Muke Ya Muzungu
JF-Expert Member
- Jun 17, 2009
- 3,444
- 264
- Thread starter
- #81
sijakataa kwamba hana akili, hiyo wengi wanakubali, ila amesomaje. Si amesomeshwa na hela zetu za kodi? mashaka anaaribu juhudi za jk za kuleta maendeleo. jk analetawawekezaji, yeye anawaita wawekezaji uchwara. ndo maana nasema kasoma lakini hajaelemika. angekuwa mtu mwenye upeo mdogo asingetamka hayo maneno. huyu ni fisadi wa wamarekani tu, au pengine anatumiwa na CHADEMA. kwa maana vijana wa ccm kama nape, january ni watu makini sana
Watu wanaoeshimika sana kwenye hili jamvi ni Mshirika wangu William Malecela ambaye aliwahi kunisimulia mengi sana kuhusu Mashaka, akisema kwamba ni mmoja wa vijana wa kuogopwa licha ya ukweli kwamba wote wawili tunamfahamu huyu kijana tangu akia kijana mdogo sana. Mimi pamoja na Mh. William Malecela tumemuona huyu kijana tangu mdogo pale Ukonga Segerea. William kwa sasa hivi ni mshirika wa karibu wa Yohana Mashaka, na nadhania wote wanajitayarisha kurudi 2015, lich aya yote, mchumba wa mashaka ana undugu na William Malecella. Mheshimiwa Pinda, Rais Kikwete, Bernanrd Membe, Dr. Wilbrod Slaa, Dr. John Magufuli, Lowassa na hata Gavana wa BoT, Ndullu, ni baadhi tu ya viongozi wa kitanzania wanaomwangalia Mashaka kwa umakini. Lau Masha alishawahi kupitia hata faili lake uhamiaji kutaka kujua kama kweli ni mtanzania. Kwa hiyo kama bado kuna mtu anakuwa na wasiwasi kuhusu umakini wa Yohana mashaka, kama alivyo Fisadi-Original, basi huyo mtu inabidi ajiulize maswali ya msingi.
Wewe unayejiita FISADI_ORIGINAL. Nina uhakika kwamba unaumwa kwa maana mada yao haieleweki. Kwanza haumjui Yohanna Mashaka. Huyu mtoto/kijana ni mstaarabu sana, mwenye upendo, heshima na bidii ya hali ya juu. nimemfahamu huyu kijana kutokea Segerea ambako amekulia. Kati ya vijana wachache walipendwa kutokana na ustaarabu wao mashaka ni wa kwanza. Nakumbuka sana akisoma Kenya miaka ya 90, akiwa na umri wa miaka kati ya 14-16. Mashaka alikuwa ni mfano wa kuigwa na vijana wenzake. Uwezo wake wa kufikiri hauna mjadala, na kwa anayemfahamu vizuri, mashaka ana uwezo mkubwa sana wa kujenga na kutetea hoja zake. Mashaka tangu utotoni kila mtu alimfahamu kwamba ni Jinias . kwa hiyo mtu anaposema kabisa bila aibu kwamba ameandikiwa makala zake, basi huyo mtu atakuwa ni chizi fulani. Kama kuna ma jenius tanzania, bila shaka mashaka ni mmoja wao.
Zitto, Mnyika, Alima Mdee, Tindu Lissu watafurahi sana kuwa na kijana kama mashaka upande wao. huyu siyo mtu wa kubabaishwa. Uzalendo wake ni wa hali ya juu, hasa katika kutetea maslahi ya kitaifa. kwa hiyo mimi sioni sababu ya msingi ya kumuita fisadi kwa sababu kapinga kuwepo kwa wawekezaji uchwara. Kwa yeyote anayefahamu nchi ya marekani, ubaguzi ni wa hali ya juu, na nafasi za investment banking nyingi ni za wazungu. kwa hiyo mweusi tena mwafrika ili aingie, ina maana mtu huyo anakubalika sana. Sina shaka kwamba Mashaka ameonyesha uwezo mkubwa ndo maana kapata nafasi ya kuingia kwenye masoko ya kifedha. kwa maana hiyo fisadi original nitakuita una chuki binafsi au wivu.
Nawakilisha