John Mnyika John, Mbatizaji anayetuhumiwa

Unapokuta anayejiita msomi wa PHD anajadili mtu badala ya issue nawasiwasi hata aliyemsahili kumpa fursa adimu ya kusomea PHD sidhani kama alijiridha hasa hasa. We are suppose to discuss ISSUES not PEOPLE kama huyu Muheshimiwa Mbunge wa ganda la ndizi
Kama ubunge alipata na kwa njia hizo hizo atapata PHD mkuu, hizi PhD kama za kitila na Bana haziishi mkuu!
 
Napita ila hizi harakati zote za kumpinga Mnyika ni kwa kuwa ni mfuasi mkubwa sana wa Dr Slaa hivyo wapiga dili lazima wampinge huyo mama mtu wa lowasa
 
Siku zote nimekuwa nikimuita Mbatizaji,

Ni mtu mwenye maarifa mengi, asiyejikweza na mwenye ustahamilivu wa kipekee, kwa sifa zake hizo alifanya watu wengi wampende, walio ndani ya CHADEMA hata nje ya CHADEMA, mimi ni miongoni mwao.

Katika Biblia ipo habari ya Mhubiri aliyependwa na YESU, pengine habari hiyo inawashangaza watu wengi kwani mhubiri huyo hakuwa mmoja wa madhehebu yetu maarufu, hakuwa Mluteri, wala mmedhodisti, wala mpentekoste, wala mwanglikana bali alikuwa MBATISTI. Aliitwa YOHANA MBATIZAJI, akibatiza watu kwa maji.

MBATIZAJI ninayetaka kumzungumzia leo anaitwa JOHN MNYIKA JOHN DALALI, Mbunge na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA…nitamzungumza ninavyomfahamu mimi na kuoanisha ufahamu huo na masaibu yanayomkuta hivi sasa.

Naomba nianze kwa kuelezea ninavyofahamu mchango wa MNYIKA ndani ya CHADEMA kwa ufupi kama ifuatavyo;

Katika mchakato wa Uandishi wa Katiba ya sasa ya CHADEMA mwaka 2006, uliwekwa utaratibu wa kuipitia Katiba ile ya 2004 kuona kama vipo vipengele vya kuvitumia kwenye Katiba mpya na baadae ukawekwa utaratibu wa waraka kwa wanachama kutoa maoni na kuyawasilisha makao makuu. Baada ya maoni hayo kuliundwa timu tatu (3) Timu moja ilihusu kuandika falsafa na itikadi ya chama ambayo Mwenyekiti alikuwa Prof Baregu na Katibu wake alikuwa Ndg John Mnyika.

Kuhusu falsafa ilinukuliwa kwa kiasi kikubwa kutoka kwenye Katiba ya 2004 na sehemu ya ITIKADI kwa mara ya kwanza ikaingizwa kwenye Katiba, hapo awali hakukuwa na kitu kinachojulikana kama itikadi ya CHADEMA.

Nimeanza na utangulizi huo kuwakumbusha Vijana wa CHADEMA ambao wanadhani ndio wameshiba itikadi ya CHADEMA kuliko MNYIKA kuwa hiyo inayoitwa ITIKADI yenyewe, imebuniwa na kuaririwa na MNYIKA.

Nguvu, uwezo, maarifa na mchango wa JOHN katika ujenzi wa CHADEMA ni wa kipekee, hakuna namna nitaelezea hatua za ukuaji na kuimarika kwa CHADEMA ikawa katika maelezo yangu hakuna jina la MNYIKA. Kwa ufupi hivyo ndivyo ninavyomfahamu Mnyika.

Nimeshtushwa na baadhi ya kadhia zinazomfika Kaka yangu huyu, nitaeleza baadhi;

1) Nadhani wengi wenu mtakumbuka kuwa Kaka yangu huyu amekuwa kimya kwa muda mrefu, ukimya wake ukapewa tafsiri kadha wa kadha kwa watu waliomzunguka. Ukimya wa MNYIKA ulianza pale tu MHE LOWASSA alipojiunga na CHADEMA, baada ya kuhama kwa Dr Slaa kulikotokana na ujio huo wa LOWASSA na kushambuliwa na GWAJIMA, na baadae andiko la Ndg Petro E. Mselewa Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA ambalo lilihusishwa na Mnyika, alituhumiwa kuwa anampinga LOWASSA na hivyo anapinga MABADILIKO. Ni kweli Dr Slaa ni Political Godfather wa Mnyika, na ni ukweli kuwa hasingelipenda kuona akina GWAJIMA wakimtukana hadharani ama kuungana nao kumkashifu kwa kila aina ya kashfa. Lakini kutokuwa tayari kuungana na akina Tundu Lissu, Mbowe na Gwajima kumshambulia Dr Slaa sio lazima kutafsiriwe kuwa ni UASI kwa Chama.

2) Tarehe 25th September, 2015 Mpambe mmoja wa wakubwa wa CHADEMA akaandika hapa JF John Mnyika, aidha ungana na wenzio au kubali kushindwa Kibamba Anatumia i.d ya Mpululu {alifunguliwa January 3, 2013 wakati wa sakata langu, ilikuwa ikinishambulia asubuhi na jioni} baadae nilifanikiwa kumjua mwenye i.d hiyo, ni mtu wa Kanda ya Juu Kusini, mzaliwa wa Njombe, Mpambe wa wakubwa, Cybercrime inamlinda. Mtu huyo akaandika akimtabiria Mnyika kushindwa jimbo la Kibamba, na kumshambulia kuwa anajitenga na UKAWA na Mhe Lowassa. Mnyika Hakujibu.

4) Baaada ya Lowassa na Sumaye kupitishwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu, kuna waraka ulitembea mitandaoni ukieleza kuwa MNYIKA hajaridhika na hatua hiyo na kwamba anataka kujiengua CHADEMA, akatuhumiwa kwa mara nyingine. Mara hii, Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi akampigia simu kutaka uhakika wa jambo hilo, na hatimae Mwananchi la tarehe 10 July,2016 likaandika “SINA MPANGO WA KUHAMA CHADEMA” lakini wale wa kazi maalum ambao wanamuona MNYIKA kuwa ni kirusi waliendelea kumshambulia kuwa kwanini iwe kwa simu, kwanini asifanye Press.

5) Kadhia ya tano (5) na ya mwisho ni habari iliyoletwa na Ndugu yangu Frey Cosseny, kwa kuwa namfahamu Frey, nimebaki na butwaa, maana si rahisi kuwa habari hiyo ni uzushi wa kutungwa. Frey anaandika kuwa Mnyika kuondolea Naibu Katibu Mkuu Chadema Anayetajwa kumrithi ni Ruth Mollel, Mbunge mwenzangu wa Viti Maalum, najua ni msomi mzuri mwenye experience kubwa kwani ameshawahi kuwa Katibu Mkuu wizara mbalimbali pamoja na ofisi ya Waziri Mkuu lakini nikikumbuka Nguvu na Jitihada za Mnyika katika ujenzi wa CHADEMA na nafasi yake kupewa mtu aliyejiunga CHADEMA juzi tena baada ya LOWASSA kujiunga na CHADEMA, Napata mashaka makubwa kuwa uamuzi huo unaokuja ndani ya CHADEMA ni rational..? Naendelea kuona Ubeberu ukitawala ndani ya CHADEMA. Pamoja na yooote ambayo Mnyika amekuwa akihusishwa nayo, bado MNYIKA ni MTU ANAYEAMINIKA na litakuwa kosa lingine la kiufundi kwa CHADEMA kumng’oa mtu kama MNYIKA.

Najua watajitokeza watu watakaosema kuwa JULIANA hawezi kuitakia mema CHADEMA, na kwamba uamuzi huo ndio hasa wa kuushikilia, lakini mimi ni kama ilivyo kwa Mwalimu ambaye mpaka kufa kwake aliamini kuwa ili tuwe na CCM imara ni lazima tuwe na Upinzani makini. Mnyika ni Mpinzani makini, inawezekana kabisa ameacha harakati na kuamua kuwa mwanasiasa kamili lakini bado MNYIKA ni mtu hodari na mwenye mchango wa kipekee kwa siasa za nje yetu. Maana limeandika Gazeti la UMMA Tanzania la Julai 28 –Agosti 3, 2016 (mmiliki wake mnamjua) katika Ukurasa wake wa mbele “MNYIKA ATENGANISHA SIASA NA HARAKATI” na maelezo ya habari hiyo yakatolewa ukurasa wa tatu. Kwamba inaonekana harakati za akina TUNDU LISSU na akina KUBENEA ndio msingi wa siasa za Upinzani na kwamba kujitenga nazo ni UASI na USALITI. Jambo hili halikuwahi kuwa kweli na halitakuwa kweli.

Binafsi namjua MBATIZAJI, najua uwezo wake na umahiri wake kwenye siasa. Nimefanya nae mambo mengi katika ujenzi wa CHADEMA, alikuwa na wito na ailutimiza kwa bidii. Nitaumia na kuona kuwa ndoto zake haziji kuwa kweli. Na kwa wale wapambe wa wakubwa wanaotumwa kushambulia watu wasiokubalina na mabosi wao mitandaoni, ufike wakati mjipime na muweke mizania ya fikra zenu.

Nitaendelea kuwafunulia yale yaliyofunikwa maana mna viongozi mabingwa wa kufunika nanyi mmekuwa wafuasi msiohoji.
nimesoma kwa umakini sana!! sikuelewa unakoelekea!! Je Mnyika bado kiongozi chadema? Je Mnyika umemwona akilalamika? wapi? Juzi alipopeleka kesi mahakama ya Afrika Mashariki alifanya kwa ajili ya nani?? Shonza Shonza jamani huko hawajakukumbuka hata kiduchu? Pole wee!
 
Uzi mzuri sana ila hakuna atakae changia hoja murua ila wote wataleta personal attac simply kwa sababu umeandika wewe juliana
 
Mimi niliona nyuzi nyingi za mawakala wa chama cha Magufuli, wakisema ati Mnyika atshamia chama cha Magufuli CCM kwa mkutano wake mkuu, mara kasema msimamo wake uko pale wa Lowassa ni Fisadi. Sasa leo Shonza umekuja na hekaya nyingine baada ya jaribio la kwanza kushindwa, na inakuwaje mnapenda kumsemea mtu aliye kimya na kutabiri uzuri na ubaya wake! Julian uliyo yaandika unayajua ila umetumia hila na hisia tu. #Tujengeukuta.
 
Umejitahidi kuandika walaka mrefu sana kwa bahati mbaya umechelewa kuandika. Now mnyika Yuko anaendelea na ukuta. Waambie waliokutuma kwamba jipangeni upya
 
Siku zote nimekuwa nikimuita Mbatizaji,

Ni mtu mwenye maarifa mengi, asiyejikweza na mwenye ustahamilivu wa kipekee, kwa sifa zake hizo alifanya watu wengi wampende, walio ndani ya CHADEMA hata nje ya CHADEMA, mimi ni miongoni mwao.

Katika Biblia ipo habari ya Mhubiri aliyependwa na YESU, pengine habari hiyo inawashangaza watu wengi kwani mhubiri huyo hakuwa mmoja wa madhehebu yetu maarufu, hakuwa Mluteri, wala mmedhodisti, wala mpentekoste, wala mwanglikana bali alikuwa MBATISTI. Aliitwa YOHANA MBATIZAJI, akibatiza watu kwa maji.

MBATIZAJI ninayetaka kumzungumzia leo anaitwa JOHN MNYIKA JOHN DALALI, Mbunge na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA…nitamzungumza ninavyomfahamu mimi na kuoanisha ufahamu huo na masaibu yanayomkuta hivi sasa.

Naomba nianze kwa kuelezea ninavyofahamu mchango wa MNYIKA ndani ya CHADEMA kwa ufupi kama ifuatavyo;

Katika mchakato wa Uandishi wa Katiba ya sasa ya CHADEMA mwaka 2006, uliwekwa utaratibu wa kuipitia Katiba ile ya 2004 kuona kama vipo vipengele vya kuvitumia kwenye Katiba mpya na baadae ukawekwa utaratibu wa waraka kwa wanachama kutoa maoni na kuyawasilisha makao makuu. Baada ya maoni hayo kuliundwa timu tatu (3) Timu moja ilihusu kuandika falsafa na itikadi ya chama ambayo Mwenyekiti alikuwa Prof Baregu na Katibu wake alikuwa Ndg John Mnyika.

Kuhusu falsafa ilinukuliwa kwa kiasi kikubwa kutoka kwenye Katiba ya 2004 na sehemu ya ITIKADI kwa mara ya kwanza ikaingizwa kwenye Katiba, hapo awali hakukuwa na kitu kinachojulikana kama itikadi ya CHADEMA.

Nimeanza na utangulizi huo kuwakumbusha Vijana wa CHADEMA ambao wanadhani ndio wameshiba itikadi ya CHADEMA kuliko MNYIKA kuwa hiyo inayoitwa ITIKADI yenyewe, imebuniwa na kuaririwa na MNYIKA.

Nguvu, uwezo, maarifa na mchango wa JOHN katika ujenzi wa CHADEMA ni wa kipekee, hakuna namna nitaelezea hatua za ukuaji na kuimarika kwa CHADEMA ikawa katika maelezo yangu hakuna jina la MNYIKA. Kwa ufupi hivyo ndivyo ninavyomfahamu Mnyika.

Nimeshtushwa na baadhi ya kadhia zinazomfika Kaka yangu huyu, nitaeleza baadhi;

1) Nadhani wengi wenu mtakumbuka kuwa Kaka yangu huyu amekuwa kimya kwa muda mrefu, ukimya wake ukapewa tafsiri kadha wa kadha kwa watu waliomzunguka. Ukimya wa MNYIKA ulianza pale tu MHE LOWASSA alipojiunga na CHADEMA, baada ya kuhama kwa Dr Slaa kulikotokana na ujio huo wa LOWASSA na kushambuliwa na GWAJIMA, na baadae andiko la Ndg Petro E. Mselewa Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA ambalo lilihusishwa na Mnyika, alituhumiwa kuwa anampinga LOWASSA na hivyo anapinga MABADILIKO. Ni kweli Dr Slaa ni Political Godfather wa Mnyika, na ni ukweli kuwa hasingelipenda kuona akina GWAJIMA wakimtukana hadharani ama kuungana nao kumkashifu kwa kila aina ya kashfa. Lakini kutokuwa tayari kuungana na akina Tundu Lissu, Mbowe na Gwajima kumshambulia Dr Slaa sio lazima kutafsiriwe kuwa ni UASI kwa Chama.

2) Tarehe 25th September, 2015 Mpambe mmoja wa wakubwa wa CHADEMA akaandika hapa JF John Mnyika, aidha ungana na wenzio au kubali kushindwa Kibamba Anatumia i.d ya Mpululu {alifunguliwa January 3, 2013 wakati wa sakata langu, ilikuwa ikinishambulia asubuhi na jioni} baadae nilifanikiwa kumjua mwenye i.d hiyo, ni mtu wa Kanda ya Juu Kusini, mzaliwa wa Njombe, Mpambe wa wakubwa, Cybercrime inamlinda. Mtu huyo akaandika akimtabiria Mnyika kushindwa jimbo la Kibamba, na kumshambulia kuwa anajitenga na UKAWA na Mhe Lowassa. Mnyika Hakujibu.

