John Mnyika John, Mbatizaji anayetuhumiwa

John Mnyika John, Mbatizaji anayetuhumiwa

Don't confuse John, the Baptist with John, the Disciple! Yohana Mbatizaji wala hakuishi na Bw. Yesu kwa kipindi kirefu; sana sana baada ya kumbatiza Yesu haukupita muda akakatwa kichwa na Herodi kwa raha za Herodia yule mwanamke, ashakum sio matusi, "malaya". John, au yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu ni John yule mdogo, mtume, na ambaye miongoni mwa mengi wasifu wake ni huu:-
  1. Aliandika 1 Yoh na 2 Yoh.
  2. Aliandika Ufunuo akiwa huko kisiwani Patmo - Ugiriki ya leo.
  3. Ndiye mtume wa mwisho wa Bw. Yesu kufariki na alifariki kwa uzee - hakuuwawa kama wengine akina Stefano, n.k.
Nimeona niweke tu rekodi sawa maana Shetani hutenda kazi zake kwa hila sana kwa lengo la kupotosha; hatakiwi kuachiwa nafasi pale anapojaribu kupotosha maandiko.
AMEN,UBARIKIWE.
 
Naam, tuko pamoja sana mkuu. Yapo mengi sana kumhusu huyu Yohana au "mwanafunzi aliyempenda"; huyu pia siku ya ufufuko wa Bwana alikuwa wa kwanza kufika kaburini lakini hakuingia akiwasubiri akina Petro. Huyu Yohana ndiye yule ambaye Bw. Yesu aliwachukua yeye, na Petro, na Yakobo hadi Mlimani na Yesu akabadilika sura, wakatokea akina ... wakaongea naye.

Huyu Yohana ndiye yule ambaye yule mwanamke mjane alipofiwa na mwanae, Yesu alipofika nyumbani, alimtwaa yeye, na Petro, na Yakobo wakaingia ndani kumfufua yule maiti. Wasifu wa huyu Yohana aliyependwa ni mrefu sana hata dissertation na thesis volume by volumes zaweza kuandikwa kumhusu yeye.

Hakika mkuu.pia alipenda kuegemea kifuani kwa Yesu.
 
Hivi karibuni nitawaletea mkakati unaoendelea ya kuwaondoa wapambe wa Dr Silaa ktk Secretariat mpya ya chadema, na kwanini salum mwalimu alipandishwa ghafla toka vodacom na kuwa NKM cdm Mara baada ya kuondolewa channel ten kuna uhusiano ipi kati ya Chanel10 vodacom na Cdm
Tunazisubiri kwa hamu hizo hisia zako!
 
nimesoma kwa umakini sana!! sikuelewa unakoelekea!! Je Mnyika bado kiongozi chadema? Je Mnyika umemwona akilalamika? wapi? Juzi alipopeleka kesi mahakama ya Afrika Mashariki alifanya kwa ajili ya nani?? Shonza Shonza jamani huko hawajakukumbuka hata kiduchu? Pole wee!

Nikweli Mnyika ni moja ya wanasiasa vijana wanaofanya siasa kwa akili kubwa bila kutumia nguvu za mwili.
Ukimya wake unanikwaza nafikiri chama chake waone tatizo ni nini hasa
 
Don't confuse John, the Baptist with John, the Disciple! Yohana Mbatizaji wala hakuishi na Bw. Yesu kwa kipindi kirefu; sana sana baada ya kumbatiza Yesu haukupita muda akakatwa kichwa na Herodi kwa raha za Herodia yule mwanamke, ashakum sio matusi, "malaya". John, au yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu ni John yule mdogo, mtume, na ambaye miongoni mwa mengi wasifu wake ni huu:-
  1. Aliandika 1 Yoh na 2 Yoh.
  2. Aliandika Ufunuo akiwa huko kisiwani Patmo - Ugiriki ya leo.
  3. Ndiye mtume wa mwisho wa Bw. Yesu kufariki na alifariki kwa uzee - hakuuwawa kama wengine akina Stefano, n.k.
Nimeona niweke tu rekodi sawa maana Shetani hutenda kazi zake kwa hila sana kwa lengo la kupotosha; hatakiwi kuachiwa nafasi pale anapojaribu kupotosha maandiko.

