Maaskofu: Kikwete ni 'Nabii'
Habari Zinazoshabihiana
Maaskofu: Kikwete ni 'Nabii' 31.05.2006 [Soma]
Maaskofu wampa mtihani Kikwete na yeye awatega 09.06.2006 [Soma]
Makamba afuata nyayo za Kikwete 10.07.2006 [Soma]
Maaskofu: Kikwete ni 'Nabii'
*Wasema hata manabii wa kweli walianza kwa matatizo
*Wadai hata shetani sasa amejenga hofu kubwa kwake
*Wawataka wananchi kuvumilia 'mitikisiko' inayotokea
Na Charles Mwakipesile, Mbeya
MAASKOFU wa Kanisa la Moravian Tanzania, wamesema matatizo yanayoikumba Serikali ya Awamu ya Nne, ni ishara kuwa Rais Jakaya Kikwete anakubalika mbele ya Mungu na ni kama manabii walivyopata shida katika ukombozi kabla ya mafanikio.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi jana katika makao makuu ya Kanisa hilo jimbo la Kusini Magharibi, walidai kuwa hakuna kitu cha ajabu kinachotokea katika utawala wa Rais Kikwete, zaidi ya kuwa ni ishara kuwa Mungu anatarajia kuinyeshea Tanzania 'mvua ya baraka' kupitia kwake.
Askofu Mkuu wa Jimbo la Kusini Magharibi, Mhashamu Alinikisa Cheyo, alisema katika vitabu vitakatifu, inaelezwa wazi, kuwa watu maarufu kama manabii wakiongozwa na Yesu, walipata matatizo makubwa kabla ya kupata mafanikio.
Alisema wakati Rais Kikwete anachukua uongozi tayari kulikuwa na mambo mabaya yaliyokuwa yamefanywa na baadhi ya viongozi hata kuwafanya Watanzania kuwa na maisha duni.
Askofu Cheyo alisema kutokana na hilo, mara baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani, alikuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa anawasafisha mafisadi waliokuwa wamejificha serikalini.
"Watanzania lazima wakubali kuwa Rais Kikwete aliahidi kuwa tutapata maisha bora, ili kufikia ahadi hiyo si kazi ndogo, ni kubwa inayokufanya wewe kukubali kuwa na maadui wengi kwa kuwa lazima uwafichue na warudishe fedha walizoiba serikalini," alisema.
Alisema hata nyumba iliyochakaa na kuharibika, inapotaka kutengenezwa lazima walio ndani yake wakubali kutikisika, kama ambavyo Watanzania wamekuwa wakitikiswa na uhalifu na majanga ya ajabu yanayotokea tangu kuanza kwa Serikali ya Awamu ya Nne.
Askofu huyo alisema kutokana na uongozi wa Rais Kikwete, ambaye alisema ni mwaminifu na msafi, