John Magufuli: Ninautamani urais!

John Magufuli: Ninautamani urais!

Huyu atakuwa dhaifu kuliko JK! Mambo mengi ya kitaifa ananyamazia hatujui msimamo wake...kwanza toka lini injinia akawa raisi! Akajenge madaraja huko!

Mangufuli ni CHEMIST alipata phd yake mwaka 2009 hapa UDSM, na hata Msc yake alifanya ya CHEM. undergraduate alisoma BED sc akamajor CHEM& MATH.
NA HII HAPA NI PUBLICATION YA KWANZA MWAKA 1999

Mulokozi, A. M., Kyobe, Magufuli, J. P. and R. Whitehead. ¿A New Rate Equation for Solid State Decompositions and its application to the Decomposition of CaCo3. TCS Inaug. Conf. Proc., 11 -16 July, 1999, p162 -183.
 
We ndo useme sasa! Huyu Kimeo bana! hana kitu cha maana....hatutak kufanya makosa tena...hata hivyo CCM unayeweza kumuamini ni yule aliekufa!
come up with fact to convise me that magufuli is not the right candidate but otherwise for me he is the right candidate
 
Nadhani unahitaji kujifunza namna ya kuishi na watu wenye mitazamo ya hovyo, na ile mizuri pia. Unatakiwa kujifunza namna ya kumeza machungu. Sidhani kama ni sahihi kwako kufanana na yule first lady wa Kenya (Lucy Kibaki.
Inawezekana kabisa kuna watu humu wana maudhi, lakini namna ya ku deal nao ni changamoto unayohitaji kuikabili. Jibu lako kwa kila maudhi yanayoelkezwa kwako linapaswa kumjenga yule anayekushambulia, sioni usahihi wa kukimbizana mitaani na mtu aliyekwapua nguo zako wakati unaoga......wanaweza wa kaingilia ili kumuokoa huyo unayemkimbiza wakidhani wewe ndiye mwenye matatizo na unataka kumdhuru.

Angalia nafasi yako, every move you make, either itajenga au kubomoa umoja.
Lastly, any advise is an option, you can take or drop it.

Mkuu maneno kuntu haya. Umenena vyema sana inabidi mama ayachukue haya maneno na kuyafanyia kazi. Mitandao ya kijamii ni hatari sana ikitumika tofauti. Inabidi tuitumie kwa busara.
 
hivi kumbe ni muhandisi enh!!
eti mimi nilijua ni chemist, manake nimesomea baadhi ya polymer alizozisyanthesize yeye pale UDSM idara ya kemia.

Yeye siyo Mhandisi. Dr. Pombe ni chemist ama Mkemia
 
Huyu atakuwa dhaifu kuliko JK! Mambo mengi ya kitaifa ananyamazia hatujui msimamo wake...kwanza toka lini injinia akawa raisi! Akajenge madaraja huko!

Moja soma hapa kuhusu rais aliyepita na wa sasa wa CHINA (both with engineering background)
Mbili usifungue domo lako kama hujui kutafuta taarifa....
Tatu Wahandisi labda na wanasheria ndio pekee wanaweza kukomboa taifa hili (kujenga mikakati ya kiuchumi) haswa wanatakiwa wapewe nafasi za juu za maamuzi mfano Taasisi ya urais

Nne Usiwe -------- siku nyingine soma halafu andika (mimi nimechukizwa na sentensi zako kuhusu uhandisi/engineering)
 
Pole mkuu!!
 
Magufuli JPJ 2009 The potential of Anacardic acid Self-Assembled Monolayers from Cashew Nut Shell Liquid as Corrosion Protection Coatings, PhD Thesis, University of Dar es Salaam
 
moja soma hapa kuhusu rais aliyepita na wa sasa wa china (both with engineering background)
mbili usifungue domo lako kama hujui kutafuta taarifa....
Tatu wahandisi labda na wanasheria ndio pekee wanaweza kukomboa taifa hili (kujenga mikakati ya kiuchumi) haswa wanatakiwa wapewe nafasi za juu za maamuzi mfano taasisi ya urais

nne usiwe -------- siku nyingine soma halafu andika (mimi nimechukizwa na sentensi zako kuhusu uhandisi/engineering)

mkuu na mimi nimechukizwa sana na hoja zako kuhusu fani nyingine. Moja nyerere alikuwa ni mwl lakini alitupatia uhuru. Asilimia 90 ya viongozi wa nchi hii walikuwa ni waalimu, na mpaka sasa hao wahandisi unao waona wengine walikuwa ni waalimu kama mimi.