4) Baaada ya Lowassa na Sumaye kupitishwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu, kuna waraka ulitembea mitandaoni ukieleza kuwa MNYIKA hajaridhika na hatua hiyo na kwamba anataka kujiengua CHADEMA, akatuhumiwa kwa mara nyingine. Mara hii, Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi akampigia simu kutaka uhakika wa jambo hilo, na hatimae Mwananchi la tarehe 10 July,2016 likaandika “SINA MPANGO WA KUHAMA CHADEMA” lakini wale wa kazi maalum ambao wanamuona MNYIKA kuwa ni kirusi waliendelea kumshambulia kuwa kwanini iwe kwa simu, kwanini asifanye Press.

5) Kadhia ya tano (5) na ya mwisho ni habari iliyoletwa na Ndugu yangu Frey Cosseny, kwa kuwa namfahamu Frey, nimebaki na butwaa, maana si rahisi kuwa habari hiyo ni uzushi wa kutungwa. Frey anaandika kuwa Mnyika kuondolea Naibu Katibu Mkuu Chadema Anayetajwa kumrithi ni Ruth Mollel, Mbunge mwenzangu wa Viti Maalum, najua ni msomi mzuri mwenye experience kubwa kwani ameshawahi kuwa Katibu Mkuu wizara mbalimbali pamoja na ofisi ya Waziri Mkuu lakini nikikumbuka Nguvu na Jitihada za Mnyika katika ujenzi wa CHADEMA na nafasi yake kupewa mtu aliyejiunga CHADEMA juzi tena baada ya LOWASSA kujiunga na CHADEMA, Napata mashaka makubwa kuwa uamuzi huo unaokuja ndani ya CHADEMA ni rational..? Naendelea kuona Ubeberu ukitawala ndani ya CHADEMA. Pamoja na yooote ambayo Mnyika amekuwa akihusishwa nayo, bado MNYIKA ni MTU ANAYEAMINIKA na litakuwa kosa lingine la kiufundi kwa CHADEMA kumng’oa mtu kama MNYIKA.

Najua watajitokeza watu watakaosema kuwa JULIANA hawezi kuitakia mema CHADEMA, na kwamba uamuzi huo ndio hasa wa kuushikilia, lakini mimi ni kama ilivyo kwa Mwalimu ambaye mpaka kufa kwake aliamini kuwa ili tuwe na CCM imara ni lazima tuwe na Upinzani makini. Mnyika ni Mpinzani makini, inawezekana kabisa ameacha harakati na kuamua kuwa mwanasiasa kamili lakini bado MNYIKA ni mtu hodari na mwenye mchango wa kipekee kwa siasa za nje yetu. Maana limeandika Gazeti la UMMA Tanzania la Julai 28 –Agosti 3, 2016 (mmiliki wake mnamjua) katika Ukurasa wake wa mbele “MNYIKA ATENGANISHA SIASA NA HARAKATI” na maelezo ya habari hiyo yakatolewa ukurasa wa tatu. Kwamba inaonekana harakati za akina TUNDU LISSU na akina KUBENEA ndio msingi wa siasa za Upinzani na kwamba kujitenga nazo ni UASI na USALITI. Jambo hili halikuwahi kuwa kweli na halitakuwa kweli.

Binafsi namjua MBATIZAJI, najua uwezo wake na umahiri wake kwenye siasa. Nimefanya nae mambo mengi katika ujenzi wa CHADEMA, alikuwa na wito na ailutimiza kwa bidii. Nitaumia na kuona kuwa ndoto zake haziji kuwa kweli. Na kwa wale wapambe wa wakubwa wanaotumwa kushambulia watu wasiokubalina na mabosi wao mitandaoni, ufike wakati mjipime na muweke mizania ya fikra zenu.

