John Magufuli: Ninautamani urais!

John Magufuli: Ninautamani urais!

Akinambia kuwa ile kauli ya kumwambia JK aongeze safari za nje kuomba misaada ni ya kinafiki tu, ntamuunga mkono. Ila akisema alikuwa anamaanisha hafai kwani yeye atakuwa analala aiport.
 
Kwa elimu yangu ya saikolojia John pombe magufuli hafai kuwa Raisi, kwanza hana busara, hana hekima, hana subira, hana uadilifu,
Kwa mnaoijua hii fani: hii kitu inahusu mabibo ya korosho au nakosea? Ningemshauri aombe kazi ya kufundisha chemistry pale Mlimani, kwa mtazamo wangu hii ingekuwa retirement plan nzuri kuliko kujaribu urais ambao ataukosa na ngeu juu!
 
Kitendo cha kukubali kuuza nyumba za serikali kinamuondolea sifa zote
 
andate ndio huyo huyo Madelu Mwigulu Nchemba ninaye mzungumzia.
Kuna wanaCCM wenzake wanasema anafaa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM kwa kuwa ataweza kupambana na CHADEMA!!!

Hao wanaosema hivyo watakuwa na vichaa.
 
vasco dagama? ckujua kama amepewa jina hili baba prince. ila ka magufuli noma? ila wale hawawezi kukaweka mana katawatawanya.
 
Ana maamuzi magumu anaweza bkasimamia vyema maendeleo lakn maamuz yake yanaweza yakaumiza wengne ama kuiingza nch vitani
 
Source NIPASHE 05/07/2013

Katika hali inayoonyesha kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, anautamani urais, amesema anaweza kutangaza nia hiyo kama atakidhi masharti yatakayowekwa kwenye Katiba mpya.

Alisema iwapo Katiba ijayo itakuja na sifa ambazo atakidhi vigezo kuna uwezekano mkubwa wa kuwania nafasi hiyo na kwamba iwapo atapungukiwa sifa zinazohitajika kwa mujibu wa Katiba hataingia kwenye kinyang'anyiro hicho.

Dk. Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wazee wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa ‘Mshikamano Saccos', muda mfupi baada ya mzee Paschal Nyambibo (87) kumsihi agombee nafasi hiyo mwaka 2015 kutokana na sifa zake za uchapakazi ndani ya serikali.

Nyambibo alisema kutokana na uwajibikaji mzuri aliouonyesha Dk. Magufuli tangu mwaka 2000 akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na katika wizara mbalimbali, Watanzania wamekuwa na imani kubwa na uwajibikaji wake na kwamba anastahili kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ifikapo mwaka 2015.

Licha ya kauli hiyo kusababisha minong'ono mingi kwa wazee waliohudhuria kikao hicho, Dk. Magufuli alionekana kutuliza hali hiyo kwa kusema isubiriwe Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano iwapo itakuwa na masharti ambayo yatamfanya kujitathimini iwapo ana sifa za kugombea au vinginevyo.

Hata hivyo, Dk. Magufuli hakusita kuonyesha hisia zake za kukerwa na baadhi ya wananchi wanaobeza maendeleo aliyotekeleza katika jimbo lake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge.

Alimshutumu hadharani aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Chato kabla ya kuhamishiwa wilayani Mbogwe, Gervas Stephano, kuwa hana shukrani.

Dk. Magufuli alimwelezea katibu huyo kuwa hana fadhila kutokana na mambo mengi aliyomtendea tangu akiwa katibu wa ofisi yake ya jimbo ambapo alimsaidia kupanda ngazi na kuwa Katibu wa CCM wilaya Chato, Kwimba, Kasulu, Kilosa na kurejea tena Chato kabla ya kuhamishiwa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kuendelea na wadhifa huo.

"Tatizo lenu watu wa Chato hamna shukrani…mambo mengi nimefanya hapa Chato, lakini yote mnaona ziro…hata niliowasaidia kama Gervas naye sasa hivi ananiponda…lakini nawashukuru sana wazee wangu kwa kunikumbusha niliyoyafanya kwenye jimbo letu kupitia risala yenu nzuri," alisema Dk. Magufuli.

"Kutokana na hali hiyo ninawazawadia Sh. 1,000,000 mfanye sherehe ya kujipongeza kwa kuwa natambua mmejitesa sana mpaka kufanikisha kikao hiki cha leo…na kwa kuwa hamna mradi wowote wa kuwaingizia kipato kama wazee, ninaahidi kuwapa Sh. 3,000,000 kutoka mfuko wa jimbo, ili muanzishe walau saccos ya kukopeshana," alisema.