Hoja ya msingi ni kwamba sio fani inayoongoza nchi bali ni uwajibikaji, utu wema, uthubutu, mamlaka na ukiona mbali. Mm japo ni mwl naamini pia ni kiongozi mzuri kuliko baadhi ya wahandisi na maloya unaowadhania.
 
Magufuli JPJ 2009 The potential of Anacardic acid Self-Assembled Monolayers from Cashew Nut Shell Liquid as Corrosion Protection Coatings, PhD Thesis, University of Dar es Salaam

Kwa mnaoijua hii fani: hii kitu inahusu mabibo ya korosho au nakosea? Ningemshauri aombe kazi ya kufundisha chemistry pale Mlimani, kwa mtazamo wangu hii ingekuwa retirement plan nzuri kuliko kujaribu urais ambao ataukosa na ngeu juu!
 
magufuli jpj 2009 the potential of anacardic acid self-assembled monolayers from cashew nut shell liquid as corrosion protection coatings, phd thesis, university of dar es salaam

hahahahah! Nimeipenda hii manake juzi tumeitumia kutoa nanoparticles kwaajili ya kutrap heavy metals kutoka kwenye maji na ilifanya kazi vyema sana. Infact he is the founder wa emerging opportunities za cns
 
kwa mnaoijua hii fani: Hii kitu inahusu mabibo ya korosho au nakosea? Ningemshauri aombe kazi ya kufundisha chemistry pale mlimani, kwa mtazamo wangu hii ingekuwa retirement plan nzuri kuliko kujaribu urais ambao ataukosa na ngeu juu!

mkuu hebu tulia kwanza haihusu mabibo ya korosho hii inahusu mabanguo ya korosho yaani zile taka zake na so far alitufungulia njia wengine tumeiendeleza mbali mno sasa hivi kwa kutumia nanotech.

Unaposema aombe kazi ya kufundisha inamana kwamba hana haki ya kugombea uraisi?? Hebu kwanza nenda kaangalie publication zake alizowah kufanya ndipo utakapojua kwamba yuko diversified kiasi gani. Huwez kumlinganisha na hao wengine ambao hawana hata vyeti vya kueleweka
 
mkuu na mimi nimechukizwa sana na hoja zako kuhusu fani nyingine. Moja nyerere alikuwa ni mwl lakini alitupatia uhuru. Asilimia 90 ya viongozi wa nchi hii walikuwa ni waalimu, na mpaka sasa hao wahandisi unao waona wengine walikuwa ni waalimu kama mimi.

Hoja ya msingi ni kwamba sio fani inayoongoza nchi bali ni uwajibikaji, utu wema, uthubutu, mamlaka na ukiona mbali. Mm japo ni mwl naamini pia ni kiongozi mzuri kuliko baadhi ya wahandisi na maloya unaowadhania.

Sikusema wengine hawawezi nachosema kwa nchi changa kama yetu twahitaji mtu mwenye akili iliyochongeka kama fani nyingine zinaweza kutupatia ni sawa lakini so far content ziijazayo akili ya WAHANDISI ndio nchi inachohitaji

China wanajijenga kwa content ninayo izungumzia no offense to any professional
Waandisi kwa nature ya knowlegde walioyapata wako decisive thats what we need in this country (hapa siko subjective bali niko objective kama waelewa nachomaanisha)
 
Doa lake ni namna walivojenga hoja ya kuuza nyumba za umma na mchakato mzima wa kutekeleza azma hiyo ya kuuza nyumba za watanzania wote kwa bei wanayojua wao! Otherwise ni miongoni mwa watu ambao kama CCM wangekuwa hawachumii tumboni angeweza kupeperusha bendera ya CCM, LAKINI kwa mfumo wao wa huyu ni mwenzetu na huyu sio mwenzetu tegemea mla rushwa,mwenye kashfa nyingi,mnafiki nk atapendekezwa na ikiwezekana kushinda!
 
mkuu hebu tulia kwanza haihusu mabibo ya korosho hii inahusu mabanguo ya korosho yaani zile taka zake na so far alitufungulia njia wengine tumeiendeleza mbali mno sasa hivi kwa kutumia nanotech.