Uko vizuri Mkuu. Herodia alimchukia Yohana mbatizaji kwa sababu alimwambia Herode (II) siyo vema kuishi na mke wa nduguye (Philip) ambaye alikuwa ni half brother wa Herode (II). Binti yake (Salome) alipocheza na kumfurahisha Herode, alimwahidi zawadi yoyote ndipo binti alipomuuliza mama yake aombe zawadi gani. Herode na Philp walikuwa watoto wa Herode mkuu (Herod The Great), Salome lilikuwa ni jina la dada yake Herod The Great.
 
Mbona unapoteza muda mwingi kuhangaika na kitu ulichokiacha? Naona unajipa majukumu mazito mno. Naamin wanaccm jimboni kwako hakukuchagua kuwachambulia mambo ya cdm.
 
Siku zote nimekuwa nikimuita Mbatizaji,

Ni mtu mwenye maarifa mengi, asiyejikweza na mwenye ustahamilivu wa kipekee, kwa sifa zake hizo alifanya watu wengi wampende, walio ndani ya CHADEMA hata nje ya CHADEMA, mimi ni miongoni mwao.

Katika Biblia ipo habari ya Mhubiri aliyependwa na YESU, pengine habari hiyo inawashangaza watu wengi kwani mhubiri huyo hakuwa mmoja wa madhehebu yetu maarufu, hakuwa Mluteri, wala mmedhodisti, wala mpentekoste, wala mwanglikana bali alikuwa MBATISTI. Aliitwa YOHANA MBATIZAJI, akibatiza watu kwa maji.

MBATIZAJI ninayetaka kumzungumzia leo anaitwa JOHN MNYIKA JOHN DALALI, Mbunge na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA…nitamzungumza ninavyomfahamu mimi na kuoanisha ufahamu huo na masaibu yanayomkuta hivi sasa.

Naomba nianze kwa kuelezea ninavyofahamu mchango wa MNYIKA ndani ya CHADEMA kwa ufupi kama ifuatavyo;

Katika mchakato wa Uandishi wa Katiba ya sasa ya CHADEMA mwaka 2006, uliwekwa utaratibu wa kuipitia Katiba ile ya 2004 kuona kama vipo vipengele vya kuvitumia kwenye Katiba mpya na baadae ukawekwa utaratibu wa waraka kwa wanachama kutoa maoni na kuyawasilisha makao makuu. Baada ya maoni hayo kuliundwa timu tatu (3) Timu moja ilihusu kuandika falsafa na itikadi ya chama ambayo Mwenyekiti alikuwa Prof Baregu na Katibu wake alikuwa Ndg John Mnyika.

Kuhusu falsafa ilinukuliwa kwa kiasi kikubwa kutoka kwenye Katiba ya 2004 na sehemu ya ITIKADI kwa mara ya kwanza ikaingizwa kwenye Katiba, hapo awali hakukuwa na kitu kinachojulikana kama itikadi ya CHADEMA.

Nimeanza na utangulizi huo kuwakumbusha Vijana wa CHADEMA ambao wanadhani ndio wameshiba itikadi ya CHADEMA kuliko MNYIKA kuwa hiyo inayoitwa ITIKADI yenyewe, imebuniwa na kuaririwa na MNYIKA.

Nguvu, uwezo, maarifa na mchango wa JOHN katika ujenzi wa CHADEMA ni wa kipekee, hakuna namna nitaelezea hatua za ukuaji na kuimarika kwa CHADEMA ikawa katika maelezo yangu hakuna jina la MNYIKA. Kwa ufupi hivyo ndivyo ninavyomfahamu Mnyika.