Baadhi ya viongozi na wananchi wamekuwa wakilitaja mara kwa mara jina la Waziri Magufuli miongoni mwa watu wanaodhaniwa kutaka kugombea nafasi ya urais wa Tanzania mwaka 2015, ingawa mwenyewe amekuwa akikanusha uvumi huo.

Mbali na Dk. Magufuli, wengine ndani ya CCM wanaotajwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye anajiita mtaji wa urais; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Ushirikiano wa Kimataifa –CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe, ambaye alipata kusema anasubiri kuiteshwa na Mungu kuwania nafasi hiyo.

Naona siasa za bongo au magamba zinatupeleka pabaya kwani nilkuwapo katika mkutano huo wa wazee wa Chato na yaliyoongelewa:

1. Mwenyekiti Mzee Samwel Bigambo kwa niaba ya Wazee wa Chato alisoma risala kumpongeza kwa mema aliyowafanyia kama Mbunge kwa kipindi chote cha kuwatumikia.

2. Makamu Mwenyekiti wa Wazee hao Mzee Saimon Mayeka kwa pamoja na wazee wenzake walimtunuku kuwa Mmoja wa Wazee wa Chato.

3. Katika hotuba yake (Magufuli) hakuna sehemu yeyote aliyotaja kuhusu kugombea Urais ifikapo mwaka 2015 na ndiyo maana utaona ni gazeti moja tu la Niapshe la leo,tarehe 5 Julai 2013 ndilo limeandika mambo hayo "Magufuli:Ninautamani Uraisi" kitu ambacho ni uongo na uzushi au uchochezi wa kisiasa kwa vile wameona sehemu nyingi amekanusha hasa ile ya Samwel Sitta kumtungia uongo wa kuchangia ujenzi wa kanisa kule Igoma, Mwanza wakati si kweli!!

4. Kumekuwepo na mbinu chafu sana za kumfuatilia kila anachoongea ili mradi tu wapate pa kuanzia kumchafua ama kutumia media n.k

5. Sasa basi aliyeandika habari hii hasa atupatie hata clip ya sauti ya Magufuli au atupe hotuba yote ya Magufuli aliyoiandika kwa wazee wa Chato. Na isitoshe risal ya Wazee wa Chato ipo na haikumsemea agombee uraisi. Ni vizuri kuwa taarifa za uhakika kuliko kukurupuka kuandika vitu vya kuchochea au kumuahribia mtu jina - tunaomba hivyo vielelezo!

6. Nasema haya kwa vile nikuwepo katika mkutano huo na nakanusha kilichoandikwa ni uongo na ndiyo maana ni gazeti moja tu limeweza kuandika uongo huo.
 
Source NIPASHE 05/07/2013

Katika hali inayoonyesha kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, anautamani urais, amesema anaweza kutangaza nia hiyo kama atakidhi masharti yatakayowekwa kwenye Katiba mpya.

Alisema iwapo Katiba ijayo itakuja na sifa ambazo atakidhi vigezo kuna uwezekano mkubwa wa kuwania nafasi hiyo na kwamba iwapo atapungukiwa sifa zinazohitajika kwa mujibu wa Katiba hataingia kwenye kinyang'anyiro hicho.

Dk. Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wazee wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa ‘Mshikamano Saccos', muda mfupi baada ya mzee Paschal Nyambibo (87) kumsihi agombee nafasi hiyo mwaka 2015 kutokana na sifa zake za uchapakazi ndani ya serikali.

Nyambibo alisema kutokana na uwajibikaji mzuri aliouonyesha Dk. Magufuli tangu mwaka 2000 akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na katika wizara mbalimbali, Watanzania wamekuwa na imani kubwa na uwajibikaji wake na kwamba anastahili kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ifikapo mwaka 2015.

Licha ya kauli hiyo kusababisha minong'ono mingi kwa wazee waliohudhuria kikao hicho, Dk. Magufuli alionekana kutuliza hali hiyo kwa kusema isubiriwe Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano iwapo itakuwa na masharti ambayo yatamfanya kujitathimini iwapo ana sifa za kugombea au vinginevyo.

Hata hivyo, Dk. Magufuli hakusita kuonyesha hisia zake za kukerwa na baadhi ya wananchi wanaobeza maendeleo aliyotekeleza katika jimbo lake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge.