Unaposema aombe kazi ya kufundisha inamana kwamba hana haki ya kugombea uraisi?? Hebu kwanza nenda kaangalie publication zake alizowah kufanya ndipo utakapojua kwamba yuko diversified kiasi gani. Huwez kumlinganisha na hao wengine ambao hawana hata vyeti vya kueleweka

Huyu mheshimiwa kichwa chake kina heshima ya kipekee na kila mtu anaona jinsi alivyo na kumbukumbu kali, yani kichwa inanasisha utirio ni balaa. Ndiyo maana napenda awe Profesa wa Chemistry, huko kwenye urais tutapata hasara.
 
sikusema wengine hawawezi nachosema kwa nchi changa kama yetu twahitaji mtu mwenye akili iliyochongeka kama fani nyingine zinaweza kutupatia ni sawa lakini so far content ziijazayo akili ya wahandisi ndio nchi inachohitaji

china wanajijenga kwa content ninayo izungumzia no offense to any professional
waandisi kwa nature ya knowlegde walioyapata wako decisive thats what we need in this country (hapa siko subjective bali niko objective kama waelewa nachomaanisha)

sijaona logic behind ur urgument dude!!!
Ukisemea china ni simple kwamba wao walipata viongozi ambao ni wahandisi lkn haimaanish kwamba kiongozi wao angekuwa dr ama mwl asingeweza kuwafikisha hapo walipo. Kwani unafkiri ni content gani zinazoijaza akili ya kihandisi?? Manake kama ni nyanga za kihandisi mm ni ticha lkn nazipga utafikir ndo injinia mwenyewe. Wewe niweke popote pale iwe kwenye highway, construction iwe kwenye chemical ana mechanics na sikupata tabu yyte kuzijua haya makitu.

Ungeniambia angepatikana mtu mwenye uchungu na nchi hii akawa na nia ya dhati ya kufufua viwanda, na kilimo, akawa na uchungu na elimu ya nchi hii binafsi nakwambia lazima tutafika lkin hata aje mhandisi gani hana hizi qualities ni bure kabisa.

Ngoja nikupe mfano mdogo sana juzi kaja obama hapa tanzania. Nilidhani kabisa mhe rais wetu alikuwa na nafasi ya kupendekeza watu gani waonane na obama cha ajabu ni kwamba hakutoa pendekezo yeye ilikuja oda tu kwamba ataonana na wafanya biashara. Nilichojiuliza mimi hawa wafanyabiashara akina mengi na bakhressa mbona viwanda vyao ni vya daraja la pili?? Je kwann asingesema waje na wakulima?? Ili wale wanaotoa malighafi nao wawe ni sehem ya mjadala wao.

Kwangu mimi nilijionea kituko na ndio maana nasema kwamba si kwamba tuahitaj mhandisi bali tunahitaj mtu anayejua vitu na ambaye anabeba uchungu wa taifa hili.
 
Sikusema wengine hawawezi nachosema kwa nchi changa kama yetu twahitaji mtu mwenye akili iliyochongeka kama fani nyingine zinaweza kutupatia ni sawa lakini so far content ziijazayo akili ya WAHANDISI ndio nchi inachohitaji

China wanajijenga kwa content ninayo izungumzia no offense to any professional
Waandisi kwa nature ya knowlegde walioyapata wako decisive thats what we need in this country (hapa siko subjective bali niko objective kama waelewa nachomaanisha)

Hapa hujanishawishi. Hizo fani nyingine umezisoma zote ukaona hazina hizo sifa unazotaja? Kama unatafuta rais wa wahandisi hapo sawa. Lakini kuwa rais wa watu wote: tycoons na wamachinga, celebrities na mama ntilie, madaktari wasomi na waganga wa kienyeji, wacheza sindimba na wale wa kibao kata, maprofesa wa kilimo na wakulima wadogowadogo, walimu wa madrasa makatekista wainjilisti na wazee wa mila,architects na wachora katuni, diplomats na wavuvi, etc etc etc, rais wa watu wote hawa anahitaji elimu zaidi ya hiyo ya engineering unayojitapa nayo. Elimu ya kumudu majukumu ya urais ipasavyo haipatikani kwenye kozi yoyote ya enginering wala law.
 
...ishu siyo mtu, ila mfumo wa chama chake ndo hovyo sana, wapo kimaslahi zaidi,wamepoteza ladha ya uzalendo na mzigo wa kuwa kwamua watu kwenye umasikini...

Magufuli ni mzuri kiutendaji na anaweza kufanya wonders akiwa Rais ila ujinga wake ni kumsifia mno mtu dhaifu aliyeshindwa kuiongoza nchi. Pia akiwa Rais atawalinda waliofisadi nchi kwa sababu atalishwa kiapo cha kisirisiri na mafisadi ya CCm.
 
Back
Top Bottom