Nimeshtushwa na baadhi ya kadhia zinazomfika Kaka yangu huyu, nitaeleza baadhi;

1) Nadhani wengi wenu mtakumbuka kuwa Kaka yangu huyu amekuwa kimya kwa muda mrefu, ukimya wake ukapewa tafsiri kadha wa kadha kwa watu waliomzunguka. Ukimya wa MNYIKA ulianza pale tu MHE LOWASSA alipojiunga na CHADEMA, baada ya kuhama kwa Dr Slaa kulikotokana na ujio huo wa LOWASSA na kushambuliwa na GWAJIMA, na baadae andiko la Ndg Petro E. Mselewa Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA ambalo lilihusishwa na Mnyika, alituhumiwa kuwa anampinga LOWASSA na hivyo anapinga MABADILIKO. Ni kweli Dr Slaa ni Political Godfather wa Mnyika, na ni ukweli kuwa hasingelipenda kuona akina GWAJIMA wakimtukana hadharani ama kuungana nao kumkashifu kwa kila aina ya kashfa. Lakini kutokuwa tayari kuungana na akina Tundu Lissu, Mbowe na Gwajima kumshambulia Dr Slaa sio lazima kutafsiriwe kuwa ni UASI kwa Chama.

2) Tarehe 25th September, 2015 Mpambe mmoja wa wakubwa wa CHADEMA akaandika hapa JF John Mnyika, aidha ungana na wenzio au kubali kushindwa Kibamba Anatumia i.d ya Mpululu {alifunguliwa January 3, 2013 wakati wa sakata langu, ilikuwa ikinishambulia asubuhi na jioni} baadae nilifanikiwa kumjua mwenye i.d hiyo, ni mtu wa Kanda ya Juu Kusini, mzaliwa wa Njombe, Mpambe wa wakubwa, Cybercrime inamlinda. Mtu huyo akaandika akimtabiria Mnyika kushindwa jimbo la Kibamba, na kumshambulia kuwa anajitenga na UKAWA na Mhe Lowassa. Mnyika Hakujibu.

4) Baaada ya Lowassa na Sumaye kupitishwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu, kuna waraka ulitembea mitandaoni ukieleza kuwa MNYIKA hajaridhika na hatua hiyo na kwamba anataka kujiengua CHADEMA, akatuhumiwa kwa mara nyingine. Mara hii, Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi akampigia simu kutaka uhakika wa jambo hilo, na hatimae Mwananchi la tarehe 10 July,2016 likaandika “SINA MPANGO WA KUHAMA CHADEMA” lakini wale wa kazi maalum ambao wanamuona MNYIKA kuwa ni kirusi waliendelea kumshambulia kuwa kwanini iwe kwa simu, kwanini asifanye Press.

5) Kadhia ya tano (5) na ya mwisho ni habari iliyoletwa na Ndugu yangu Frey Cosseny, kwa kuwa namfahamu Frey, nimebaki na butwaa, maana si rahisi kuwa habari hiyo ni uzushi wa kutungwa. Frey anaandika kuwa Mnyika kuondolea Naibu Katibu Mkuu Chadema Anayetajwa kumrithi ni Ruth Mollel, Mbunge mwenzangu wa Viti Maalum, najua ni msomi mzuri mwenye experience kubwa kwani ameshawahi kuwa Katibu Mkuu wizara mbalimbali pamoja na ofisi ya Waziri Mkuu lakini nikikumbuka Nguvu na Jitihada za Mnyika katika ujenzi wa CHADEMA na nafasi yake kupewa mtu aliyejiunga CHADEMA juzi tena baada ya LOWASSA kujiunga na CHADEMA, Napata mashaka makubwa kuwa uamuzi huo unaokuja ndani ya CHADEMA ni rational..? Naendelea kuona Ubeberu ukitawala ndani ya CHADEMA. Pamoja na yooote ambayo Mnyika amekuwa akihusishwa nayo, bado MNYIKA ni MTU ANAYEAMINIKA na litakuwa kosa lingine la kiufundi kwa CHADEMA kumng’oa mtu kama MNYIKA.

