Alvajumaa
JF-Expert Member
- Jul 5, 2018
- 5,471
- 6,913
Watujuze wadauHuyo Gervas Stephano vipi sasa hivi ana hali gani?
Watujuze wadauHuyo Gervas Stephano vipi sasa hivi ana hali gani?
Ni kaada wa mtiifu wa ccmAnayejua ndugu Gervas Stephano alipo na shughuli anayofanya kwa sasa atujuze.
Hili la julai 2013 mnalikumbuka? Kazi hii aliishajiandaa kwahiyo tuwe wapole na tuendelee kuunga mkono kwa ustawi wa taifa lake letu lao?Katika hali inayoonyesha kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, anautamani urais, amesema anaweza kutangaza nia hiyo kama atakidhi masharti yatakayowekwa kwenye Katiba mpya.
Alisema iwapo Katiba ijayo itakuja na sifa ambazo atakidhi vigezo kuna uwezekano mkubwa wa kuwania nafasi hiyo na kwamba iwapo atapungukiwa sifa zinazohitajika kwa mujibu wa Katiba hataingia kwenye kinyang'anyiro hicho.
Dk. Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wazee wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa ‘Mshikamano Saccos', muda mfupi baada ya mzee Paschal Nyambibo (87) kumsihi agombee nafasi hiyo mwaka 2015 kutokana na sifa zake za uchapakazi ndani ya serikali.
Nyambibo alisema kutokana na uwajibikaji mzuri aliouonyesha Dk. Magufuli tangu mwaka 2000 akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na katika wizara mbalimbali, Watanzania wamekuwa na imani kubwa na uwajibikaji wake na kwamba anastahili kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ifikapo mwaka 2015.
Licha ya kauli hiyo kusababisha minong'ono mingi kwa wazee waliohudhuria kikao hicho, Dk. Magufuli alionekana kutuliza hali hiyo kwa kusema isubiriwe Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano iwapo itakuwa na masharti ambayo yatamfanya kujitathimini iwapo ana sifa za kugombea au vinginevyo.
Hata hivyo, Dk. Magufuli hakusita kuonyesha hisia zake za kukerwa na baadhi ya wananchi wanaobeza maendeleo aliyotekeleza katika jimbo lake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge.
Alimshutumu hadharani aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Chato kabla ya kuhamishiwa wilayani Mbogwe, Gervas Stephano, kuwa hana shukrani.
Dk. Magufuli alimwelezea katibu huyo kuwa hana fadhila kutokana na mambo mengi aliyomtendea tangu akiwa katibu wa ofisi yake ya jimbo ambapo alimsaidia kupanda ngazi na kuwa Katibu wa CCM wilaya Chato, Kwimba, Kasulu, Kilosa na kurejea tena Chato kabla ya kuhamishiwa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kuendelea na wadhifa huo.
"Tatizo lenu watu wa Chato hamna shukrani, mambo mengi nimefanya hapa Chato, lakini yote mnaona ziro hata niliowasaidia kama Gervas naye sasa hivi ananiponda lakini nawashukuru sana wazee wangu kwa kunikumbusha niliyoyafanya kwenye jimbo letu kupitia risala yenu nzuri," alisema Dk. Magufuli.
"Kutokana na hali hiyo ninawazawadia Sh. 1,000,000 mfanye sherehe ya kujipongeza kwa kuwa natambua mmejitesa sana mpaka kufanikisha kikao hiki cha leo&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];na kwa kuwa hamna mradi wowote wa kuwaingizia kipato kama wazee, ninaahidi kuwapa Sh. 3,000,000 kutoka mfuko wa jimbo, ili muanzishe walau saccos ya kukopeshana," alisema.
Baadhi ya viongozi na wananchi wamekuwa wakilitaja mara kwa mara jina la Waziri Magufuli miongoni mwa watu wanaodhaniwa kutaka kugombea nafasi ya urais wa Tanzania mwaka 2015, ingawa mwenyewe amekuwa akikanusha uvumi huo.
Mbali na Dk. Magufuli, wengine ndani ya CCM wanaotajwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye anajiita mtaji wa urais; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Ushirikiano wa Kimataifa &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG];CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe, ambaye alipata kusema anasubiri kuiteshwa na Mungu kuwania nafasi hiyo.
Chanzo: Nipashe
==============
UPDATE (1):
Tarehe 18, Feb 2015: Kwa mujibu wa magazeti ya leo; Magufuli katangaza nia kutaka kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano
Munakumbuka hizi comments kweli?CCM hawawezi kumteua huyu apeperushe bendera ya urais maana atawafunga wote waliofanya ubadhilifu. Wanachofanya ni kumwekam2 atakayelinda mfumo wa kifisadi, wanataka m2 subjective sio objective kama Magufuli.
