John Heche moments special thread

John Heche moments special thread

Huwa nikiingia YouTube kitu Cha kwanza kutafuta ni wapi heche ameongea kwa siku hiyo huwa napenda sana kufuatilia hotuba zake jamaa ni a good public speaker
 
Mh. hechejohn anaandika

"Nchi imegeuzwa kama ghetto kila mtu anajifanyia anavyotaka!!!!
Huyu amejigeuza polisi, yeye huyo huyo mahakama!!! Anaita watu,
anawahoji na kuwapa msamaha!!!!

Kama hao watu wana makosa kweli huyu Katambi ana mamlaka kwa mujibu
wa sheria ipi kufuta makosa?

Watu wanatekwa kila siku hata jana Rose ametekwa na Katambi hajawahi
kutuambia watu waliotekwa wakina Mdude wako wapi?

Huyu Katambi hajawahi kuwambia Watanzania alipo Polepole, leo
anapambana na wasanii!!!"
Huu ni ujingaa"
1788595433660.jpg
 
Hakika tungekuwa na makamu legelege kipindi hiki sijui CDM ingekuwa kwenye hali gani
 
Tayari Mhe. John Heche amepanda kizimbani kwa ajili ya kutoa ushahidi wake.
1789003769919.jpg
 
Katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu shahidi wa tano wa upande wa utetezi na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche ameieleza Mahakama kuwa madhila mbalimbali ambayo CHADEMA ilipitia katika chaguzi zilizopita ndiyo yaliyochochea kamati kuu kupitisha msimamo wa “No Reforms, No Election”… yaani, bila mabadiliko hakuna uchaguzi.

Heche ameyasema hayo mbele ya Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, wakati akitoa ushahidi katika kesi hiyo inayosikilizwa na jopo la majaji watatu, likiongozwa na Jaji Dustan Ndunguru.
 
Back
Top Bottom