Nitaendelea kuwafunulia yale yaliyofunikwa maana mna viongozi mabingwa wa kufunika nanyi mmekuwa wafuasi msiohoji.
Kwa kuwa hujui Biblia ninakushauri sana acha kutumia maandiko vibaya. Hakuna mahali popote panapoonesha Yohana Mbatizaji kupendwa na Yesu. Fanya siasa zako achana na maandiko matakatifu. Biblia iko wazi: Kila alitajaye jina la Bwana aache uovu. Je, wewe umeacha uovu wako? Juliana Shonza. Fanya siasa zako na akina John Mnyika. Acha kebehi kwa neno la Mungu. Mungu hachangamani na dhambi wewe mwanamke. What audacity do you have Juliana Shonza?
 
Anajina la I.D "siasa basi"
Amejiunga JF; tarehe 10 July 2016.

Bila shaka ni katika zile ajira mpya,

Reply: 177
likes: 261
Trophies: 80.

Ndio ajira zenyewe hizi...!!!
Toka kujiunga kwako JF nikipi cha maana ulichokiandika humu zaidi ya pumba na umbea tu. Siasa nimeanza kabla yako wakati unaingia Chadema na kamasi zako. Leo unajifanya mwalimu endelea kukaa huko kwa matapeli wenzako, ya Chadema hayakuhusu, waachie Wanachadema.
 
Hivi karibuni nitawaletea mkakati unaoendelea ya kuwaondoa wapambe wa Dr Silaa ktk Secretariat mpya ya chadema, na kwanini salum mwalimu alipandishwa ghafla toka vodacom na kuwa NKM cdm Mara baada ya kuondolewa channel ten kuna uhusiano ipi kati ya Chanel10 vodacom na Cdm
Makubwa haya!!!!
 
Don't confuse John, the Baptist with John, the Disciple! Yohana Mbatizaji wala hakuishi na Bw. Yesu kwa kipindi kirefu; sana sana baada ya kumbatiza Yesu haukupita muda akakatwa kichwa na Herodi kwa raha za Herodia yule mwanamke, ashakum sio matusi, "malaya". John, au yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu ni John yule mdogo, mtume, na ambaye miongoni mwa mengi wasifu wake ni huu:-
  1. Aliandika 1 Yoh na 2 Yoh.
  2. Aliandika Ufunuo akiwa huko kisiwani Patmo - Ugiriki ya leo.
  3. Ndiye mtume wa mwisho wa Bw. Yesu kufariki na alifariki kwa uzee - hakuuwawa kama wengine akina Stefano, n.k.
Nimeona niweke tu rekodi sawa maana Shetani hutenda kazi zake kwa hila sana kwa lengo la kupotosha; hatakiwi kuachiwa nafasi pale anapojaribu kupotosha maandiko.
Huyu Juliana Shonza hajui maandiko. Alisikika pia bungeni akisema kuna wafalme wawili hapa duniani ambao ni Bwana Yesu na mtume Muhamadi. Jamani mwambieni huyo mwanamke asijitafutie balaa. Kama ni siasa afanye siasa. Hajui maandiko na kwa sababu hiyo anatumika na Shetani kupotosha watu. Ajue Mungu hataacha kuwahukumu watu wa namna hii kama Juliana Shonza kuwa hawana makosa.
 
Yawezekana wewe ni mjuzi hasa wa Biblia, na unacho kipawa cha kipekee cha kutambua mashetani na kuwakemea. Lakini jihadhari kuwa Nabii wa Zama za Mwisho. Maana unachokipinga na kukisahihisha sikioni. Inawezekana unao ushahidi wa wazi unaotokana na maneno ya Biblia ama Kitabu chochote kilicho na maneno ya Mungu kuwa YESU hakuwahi kumpenda MBATIZAJI.

hata udhani kuwa nimekosea ama nimepotosha kusema kuwa MBATIZAJI alipendwa na YESU. Basi tuambie wewe kuwa MBATIZAJI alichukiwa na YESU na kwamba nilichokisema sio sahihi.