Alimshutumu hadharani aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Chato kabla ya kuhamishiwa wilayani Mbogwe, Gervas Stephano, kuwa hana shukrani.

Dk. Magufuli alimwelezea katibu huyo kuwa hana fadhila kutokana na mambo mengi aliyomtendea tangu akiwa katibu wa ofisi yake ya jimbo ambapo alimsaidia kupanda ngazi na kuwa Katibu wa CCM wilaya Chato, Kwimba, Kasulu, Kilosa na kurejea tena Chato kabla ya kuhamishiwa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kuendelea na wadhifa huo.

"Tatizo lenu watu wa Chato hamna shukrani…mambo mengi nimefanya hapa Chato, lakini yote mnaona ziro…hata niliowasaidia kama Gervas naye sasa hivi ananiponda…lakini nawashukuru sana wazee wangu kwa kunikumbusha niliyoyafanya kwenye jimbo letu kupitia risala yenu nzuri," alisema Dk. Magufuli.

"Kutokana na hali hiyo ninawazawadia Sh. 1,000,000 mfanye sherehe ya kujipongeza kwa kuwa natambua mmejitesa sana mpaka kufanikisha kikao hiki cha leo…na kwa kuwa hamna mradi wowote wa kuwaingizia kipato kama wazee, ninaahidi kuwapa Sh. 3,000,000 kutoka mfuko wa jimbo, ili muanzishe walau saccos ya kukopeshana," alisema.

Baadhi ya viongozi na wananchi wamekuwa wakilitaja mara kwa mara jina la Waziri Magufuli miongoni mwa watu wanaodhaniwa kutaka kugombea nafasi ya urais wa Tanzania mwaka 2015, ingawa mwenyewe amekuwa akikanusha uvumi huo.

Mbali na Dk. Magufuli, wengine ndani ya CCM wanaotajwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye anajiita mtaji wa urais; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Ushirikiano wa Kimataifa –CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe, ambaye alipata kusema anasubiri kuiteshwa na Mungu kuwania nafasi hiyo.

Last edited by a moderator:

Alisema iwapo Katiba ijayo itakuja na sifa ambazo atakidhi vigezo kuna uwezekano mkubwa wa kuwania nafasi hiyo na kwamba iwapo atapungukiwa sifa zinazohitajika kwa mujibu wa Katiba hataingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Dk. Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wazee wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa ‘Mshikamano Saccos’, muda mfupi baada ya mzee Paschal Nyambibo (87) kumsihi agombee nafasi hiyo mwaka 2015 kutokana na sifa zake za uchapakazi ndani ya serikali.

Nyambibo alisema kutokana na uwajibikaji mzuri aliouonyesha Dk. Magufuli tangu mwaka 2000 akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na katika wizara mbalimbali, Watanzania wamekuwa na imani kubwa na uwajibikaji wake na kwamba anastahili kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ifikapo mwaka 2015.

Licha ya kauli hiyo kusababisha minong’ono mingi kwa wazee waliohudhuria kikao hicho, Dk. Magufuli alionekana kutuliza hali hiyo kwa kusema isubiriwe Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano iwapo itakuwa na masharti ambayo yatamfanya kujitathimini iwapo ana sifa za kugombea au vinginevyo.

Hata hivyo, Dk. Magufuli hakusita kuonyesha hisia zake za kukerwa na baadhi ya wananchi wanaobeza maendeleo aliyotekeleza katika jimbo lake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge.

Alimshutumu hadharani aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Chato kabla ya kuhamishiwa wilayani Mbogwe, Gervas Stephano, kuwa hana shukrani.

Dk. Magufuli alimwelezea katibu huyo kuwa hana fadhila kutokana na mambo mengi aliyomtendea tangu akiwa katibu wa ofisi yake ya jimbo ambapo alimsaidia kupanda ngazi na kuwa Katibu wa CCM wilaya Chato, Kwimba, Kasulu, Kilosa na kurejea tena Chato kabla ya kuhamishiwa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kuendelea na wadhifa huo.

“Tatizo lenu watu wa Chato hamna shukrani…mambo mengi nimefanya hapa Chato, lakini yote mnaona ziro…hata niliowasaidia kama Gervas naye sasa hivi ananiponda…lakini nawashukuru sana wazee wangu kwa kunikumbusha niliyoyafanya kwenye jimbo letu kupitia risala yenu nzuri,” alisema Dk. Magufuli.

