmoja wa madhehebu yetu maarufu, hakuwa Mluteri, wala mmedhodisti, wala mpentekoste, wala mwanglikana bali alikuwa MBATISTI. Aliitwa YOHANA MBATIZAJI, akibatiza watu kwa maji.

Dudus umemgusa hapo kwenye rejeo lako la Biblia, na kwa kuwa yeye ni mkereketwa wa Neno la Mungu, ndio ukamuibua. kwa hiyo usishangae sana anapojikita katika eneo hilo, kwamba mbona hajatoa maoni yoyote katika mada uliyokuwa unaiwasilisha. mimi pia ni mkereketwa wa Biblia na nimefuatilia vizuri majibizano yako na Dudus. nakubaliana kabisa na hoja za Dudus, na amekupa ushauri mzuri tu ambao hukuwa na haja ya kubwatizana naye. sana sana ni kumshukuru tu kwa sababu yeye si mkereketwa wa mambo ya Siasa kwa namna unayofikiria.

Kwa kuongozea, mimi nisingefikiria kwamba Yohani Mbatizaji alikuwa "Mhubiri", maana kwa hakika alikuwa "Nabii" ambaye alikuja kwa lengo la kuandaa ujio wa Mkombozi, Yesu Kristu. Alibatiza watu kwa maji. sifa ya "kupendwa na Yesu" nadhani ingefaa zaidi kwa Yohana Mtume, na siyo huyu, kwa kuwa imeandikwa wazi katika maandiko [Yoh.13:23, etc.], kama alivyofafanua Dudus. Ni kweli, Yohana Mbatizaji alikuwa jamaa hasa wa Yesu kwa maana ya upande wa mama yake Mariamu [Lk. 1:36], na kwa kweli Yesu alimwona kama Nabii wa hali ya juu kabisa [Mathayo 11:9], na hata kudiriki kusema kwamba katika waliozaliwa na wanawake, hakuna aliye mkuu kuliko Yohane Mbatizaji [Mathayo 11:11]. Lakini pamoja na hayo yote, sifa ya "aliyependwa na Yesu" bado inakwenda kwa Yohane Mtume.

Pia nisingefikiria kwamba Yohane Mbatizaji alikuwa "Mbatisti", kwa kuwa mgawanyo wa madhehebu ulikuja baadaye sana, kwa imani fulani kuhusu ubatizo. tatizo ni kwamba ubatizo wa Yohana ulikuwa tofauti na huu wa sasa hivi baada ya ufufuko wa Yesu. kwa hiyo hii ni michango tunaitoa kuweka sawa hicho ulichonukuu. kumbuka kwamba kuna wengi sana wanasoma hii michango, na wana interest tofauti.
 
Sijakuelewa..? Labda ujaribu kutuma tena ujumbe wako ukiwa umefanyiwa masahihisho.
Nasema tumechoka kujadili ya CHADEMA kila siku kutoka kwako,naomba utuletee mazuri ya chama chako kipya tuyajadili,maana umehama CHADEMA lakini kila ukiingia jamvini unajadili CHADEMA tu,au huko hamna jipya
 
Asante ndugu.kwa kuongezea ndiyo mwanafunzi pekee alikuwepo na Yesu hadi wakati wa kifo msalabani.na Yesu akamwambia mama tazama mwanao na akamwambia mwanafunzi tazama mama.mara nyingi ametajwa kwa sifa hii Mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda.yohana 19:25-27. Yohana mbatizaji hakuwa mwanafunzi wa Yesu.
Naam, tuko pamoja sana mkuu. Yapo mengi sana kumhusu huyu Yohana au "mwanafunzi aliyempenda"; huyu pia siku ya ufufuko wa Bwana alikuwa wa kwanza kufika kaburini lakini hakuingia akiwasubiri akina Petro. Huyu Yohana ndiye yule ambaye Bw. Yesu aliwachukua yeye, na Petro, na Yakobo hadi Mlimani na Yesu akabadilika sura, wakatokea akina ... wakaongea naye.