Aisee Asiyependwa ndiye aliyekuja sasakumbe unapenda waongeaji!! kwa taarifa yako magufuli.....hapendwi ndani ya ccm EITHER.....JK na Pinda wanamuogopa na hakuna mwana CCM ndani ya CC atakayempitisha
kingine mkuu Magufuli siyo injinia.......by his age he will never be!!!! ni mkemia
Upo mzizi wa mbuyu? NakusalimuHuyu atakuwa dhaifu kuliko JK! Mambo mengi ya kitaifa ananyamazia hatujui msimamo wake...kwanza toka lini injinia akawa raisi! Akajenge madaraja huko!
Heko ulimjua vizuriNdo uzuri wa jamaa,hanaga kuzunguka point na kuremba.
haya mawazo yako yalikuwa nega kinoma😂😂Huyu atakuwa dhaifu kuliko JK! Mambo mengi ya kitaifa ananyamazia hatujui msimamo wake...kwanza toka lini injinia akawa raisi! Akajenge madaraja huko!
Rejea andiko lako unabii umetimiaCCM hawawezi kumteua huyu apeperushe bendera ya urais maana atawafunga wote waliofanya ubadhilifu. Wanachofanya ni kumwekam2 atakayelinda mfumo wa kifisadi, wanataka m2 subjective sio objective kama Magufuli.
Bernard Membe, ambaye alipata kusema anasubiri kuiteshwa na Mungu kuwania nafasi hiyo.
Anayejua ndugu Gervas Stephano alipo na shughuli anayofanya kwa sasa atujuze.
DuuhTo be realistic, huyu anakurupuka katika maamuzi! Anakuwa driven na hisia na si reasoning! Dikteita mkubwa hafai! Anatoa maamuzi kwenye jukwaa watu wamsikie. Sawa na Mrema enzi zake. Kweli nchi hii na vichaa wa siasa!
Magufuli siyo tu hana nguvu ndani ya Chama , bali pia Hana sifa za kuwa Rais. Rais lazima awe mtu mwenye uwezo aw kujenga Hoja , siyo wa kukariri kilometer au idadadi ya Samaritan haharini. Anatakiwa mtu mwenye uadilifu usiotiliwa shaka. Magufuli si madilifu, licha ya kupiga makelele, ni mpokeaji mkubwa we rushwa kutoka kwa makandarasi. Vile vitisho anayo toa kwa makandarasi ndiyo mbinu yake ya kujizolea milungula kutoka Kwao. Ni mtu asiyesikiliza ushauri wowote kutoka kwa watalaamu wake, kwa vile anadhani anajua kila kitu. Ndiyo maana Aliza nyumba zote za serikali mpaka za hospitali na Vito vya polisi na kuuza nyumba za serikali kwa hawala na nudge zake walikuwa watumishi aw serikali. Mbali na hayo wizard yake inashindwa kueleza ziliko shs 260 bn zilizotengwa kulipa madeni ya makandarasi ambayo haya kulipwa na fedha hazijulikani zilipo. Kama hayo yote anayafanya akiwa waziri je akiwa itakuwaje. Hafar Hafai Hafai.
..kashfa yake ya kuuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupa na kusababisha hasara ya mabilioni kama siyo trilioni ni ushahidi kwamba Dr.Magufuli hafai kwa nafasi ya uraisi.
..lingine ni tabia yake ni kiburi na ubabe katika utekelezaji wa majukumu yake. kuna wakati alivunja kituo cha mafuta kule Mwanza bila kuzingatia ushauri wa wataalamu. matokeo yake serikali ikaburuzwa mahakamani na ikaamuliwa kwamba mwenye kituo cha mafuta alipwe sh bilioni 14.
..vilevile Magufuli kwa kauli zake ktk mikutano mbalimbali inaelekea haamini ktk siasa za ushindani. yeye siku zote hutoa kauli za kukashifu wapinzani, na kudanganya wananchi waziwazi kuhusu mfumo wetu wa vyama vingi.
..mwisho, Dr.Magufuli hana busara na umakini unaotakiwa kuwa nao head of state. chukulia kitendo chake cha kwenda Kenya wakati wa uchaguzi na kumpigia kampeni Raila Odinga. Lile lilikuwa ni kosa kubwa sana la kidiplomasia kwa kuzingatia kwamba Dr.Magufuli ni waziri mwandamizi ktk serikali ya Tanzania. Kidiplomasia kitendo cha Magufuli kinaweza kabisa kuchukuliwa kama Tanzania kuingilia uchaguzi wa Kenya.
cc domokaya, Camalillo, Mojo, Mahebe, Mp Kalix2