“Kutokana na hali hiyo ninawazawadia Sh. 1,000,000 mfanye sherehe ya kujipongeza kwa kuwa natambua mmejitesa sana mpaka kufanikisha kikao hiki cha leo…na kwa kuwa hamna mradi wowote wa kuwaingizia kipato kama wazee, ninaahidi kuwapa Sh. 3,000,000 kutoka mfuko wa jimbo, ili muanzishe walau saccos ya kukopeshana,” alisema.

Baadhi ya viongozi na wananchi wamekuwa wakilitaja mara kwa mara jina la Waziri Magufuli miongoni mwa watu wanaodhaniwa kutaka kugombea nafasi ya urais wa Tanzania mwaka 2015, ingawa mwenyewe amekuwa akikanusha uvumi huo.

Mbali na Dk. Magufuli, wengine ndani ya CCM wanaotajwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye anajiita mtaji wa urais; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Ushirikiano wa Kimataifa –CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe, ambaye alipata kusema anasubiri kuiteshwa na Mungu kuwania nafasi hiyo.

CHANZO: NIPASHE
 
lione bila hata aibu unasema hayo, Nyie ndo mnaharibu nchi hii!

Huyu alieshindwa kuondoa kadhia ya KUCHINJA jimboni kwake, ataweza kufuta huu msamiati wa DHAIFU?
Ni mchapakazi, apewe ukatbu mkuu kiongozi.

tragedy of the commons
 
Freemason chaggawood ltd huioni. To hell with these peoples. Like kikuyu of kenya. Peoples will be when you they are against them
hii inaonyesha wazi ni
nani mwanzilishi wa sera ya ukabila.sijawahi kumsikia mbowe wala mtu
yeyote wa chadema akiwazungumzia viongozi wa ccm kwa makabila yao kama
kigezo cha kuwanyima uongozi lakini nyinyi ccm mnafanya hivyo na wewe
hapa umeshaonyesha hilo.kutwa kucha mbowe mchaga,chagaa,chagaa,hata
baadhi yenu mlidiriki kuja hapa kuwachafua hata baadhi ya mawaziri tena
waadilifu wa jk kutoka huko huko ccm kisa tu wameoa wachaga.kati yenu
nyinyi na chadema nani mkabila hapo?hata humo ccm wapo watu waadilifu na
baadhi yetu tunawajua watu makini waadilifu lakini hawapewi priority
zaidi ya kupigwa vita tu.ukiona mtu anakuwa maarufu ndani ya ccm hii ya
leo basi ujue mhuni mwenzao na lile kundi la wahuni ndani ya chama.hata
humu ndani jf tayari wewe ushaibuka na uchaga wa mbowe.unajionyesha ndio
wale wale ccm ya wahuni na makaburu mliokwishaigawa tz kikabila na
kuwapuuza wale wanaowakosoa.kwa hiyo wewe unataka kuniambia kwenu ccm
wachaga ni second class citizen,hawastahili kutoa
viongozi?endeleeni,mnajionyesha taratibu sera zenu na wananchi
tunaona!
 
Waungwana naomba mulonge si kwa ushabiki wala unafiki, ila kwa hoja zilizoshiba na zenye mashiko. Kama uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ungefanyika leo, ni nani ungempa kura yako aiongoze Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya Dr. MAGUFULI na EDWARD LOWASA?
Kiongozi ambae ataweza kututoa kwenye hii bahari ya Ufukara, asimamie haki na kutetea maslahi ya wanyonge wa Tanzania na raslimali zao ambazo kwa mda mrefu sasa zinawanufaisha wachache hasa wa tabaka tawala?
Najua wengi ni wakereketwa wa vyama fulani fulani vya siasa hapa nchini, naomba tutoke huko kwa mda mfupi, tujengane kwa hoja zenye mashiko bila kujali chama cha siasa wanachotoka niliowataja. Mikataba isiyo na tija kwa Taifa, hofu ya kuwawajibisha mafisadi, wala rushwa na wimbi la uanzishaji wa mifumo ya utendaji kazi isio na tija kwa Taifa iwe dira yetu katika kuchambua uwezo wa wawahusika niliowataja hapo juu kwenye nafasi ya Uraisi wa nchi hii.
Mashiko ya hoja zenu, yatatujenga wengi na kutoa mwelekeo mpya wa harakati zinazoendelea hapa nchini na baadhi ya vigogo wenye nia ya kuwania nafasi 2015.
By LULAMSO
 
Back
Top Bottom