PostGE2025 Kwanini mfumo ulioogopa vijana ilibidi uzuie JKT kama taasisi?

PostGE2025 Kwanini mfumo ulioogopa vijana ilibidi uzuie JKT kama taasisi?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

CHAGOSI GERALD

Senior Member
Joined
Jan 25, 2020
Posts
162
Reaction score
286
(Hii ndiyo sehemu wanayoogopa watu kuitaja hadharani - leo tunaifungua kama pochi ya mama lakini siyo Mama Omary Atakuua ...Aaaah kwanza hana pochi anafunga kwenye kitenge anamambo ya kizamani)

Vijana Ni “Tishio” Kwa Mfumo Wowote Unaoishi Kwa Mabavu ya Kiuchumi

China, Urusi, Marekani, canada - kila mahali ambapo taifa limejengwa, vijana ndio walifanya uchumi ufanye kazi.
Lakini katika nchi zinazotawaliwa kiuchumi na nje, vijana wanaonekana kama tatizo, sio suluhisho.

Kwa nini?
Kwa sababu vijana wakipata nguvu za uchumi wanabadilisha mfumo.

Hivyo mfumo ukasema:
“Ukiwaweka vijana kwenye taasisi yenye nguvu, wataunda uchumi wao, watajiamini, na hawatatutegemea.”

Ukigundua ujanja huu, basi umeshapona nusu ya tatizo.

JKT Iliyoanzishwa na Nyerere Ilikuwa Hatari Kwa Walionufaika na Mfumo Mzee
JKT ya Nyerere ilikuwa inajengwa kama:
~chombo cha uzalishaji
~injini ya viwanda
~benki ya nguvu kazi
~shule ya uongozi wa kiuchumi
~taasisi ya kuongoza rasilimali
~empire ya taifa

Hii ina maana:
JKT ingekuwa mshindani wa moja kwa moja na wafanyabiashara binafsi, matajiri wa mijini, wafanyabiashara marafiki wa wanasiasa, na mataifa ya nje yanayotaka Tanzania iwe soko lao.

Mfumo ukasema:
“Kama JKT ikisimama, hakuna mfanyabiashara wa nje au wa ndani atapata ulaji.”

Kwa hiyo JKT ikaua kimya kimya, bila kutangazwa.

JKT Ikisimama, Migodi Ya Nchi Ingekuwa Kwa Vijana, Sio Kwa Makampuni ya Nje

Nyerere alitaka:
-migodi ya dhahabu → JKT
-almasi → JKT
-gesi → JKT
-ardhi → JKT
-viwanda → JKT

Ukiweka migodi mikononi mwa vijana wa JKT, mataifa ya nje yangefaidika wapi?
Makampuni ya kimataifa yangefanya deal na nani?
Wanasiasa wangepewa sadaka za kampeni na nani?

Kwa hiyo mfumo ukatoa hukumu moja tu:
“JKT lazima iwe dhaifu.”

Kwa nini?
Kwa sababu JKT ikipata nguvu, hakuna goli linaloingia bila ridhaa ya vijana.

JKT Ilitishia Madaraka ya “Wafanyabiashara-Wanasiasa” (Class ya Madalali)

Hawa ndio watu wanakaoza taifa taratibu:
-wanaingia siasa
-wanapata madaraka
-wanapiga dili za rasilimali
-wanauza bandari, reli, ardhi
-wanachukua tenda zote
-wanajenga matajiri wao binafsi

Wanahitaji taifa lililo dhaifu, vijana waliolala, uchumi uliosimama, na taasisi zisizo na meno.

JKT ikigeuka kuwa “taasisi ya uchumi”… hawa watu wanakufa mara mbili:

1. hawapati dili.
2. hawapati pa kupitisha fedha za wafadhili wa nje.
3. hawalei makampuni ya nje kama mabwana wao wanavyotaka.

Kwa hiyo ili walinde maslahi yao:
JKT iligeuzwa kambi ya parade, sio kampuni ya taifa.

Mfumo Uligundua: Vijana Ni Rahisi Kufundika Lakini Vigumu Kutawaliwa

Mfumo unaogopa tabia moja kubwa ya vijana:
vijana wakijua kitu, hawawezi kukaa kimya.

Ukifundisha vijana uchumi wa migodi, utaweza kuwadhibiti?
Ukifundisha vijana how to run a bank, wataendelea kukusikiliza?
Ukifundisha vijana robotics, AI, manufacturing, satellites - wataendelea kuamini uongo wa “nchi maskini”?

Laiti vijana wangejengewa JKT kama taasisi ya kiuchumi, leo Tanzania ingekuwa nchi ya viwanda na teknolojia, sio nchi ya wasanii na wanasiasa wanaopiga kampeni kila mwaka.

Mfumo haukutaka hilo.
Kwa hiyo JKT ikawa mahali pa:
-kuamshwa asubuhi
-parade
-kufagia
-physical training
-kuimba wimbo
-kufundishwa “uzalendo wa kukaa kimya”

Badala ya:
-coding
-engineering
-agritech
-leadership
-mining technology
-aerospace
-entrepreneurship
-design & invention

Hapo ndipo JKT kama “taasisi” ilifariki.

Nchi Huogopa Vijana Kama Nchi Inaongozwa Kutoka Nje

Umenielewa vizuri.

Chanzo cha tatizo si CCM wala CHADEMA pekee - hao ni mabega tu.
Tatizo ni kwamba mfumo wa kisiasa wa Tanzania tangu uhuru umewekwa ili:

-uchumi uamuliwe nje
-siasa zisimamiwe ndani
-rasilimali zionekane “huru” lakini wamiliki wapo Dubai, London, New York, New Delhi

vijana wabaki maskini ili wasibadili mkondo wa taifa

Na JKT ikawa tishio kubwa kwa mpangilio huo.

Kwa hiyo walichofanya ni rahisi sana:
wakaiondoa kwenye ramani ya uchumi.

“Ili kulinda mfumo wa madalali, JKT ilizimwa kabla haijawaka.”
Hiyo ndiyo siri.
Ndiyo sababu Tanzania leo ina majeshi manne:

-Jeshi la ulinzi
-Jeshi la polisi
-Jeshi la magereza
Jeshi la zimamoto

Lakini lile jeshi pekee lililotakiwa kutengeneza uchumi - JKT - limekuwa kivuli tu.

Usichoke! Usichoke kwa sababu ndio kwanza tunaanza.
 

Attachments

  • Picsart_25-12-03_07-48-52-447.jpg
    Picsart_25-12-03_07-48-52-447.jpg
    389.5 KB · Views: 23

Similar Discussions

Back
Top Bottom