Juliana Shonza
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 2,009
- 1,609
Siku zote nimekuwa nikimuita Mbatizaji,
Ni mtu mwenye maarifa mengi, asiyejikweza na mwenye ustahamilivu wa kipekee, kwa sifa zake hizo alifanya watu wengi wampende, walio ndani ya CHADEMA hata nje ya CHADEMA, mimi ni miongoni mwao.
Katika Biblia ipo habari ya Mhubiri aliyependwa na YESU, pengine habari hiyo inawashangaza watu wengi kwani mhubiri huyo hakuwa mmoja wa madhehebu yetu maarufu, hakuwa Mluteri, wala mmedhodisti, wala mpentekoste, wala mwanglikana bali alikuwa MBATISTI. Aliitwa YOHANA MBATIZAJI, akibatiza watu kwa maji.
MBATIZAJI ninayetaka kumzungumzia leo anaitwa JOHN MNYIKA JOHN DALALI, Mbunge na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA…nitamzungumza ninavyomfahamu mimi na kuoanisha ufahamu huo na masaibu yanayomkuta hivi sasa.
Naomba nianze kwa kuelezea ninavyofahamu mchango wa MNYIKA ndani ya CHADEMA kwa ufupi kama ifuatavyo;
Katika mchakato wa Uandishi wa Katiba ya sasa ya CHADEMA mwaka 2006, uliwekwa utaratibu wa kuipitia Katiba ile ya 2004 kuona kama vipo vipengele vya kuvitumia kwenye Katiba mpya na baadae ukawekwa utaratibu wa waraka kwa wanachama kutoa maoni na kuyawasilisha makao makuu. Baada ya maoni hayo kuliundwa timu tatu (3) Timu moja ilihusu kuandika falsafa na itikadi ya chama ambayo Mwenyekiti alikuwa Prof Baregu na Katibu wake alikuwa Ndg John Mnyika.
Kuhusu falsafa ilinukuliwa kwa kiasi kikubwa kutoka kwenye Katiba ya 2004 na sehemu ya ITIKADI kwa mara ya kwanza ikaingizwa kwenye Katiba, hapo awali hakukuwa na kitu kinachojulikana kama itikadi ya CHADEMA.
Nimeanza na utangulizi huo kuwakumbusha Vijana wa CHADEMA ambao wanadhani ndio wameshiba itikadi ya CHADEMA kuliko MNYIKA kuwa hiyo inayoitwa ITIKADI yenyewe, imebuniwa na kuaririwa na MNYIKA.
Nguvu, uwezo, maarifa na mchango wa JOHN katika ujenzi wa CHADEMA ni wa kipekee, hakuna namna nitaelezea hatua za ukuaji na kuimarika kwa CHADEMA ikawa katika maelezo yangu hakuna jina la MNYIKA. Kwa ufupi hivyo ndivyo ninavyomfahamu Mnyika.
Nimeshtushwa na baadhi ya kadhia zinazomfika Kaka yangu huyu, nitaeleza baadhi;
1) Nadhani wengi wenu mtakumbuka kuwa Kaka yangu huyu amekuwa kimya kwa muda mrefu, ukimya wake ukapewa tafsiri kadha wa kadha kwa watu waliomzunguka. Ukimya wa MNYIKA ulianza pale tu MHE LOWASSA alipojiunga na CHADEMA, baada ya kuhama kwa Dr Slaa kulikotokana na ujio huo wa LOWASSA na kushambuliwa na GWAJIMA, na baadae andiko la Ndg Petro E. Mselewa Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA ambalo lilihusishwa na Mnyika, alituhumiwa kuwa anampinga LOWASSA na hivyo anapinga MABADILIKO. Ni kweli Dr Slaa ni Political Godfather wa Mnyika, na ni ukweli kuwa hasingelipenda kuona akina GWAJIMA wakimtukana hadharani ama kuungana nao kumkashifu kwa kila aina ya kashfa. Lakini kutokuwa tayari kuungana na akina Tundu Lissu, Mbowe na Gwajima kumshambulia Dr Slaa sio lazima kutafsiriwe kuwa ni UASI kwa Chama.
2) Tarehe 25th September, 2015 Mpambe mmoja wa wakubwa wa CHADEMA akaandika hapa JF John Mnyika, aidha ungana na wenzio au kubali kushindwa Kibamba Anatumia i.d ya Mpululu {alifunguliwa January 3, 2013 wakati wa sakata langu, ilikuwa ikinishambulia asubuhi na jioni} baadae nilifanikiwa kumjua mwenye i.d hiyo, ni mtu wa Kanda ya Juu Kusini, mzaliwa wa Njombe, Mpambe wa wakubwa, Cybercrime inamlinda. Mtu huyo akaandika akimtabiria Mnyika kushindwa jimbo la Kibamba, na kumshambulia kuwa anajitenga na UKAWA na Mhe Lowassa. Mnyika Hakujibu.
4) Baaada ya Lowassa na Sumaye kupitishwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu, kuna waraka ulitembea mitandaoni ukieleza kuwa MNYIKA hajaridhika na hatua hiyo na kwamba anataka kujiengua CHADEMA, akatuhumiwa kwa mara nyingine. Mara hii, Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi akampigia simu kutaka uhakika wa jambo hilo, na hatimae Mwananchi la tarehe 10 July,2016 likaandika “SINA MPANGO WA KUHAMA CHADEMA” lakini wale wa kazi maalum ambao wanamuona MNYIKA kuwa ni kirusi waliendelea kumshambulia kuwa kwanini iwe kwa simu, kwanini asifanye Press.
5) Kadhia ya tano (5) na ya mwisho ni habari iliyoletwa na Ndugu yangu Frey Cosseny, kwa kuwa namfahamu Frey, nimebaki na butwaa, maana si rahisi kuwa habari hiyo ni uzushi wa kutungwa. Frey anaandika kuwa Mnyika kuondolea Naibu Katibu Mkuu Chadema Anayetajwa kumrithi ni Ruth Mollel, Mbunge mwenzangu wa Viti Maalum, najua ni msomi mzuri mwenye experience kubwa kwani ameshawahi kuwa Katibu Mkuu wizara mbalimbali pamoja na ofisi ya Waziri Mkuu lakini nikikumbuka Nguvu na Jitihada za Mnyika katika ujenzi wa CHADEMA na nafasi yake kupewa mtu aliyejiunga CHADEMA juzi tena baada ya LOWASSA kujiunga na CHADEMA, Napata mashaka makubwa kuwa uamuzi huo unaokuja ndani ya CHADEMA ni rational..? Naendelea kuona Ubeberu ukitawala ndani ya CHADEMA. Pamoja na yooote ambayo Mnyika amekuwa akihusishwa nayo, bado MNYIKA ni MTU ANAYEAMINIKA na litakuwa kosa lingine la kiufundi kwa CHADEMA kumng’oa mtu kama MNYIKA.
Najua watajitokeza watu watakaosema kuwa JULIANA hawezi kuitakia mema CHADEMA, na kwamba uamuzi huo ndio hasa wa kuushikilia, lakini mimi ni kama ilivyo kwa Mwalimu ambaye mpaka kufa kwake aliamini kuwa ili tuwe na CCM imara ni lazima tuwe na Upinzani makini. Mnyika ni Mpinzani makini, inawezekana kabisa ameacha harakati na kuamua kuwa mwanasiasa kamili lakini bado MNYIKA ni mtu hodari na mwenye mchango wa kipekee kwa siasa za nje yetu. Maana limeandika Gazeti la UMMA Tanzania la Julai 28 –Agosti 3, 2016 (mmiliki wake mnamjua) katika Ukurasa wake wa mbele “MNYIKA ATENGANISHA SIASA NA HARAKATI” na maelezo ya habari hiyo yakatolewa ukurasa wa tatu. Kwamba inaonekana harakati za akina TUNDU LISSU na akina KUBENEA ndio msingi wa siasa za Upinzani na kwamba kujitenga nazo ni UASI na USALITI. Jambo hili halikuwahi kuwa kweli na halitakuwa kweli.
Binafsi namjua MBATIZAJI, najua uwezo wake na umahiri wake kwenye siasa. Nimefanya nae mambo mengi katika ujenzi wa CHADEMA, alikuwa na wito na ailutimiza kwa bidii. Nitaumia na kuona kuwa ndoto zake haziji kuwa kweli. Na kwa wale wapambe wa wakubwa wanaotumwa kushambulia watu wasiokubalina na mabosi wao mitandaoni, ufike wakati mjipime na muweke mizania ya fikra zenu.
Nitaendelea kuwafunulia yale yaliyofunikwa maana mna viongozi mabingwa wa kufunika nanyi mmekuwa wafuasi msiohoji.