Najua watajitokeza watu watakaosema kuwa JULIANA hawezi kuitakia mema CHADEMA, na kwamba uamuzi huo ndio hasa wa kuushikilia, lakini mimi ni kama ilivyo kwa Mwalimu ambaye mpaka kufa kwake aliamini kuwa ili tuwe na CCM imara ni lazima tuwe na Upinzani makini. Mnyika ni Mpinzani makini, inawezekana kabisa ameacha harakati na kuamua kuwa mwanasiasa kamili lakini bado MNYIKA ni mtu hodari na mwenye mchango wa kipekee kwa siasa za nje yetu. Maana limeandika Gazeti la UMMA Tanzania la Julai 28 –Agosti 3, 2016 (mmiliki wake mnamjua) katika Ukurasa wake wa mbele “MNYIKA ATENGANISHA SIASA NA HARAKATI” na maelezo ya habari hiyo yakatolewa ukurasa wa tatu. Kwamba inaonekana harakati za akina TUNDU LISSU na akina KUBENEA ndio msingi wa siasa za Upinzani na kwamba kujitenga nazo ni UASI na USALITI. Jambo hili halikuwahi kuwa kweli na halitakuwa kweli.

Binafsi namjua MBATIZAJI, najua uwezo wake na umahiri wake kwenye siasa. Nimefanya nae mambo mengi katika ujenzi wa CHADEMA, alikuwa na wito na ailutimiza kwa bidii. Nitaumia na kuona kuwa ndoto zake haziji kuwa kweli. Na kwa wale wapambe wa wakubwa wanaotumwa kushambulia watu wasiokubalina na mabosi wao mitandaoni, ufike wakati mjipime na muweke mizania ya fikra zenu.

Nitaendelea kuwafunulia yale yaliyofunikwa maana mna viongozi mabingwa wa kufunika nanyi mmekuwa wafuasi msiohoji.
huu muda unaotumia kuandika huu uchafu wako mnge msaidia mwenyekikiti wenu kuielewa katiba
 
Mnyika angehamia CCM on time angekuwa mbali sana kisiasa, sasa ni too late. Chama kimeshanunuliwa na kina Mnyika wote wamegeuzwa bidhaa.

Unaona kina Shonza na Mtela walishtuka mapema sasa hivi wanashine. Ben Saanane sasa hivi anajuta kwanini hakushirikiana na vijana wenzake.
Upinzani ni mbovu sana, ila nje dola ccm ni mbovu kuawzidi.
 
Mnyika lazima alishafanya yake mana anavyosifiwa... Nway ya ngoswe muachie ngoswe mwenyewe
 
Uzi mzuri sana ila hakuna atakae changia hoja murua ila wote wataleta personal attac simply kwa sababu umeandika wewe juliana
Juliana ana sifa za kuwa mwanasiasa kwani ana ngozi ngumu, anavumilia mashambulizi
Napita ila hizi harakati zote za kumpinga Mnyika ni kwa kuwa ni mfuasi mkubwa sana wa Dr Slaa hivyo wapiga dili lazima wampinge huyo mama mtu wa lowasa
 
Nimesikia maneno mengi kuhusu jambo la Mnyika
, nadhani ni vyema sasa Mnyika akazungumza maana haya ya watu kujipa usemaji wa Mnyika sio pouwa sana. Jamaa atueleze nini kinaendelea..kama kuna sintofahamu kati yake na Lowassa au maneno tu.
 