Huyu Yohana ndiye yule ambaye yule mwanamke mjane alipofiwa na mwanae, Yesu alipofika nyumbani, alimtwaa yeye, na Petro, na Yakobo wakaingia ndani kumfufua yule maiti. Wasifu wa huyu Yohana aliyependwa ni mrefu sana hata dissertation na thesis volume by volumes zaweza kuandikwa kumhusu yeye.
 
Kwa maelezo yote haya sijaona cha maana zaidi ya majungu na umbea tu. Kama unampenda Mnyika kamwambie huko sasa sisi yanatuhusu nini. Hivi hizi elimu na vyeti mnapataje? Maana ulichokiandika akiendani na elimu uliyonayo kabisa. PhD inakufundisha kuleta majungu humu, acha umbea Dada. Umeshapata ulaji wa ganda la dizi tulia ule sio kutuletea siasa taka hapa.

Chadema ndiyo iliyokulea mpaka kufika hapo alafu leo unatuletea pumba zako humu. Jifunze kufikiri kwanza kabla ya kuleta ujinga wako hapa.
Anajina la I.D "siasa basi"
Amejiunga JF; tarehe 10 July 2016.

Bila shaka ni katika zile ajira mpya,

Reply: 177
likes: 261
Trophies: 80.

Ndio ajira zenyewe hizi...!!!
 
CCM inarecruit watu kama hawa wenye upeo mdogo, hizi ni type za wale wabunge kama yule sanamu la diamond, yule wa Kutaka kulia na yule wa kilimo cha bhangi halafu kipindi cha kampeni kuwauza inakuwa ngumu wanaanza kutumia nguvu! Sasa mleta uzi kweli anaweza kujenga hoja na akaitete mbele ya wabunge Kama mdee, bulaya, anatropia, gekul, ruth, sakaya na wengine kweli? Wakifikia hapo kwa akili zilivyofupi wanaanza kusema Wanataka kulia kumbe kichwani wamejaza ujinga! CCM inajiua yenyewe kwa kuchukua mizigo ambayo kichwani ni mitambo! Mleta mada anaweza kusimama mahali akatoa hoja ya maana kukitetea chama kweli kwa upeo huu, CCM wachawi wenu ni mfumo wenu wa Kuwapata viongozi wenu na hichi kitanzi lazima kiwamalize.
 
Kwanza mwandishi mwenyewe ni kama ndo anajifunza kuandika....hakuna logical sequence....kwenye hilo andiko.....nataman Mnyika aje akufundishe jinsi ya kuandika .....kuhusu ulichoandoka hakuna namna naweza kujibu kwani hakieleweki
 
Huyu asitafute kick kwa ubunge ambao huwezi kupigwa mahakamani, halafu anamjadili mbunge anayeweza kupigwa mahakamani? CCM wenyewe wanamjua Mnyika ni nani maana kapigana na anaubunge wa kuchaguliwa sio huu wa ganda la ndizi, akafanye yake na mwenzake
Ruth molel, Joyce Mukya nao ubunge wao wa ganda la ndizi?
 
Siasa za nchi hii vijana
Unahisi nafikiri ndani ya boksi? Acheni siasa za majitaka za kwenye mitandao ya kijamii! Siasa za kujenga majungu, kuleta uchonganishi, hizo ni siasa muflisi na Kijana hapaswi kuendekeza kwani zinatabia ya kudumaza akili na matokeo yake Tunakuja kupata watu kama Olesendaka na kina makamba Sr

Nakuhurumia sana ,kwa vile najua statas yako ndo maana inabidi nikusamehe tu ,hivi MBOWE NA OLE SENDEKA wanatofauti gani ukiachilia mbali ubepari wa mbowe
 
TUMEFIKA HAPA KWA UDHAIFU WA .........K
 
Back
Top Bottom