Joe Biden: China Iko Taabani Kiuchumi

Joe Biden: China Iko Taabani Kiuchumi

Una ushahidi wa kitaalamu juu iko alichosema Biden?? Wewe ni mchumi?

Or kwasababu kaongea Biden na wewe unaamini ?? Hujui USA ndio mpinzani mkubwa wa China kiuchumi??, Sasa unategemea USA waisifu china?

Watu weusi sjui tunashida gani,yaani kitu akiongea Marekani basi nasisi tunaamini
Wewe kafatilia data walizotoa Wachina wenyewe wiki iliyopita
 
Huu ndio ukweli ila wale wafuasi wake Watapinga.

Idadi ya Watu wanaozaliwa China imepungua kuliko vifo.

Idadi ya Wazee inazidi kuongezeka

Ukuaji wa Uchumi wake Umepungua sana.

Shida ya Kisiasa za ndani zimenza,sera ya zero covid iliwaahinda Hadi watu wakaandamana dhidi ya Utawala.

Kampuni zake za nyumba zimeanza kupata shida na Baadhi mbioni kufilisika eg Garden

Gharama za Uwekezaji wa viwandani zimeanza kuongezeka.

Mwisho China imeanza Utapeli wa Mali na ukoloni mamboleoa Kwa Nchi za Kiafrika Kwa njia ya Mikopo nk.


My Take
China haiaminiki, siku yaja Yuan yake itaporomoka sana.

ubongo wake ulishachoka huyu, si ajabu hata ukimuuliza jina la mtoto wake hakumbuki mpaka amuulize mkewe
 
China imetangaza kupata deflation mwezi huu nadhani ilikuwa kama 0.3%. Na ajira hazipatikani.
Hayo ndiyo matatizo makubwa nayaona kwake, mengine ya wazee kuongezeka, uchumi kupungua na gharama za uwekezaji kuongezeka yalitarajiwa huwezi kuyakwepa kutokana na sera zao na structure yao ya kiuchumi.

Nchi nyingi duniani zina uchumi wa kusuasua sasa hivi
Ila hapo ukute bado wameficha uhalisia.

Swala la majumba linawahenyesha sana
 
ila ule ujinga wao wa kupangiana idadi ya kuzaa ndio sijawahi kuuelewa hadi kesho. mtu hata kama una pesa za kutunza watoto ungetamani kuzaa watoto 12, wamekulimit.
Wameshtuka muda ushaenda
 
Zimegomaje wakati bado China muuzaji mkubwa wa bidhaa nje ya nchi na nchi yenye uchumi mkubwa duniani baada ya Marekani.
Ukisoma ripoti ya Ijumaa China uuzaji nje na manunuzi yamepungua kwa miezi 4 kwa 5 mtawalia
 
Ile ilikuwa ni sera muhimu sana kwa kipindi kile, na hawakuiweka kwamba itadumu milele na kwanza sasa hivi haipo. Hawakukosea kwenye hilo.

Alafu China mnaiponda sana, taja superpower iliyowahi kua kiuchumi kwa kasi kuizidi hapa duniani zaidi ya China. Nchi nyingi kwa sasa zina shida za Uingereza wana shida kibao hasa kwenye mfumo wao wa afya, Ufaransa matatizo kibao ya jamii yake na wahamiaji na nishati, Japan ina deni kubwa na population yake imejaa wazee, Marekani naye shida zake.

China ana matatizo makubwa ila tusisahau kipindi hiki matatizo ni mengi kwa mataifa makubwa.
Je nchi changa, tegemezi kama za Afrika zitasimama ikitokea hizo kubwa zinadororora kiuchumi?
 
Yeye ameshindwa ya America anaongelea ya China ?

China ni Taifa lililokuwa Kubwa. Likapata Shida hapo Katikati, Limefufuka tena na hata likioata shida wananchi wake wata-sustain..., Hio ndio tofauti ya Nchi kama China, Russia na USA; Watu sio wabishi wanachapa kazi na wakipata mtu visionary wanakwenda wanapopelekwa (A Benevolent Dictator)...

Tofauti na US watu ni lawama na kulauminiana (a Country Divided) ngoja Trump arudi au hata Republican waanze kubadilisha haya yaliyofanywa na huyu..., Ni mwendo wa kurumbana
 
Je nchi changa, tegemezi kama za Afrika zitasimama ikitokea hizo kubwa zinadororora kiuchumi?
Afrika haijawahi kuwa chanzo cha tatizo lolote duniani labda ile scramble for Africa ambayo mkutano wa Berlin ililimaliza. Sisi tunapokea kila mabadiliko iwe vita za dunia, utandawazi, matatizo mengine na maendeleo. Na Afrika haiwezi simama peke yake hivyo itaathirika na mdororo huu wa kiuchumi duniani
 
Huu ndio ukweli ila wale wafuasi wake Watapinga.

Idadi ya Watu wanaozaliwa China imepungua kuliko vifo.

Idadi ya Wazee inazidi kuongezeka

Ukuaji wa Uchumi wake Umepungua sana.

Shida ya Kisiasa za ndani zimenza,sera ya zero covid iliwaahinda Hadi watu wakaandamana dhidi ya Utawala.

Kampuni zake za nyumba zimeanza kupata shida na Baadhi mbioni kufilisika eg Garden

Gharama za Uwekezaji wa viwandani zimeanza kuongezeka.

Mwisho China imeanza Utapeli wa Mali na ukoloni mamboleoa Kwa Nchi za Kiafrika Kwa njia ya Mikopo nk.


My Take
China haiaminiki, siku yaja Yuan yake itaporomoka sana.

Mzee babu hajiwezi anatuletea habari za China, Mzee mwenyewe hata memory card yake haifanyi kazi
 
Back
Top Bottom