Sina tabia ya kujibu wala mie sio mwanasiasa..
Sijawahi kukufuatilia Juliana Shonza kwa sababu sio type ya wanasiasa ninaowafuatilia,wala hujawahi kuwa mwanasiasa ambaye unaweza kufuatiliwa na vijana ambao wangependa kuona Taifa hili linasonga mbele,,nimeshangaa sana kuniita mpambe wa viongozi wa Chadema,mpaka kunifuatilia wapi natokea, sijawahi kuwa mwanachama wa Chadema wala sijawahi kuchukua kadi ya Chama chochote cha siasa ,me ni Mtanzania ninayeitakia mema nch yangu,sijuani hata na kiongozi wa Chadema,na wala sijawahi hata kusalimiana na mtu yeyote anayeitwa kiongozi wa Chadema japo nimewahi kukishangilia Chadema kama Mtanzania mwingine mpenda democrasia na maendeleo ya nch yake, kama ambavyo namshangilia this time Mheshimiwa Daktari J Magufuli kwa nia yake ya dhati ya kutaka kuona Tanzania inasonga mbele..
Msingi wangu wa maada hiyo uliyoweka hapo kuwa nilitumwa nimshambulie Mnyika ilijikita katika ukimya wa Mnyika kwa kipindi kile,ndio maana kwa Mtazamo wangu nilitamani sana kuona Mnyika akiwa active kama ambavyo tumemzoea(Mnyika ni mwanasiasa ninayemfuatilia sana kwa mchango wake kwa Taifa hili na wala sio kwa mchango wake kwa Chadema )
Naomba nikwambie Juliana Shonza sijawahi kuwa mpambe wa Chadema,wala mpambe wa kiongozi yeyote,,acha kutuhumu watu usio wajua,haipendezi mke wa mtu kama wewe kuanza kuropoka mambo,kutoa kashifa kwa vitu ambavyo huna hata chembe ya uhakika navyo..@Mods naomba mnisaidie huyu dada athibitishe kuwa nilitumwa na viongozi wa Chadema kuandika hiyo post aliyoisema
USHAURI...Ukiamua kuolewa usikumbuke nyumbani kwenu bali jenga nyumba yako nawe uwe mama bora na nyumba yako, ni bora ukafanya siasa za kuimarisha chama chako cha Ccm kuliko kila siku kukaa kuyaongelea hayo ya familia ya CHADEMA MPAKA KUANZA KUSEMA UONGO,KUHUSISHA WATU WASIO WANASIASA NA SIASA ZAKO
Kwa kunihusisha mimi mpululu na maada yake naomba niwambie wanaukumbi kuwa nadhani maelezo yake yote ni uongo maana hakuna la ukweli aliloandika juu yangu...
 
Mbona unajichanganya ktk hoja? Umewai kushabikia cdm ila wewe siyo mwanasiasa, unamfuatilia siasa za Mnyika ila wewe siyo mwanasiasa, mi nadhani soma tena bandiko la Juiana ili ujue alichosema juu yako sidhani km alisema wewe ni mwanasiasa au mwanachama wa Cdm? Ukiona una jina bandia halafu mtu akakufahamu ujue amefanya reseach ya kutosha na jina lako analo
 
kwahiyo anayefuatilia mpira lazima awe mchezaji? sijui unatumia ubongo au nini...kwa taarifa yako na huyo Juliana wako,,hata anakosema nimetokea sio kweli..Hudhani kasema kuwa...soma bandiko lake ujue kanihusisha wapi sio unakuja na nadharia za kudhani..Juliana kasema nilitumwa na mabosi wangu ambao ni viongozi wa juu wa CDM...kukumbusha tu Sabodo ashawahi kuishabikia Chadema na huku hakuwa mwanachadema
 
Jitadhimini hakuna ktk post ambapo Juliana kasema umetumwa na wakubwa wa Cdm unajishuku mwenyewe mkuu. Alichpandika ni kuwa wewe ni mpambe wa wakubwa cdm na unalindwa na wakubwa wa cdm cybecrime wasikukukamate
 
we jamaa mbona kaandika kiswahili wapi huelewi? hakuna sehemu aliyoandika kuwa nalindwa na wakubwa wa Chadema cybecrime wasinikamate...ILA KAANDIKA CYBECRIME INANILINDA AKIMAANISHA KUWA HAWEZI KUNIEXPOSE MAJINA YANGU NA DETAILS ZANGU MAANA ATABANWA NA SHERIA HIYO..sasa kama hata kusoma na kuelewa tu alichoandika ni tatizo halafu unataka uchangie kweli tatizo,vingine muwe mnaacha vipite
NIKUKUMBUSHE TU CHADEM SIO WASIMAMIZI WA MAKOSA YA MITANDAO,CHADEMA NI CHAMA CHA SIASA,WANAOSIMAMIA MAMBO HAYO NI TCRA
 
Back
Top Bottom