JKT waliorudishwa nyumbani watakiwa makambini

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,982
144,306
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge, amewataka vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea kwa mwaka 2020/2021 na kurejeshwa nyumbani mwezi Februari mwaka huu kurejea makambini.

Kaimu mkuu wa utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Hassan Mabena, amewaambia wanahabari kuwa vijana hao wanatakiwa kuripoti kwenye makambi waliyopangiwa awali.

Aidha Kanali Mabena amesema kuwa JKT wameingia makubaliano na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kwa ajili ya vijana kupata elimu ya vitalu.

Mwezi Februari mwaka huu, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alitangaza kuwarejesha nyumbani zaidi ya vijana 12,000, hadi ambapo wangetangaziwa tena.
 
Usikute ndo vibaka wa muda huu. Maana matukio ya ukwapuaji yameongeza Dar. Juzi rafiki yangu kapigwa roba na kuchukuliwa simu.
Bora warudishe huko. Pia, next time CDF afanye upembuzi kabla ya kufikia maamuzi.
 
Back
Top Bottom