John Heche: CHADEMA haiko tayari kwa Maridhiano

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
24,143
Reaction score
56,407
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakitakuwa tayari kwa maridhiano yenye kupumbaza, kuhadaa, yenye ulaghai na yenye kuliondoa Taifa kwenye ukweli, haki na kile ambacho Taifa inataka na kusisitiza kuwa kamwe CHADEMA haitowasiliti Watanzania.

Akiongea leo January 03,2026, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche amesema “CHADEMA, Chama chenu hakitakuwa tayari kwa maridhiano yenye kupumbaza, kuhadaa, yenye ulaghai na yenye kuliondoa Taifa kwenye ukweli, haki na kile ambacho Taifa inataka, kamwe hatuwasaliti Watanzania”

“Ni ubatili na dharau kubwa kwa Watanzania kuyaita maridhiano sasa katika mazingira ambapo Serikali iliamua kwa makusudi kuwapuuza Wananchi, Vyama vya siasa na Wadau wa demokrasia juu ya hitaji la nchi kuhusu mabadiliko (reforms) ya mifumo ya uchaguzi nchini, uchaguzi batili hauishii kwenye siasa pekee, huingia moja kwa moja kwenye tumbo la mwananchi na heshima ya maisha yake ya kila siku”

“Leo ninapotoa salamu hizi ni siku ya 269, tangu Mwenyekiti wetu, Tundu Lissu alipokamatwa na kuwekwa mahabusu kwa kesi ya uongo, batili na yenye uonevu wa makusudi wakidhani atapiga magoti kusujudia sanamu”.
 
Waotishe wagiwa wote wawape maridhiano nao.....sio chauma na fake fake kina malasusa .....toilet paper...na sheikh ubwabwa sijui bwabwajas......
 
Kwani wameitwa kwenye maridhiano!?..sisi tunataka wadakwe wanyee debe
 
Nilishashauri hakuna haja ya maridhiano na hawa wahuni. Serikali isonge mbele kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM kwa sababu miaka 5 ni michache mno. Tusipoteze kuridhiana na wahuni aina ya Heche.
 
Huu ndio msimamo makini sana. Najivunia sana kushabikia chama kinachojitambua. Kuna wajinga wanadhani bado cdm ni chama kinachotetemekea ruzuku. Cdm imeshavuka hatua ya kutegemea ruzuku, maana hiyo ilitumika kuvuruga vyama vya upinzani. Msimamo ni huo huo. Bigup cdm.
stakehigh ERTUGRUL BEY HAYA LAND HOV THE BIG SHOW
mkuu hao machawa wanatapatapa sana walidhani itakuwa rahisi hivyo
 
“Ni ubatili na dharau kubwa kwa Watanzania kuyaita maridhiano sasa katika mazingira ambapo Serikali iliamua kwa makusudi kuwapuuza Wananchi, Vyama vya siasa na Wadau wa demokrasia juu ya hitaji la nchi kuhusu mabadiliko (reforms) ya mifumo ya uchaguzi nchini, uchaguzi batili hauishii kwenye siasa pekee, huingia moja kwa moja kwenye tumbo la mwananchi na heshima ya maisha yake ya kila siku”
Samia na kundi linalomzunguka ni kama watu ambao akili zao zina kasoro kubwa sana; kwa kudhani kuwa waTanzania hawajui chochote au hawakumbuki ulaghai na hadaa zinazofanywa na kundi hili.

Baada ya kufanya mambo ya hovyo kabisa na kusababisha vifo vya waTanzania, bado wanadiriki kuleta ulaghai wa aina hii mapema namna hii?

Na kama hiyo haitoshi; wanahimiza "maridhiano" wakati mambo yaleyale ya hovyo yakiendelea kufanyika.
Kwa mfano: utawaambia CHADEMA washiriki vipi kwenye maridhiano wakati viongozi wao wakiwa kwenye hatihati, na chama chao kikiwa kwenye kesi za kutungwa tu?
Hawa na wanachama wao na wapenzi wa chama hicho utawashirikisha vipi kwenye maridhiano?

WaTanzania wanaendelea kukamatwa/kutekwa kwa kutoa tu maoni yao. Bunge na Mahakama vikiwa vyombo vya kukandamiza hao unaotaka kuridhiana nao!
Haya yatakuwa ni maridhiano ya namna gani haya!
 
Nilishashauri hakuna haja ya maridhiano na hawa wahuni. Serikali isonge mbele kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM kwa sababu miaka 5 ni michache mno. Tusipoteze kuridhiana na wahuni aina ya Heche.
Kwani aliyetaka maridhiano ni heche au ccm? Hebu ni wapi chadema au heche waliitisha maridhiano baada y uchaguzi.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakitakuwa tayari kwa maridhiano yenye kupumbaza, kuhadaa, yenye ulaghai na yenye kuliondoa Taifa kwenye ukweli, haki na kile ambacho Taifa inataka na kusisitiza kuwa kamwe CHADEMA haitowasiliti Watanzania.

Akiongea leo January 03,2026, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche amesema “CHADEMA, Chama chenu hakitakuwa tayari kwa maridhiano yenye kupumbaza, kuhadaa, yenye ulaghai na yenye kuliondoa Taifa kwenye ukweli, haki na kile ambacho Taifa inataka, kamwe hatuwasaliti Watanzania”

“Ni ubatili na dharau kubwa kwa Watanzania kuyaita maridhiano sasa katika mazingira ambapo Serikali iliamua kwa makusudi kuwapuuza Wananchi, Vyama vya siasa na Wadau wa demokrasia juu ya hitaji la nchi kuhusu mabadiliko (reforms) ya mifumo ya uchaguzi nchini, uchaguzi batili hauishii kwenye siasa pekee, huingia moja kwa moja kwenye tumbo la mwananchi na heshima ya maisha yake ya kila siku”

“Leo ninapotoa salamu hizi ni siku ya 269, tangu Mwenyekiti wetu, Tundu Lissu alipokamatwa na kuwekwa mahabusu kwa kesi ya uongo, batili na yenye uonevu wa makusudi wakidhani atapiga magoti kusujudia sanamu”.
Waridhiane na magari na pikipiki zilizochomwa moto. Hatukubali....tunataka miili ya ndugu zetu, watueleze kwanini hadi leo wameficha maiti za ndugu zetu? Na kwanini wameficha?
 
Sahihi kabisa. Hongera sana Heche. CHADEMA isijiingize kwenye laana kwa kukaa meza moja na wauaji.

Kinachotakiwa ni wauaji wote kukamatwa na kuwajibishwa. Baada ya wauaji na watekaji kukamatwa na kuadhibiwa sawasawa na uovu wao, ndipo watu wema wafanye majadiliano namna ya kutengeneza mifumo mipya ya kuongoza nchi itakayozuia kabisa kuwa na watawala waovu kama hawa wa sasa.
 
Back
Top Bottom