Rejea maneno haya;

Ingawa Yohana alitumiwa sana na Mungu na kuwa maarufu sana na kupendwa na watu, alijua yeye si kitu kulinganishwa na Yesu. Basi, kila wakati alimtukuza Bwana wake, kama ifuatavyo:​

"..Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba, bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.." (Mathayo 3:11).​
Hayo maneno ya rejea ni ya kwako. Juliana Shonza. Achana na Biblia. Fanya siasa wewe mwanamke.
 
CCM imebeba majitu yasiyojiweza, sasa mleta mada anatofauti gani na yule mbunge wa Kutaka kulia? Na yule wa sanamu la diamond au yule wa kilimo cha bhangi? CCM inajiua yenyewe kwa kushindwa kutengeneza wabunge na viongozi wanaoweza kujenga hoja na kuchambua mambo kwa kina matokeo ndio watu kama hawa nao ni wabunge! Huyu unategemea ataweza kujenga hoja dhidi ya watu kama kina lucy, ruth, anatropia, bulaya, mdee and co!!!
Hana kitu. Nilimdharau sana aliposimama na kusema Bwana Yesu ni mfalme wa dunia. Ovyo sana huyu mwanamke.
 
Heheeheee! Hata kama uliwahi kuingia huko wewe ni ng'ombe uliekatwa mkia na baada ya awamu hii huingii tena mjengoni huna mkia dada, fanya kuweka akili yako kwenye mambo ya maendeleo achana na Mnyika/chadema. Ng'ombe usie na mkia ni tusi kweli rais kawaweza wenye ulafi wa madaraka.
 
Huyu Juliana Shonza hajui maandiko. Alisikika pia bungeni akisema kuna wafalme wawili hapa duniani ambao ni Bwana Yesu na mtume Muhamadi. Jamani mwambieni huyo mwanamke asijitafutie balaa. Kama ni siasa afanye siasa. Hajui maandiko na kwa sababu hiyo anatumika na Shetani kupotosha watu. Ajue Mungu hataacha kuwahukumu watu wa namna hii kama Juliana Shonza kuwa hawana makosa.
Juzi kati alianzisha uzi mwingine hapa akijitapa jinsi alivyo msomi tena katika umri "mdogo" pamoja na kutudokezea imani yake ambapo alitueleza yeye ni MKRISTO MPENTEKOSTE. Ni utoto fulani unamsumbua huyo ni wa kusamehe tu. Hilo la Mtume Muhamad (SAW) sina ujuzi nalo ila hilo la Bwana Yesu; yeye mwenye alitamka waziwazi wala hakuficha - UFALME WANGU SIO WA ULIMWENGU HUU.

Sasa kama ataibuka mtu akidai ufalme wa Yesu ni wa dunia hii (wakati mfalme wa dunia maandiko yamemwelezea waziwazi ni nani) kwa hakika mtu huyo akili yake punje ya haradali kubwa. Huyo wala sio wa kufanya naye mashindano ya maneno maana ni kupoteza tu muda.
 
Hivi karibuni nitawaletea mkakati unaoendelea ya kuwaondoa wapambe wa Dr Silaa ktk Secretariat mpya ya chadema, na kwanini salum mwalimu alipandishwa ghafla toka vodacom na kuwa NKM cdm Mara baada ya kuondolewa channel ten kuna uhusiano ipi kati ya Chanel10 vodacom na Cdm
Fanya haraka kuuanika unafiki wa hawa wanaharakati uchwara.
 
Umejiunga 2012 una likes 99 hujishangani?
Nami nimeshangaa na sio kwamba hapost threads ana post sana ila nadhani huko Facebook ana members kibao! Hili jamvi naona limemzidi kimo!
 
Binafsi namjua MBATIZAJI, najua uwezo wake na umahiri wake kwenye siasa. Nimefanya nae mambo mengi katika ujenzi wa CHADEMA, alikuwa na wito na ailutimiza kwa bidii. Nitaumia na kuona kuwa ndoto zake haziji kuwa kweli.
Njia 'nzuri' ingekuwa kumshauri aungane na wewe huko ulipo. Kuna 'fursa' zaidi!
 
Back
Top Bottom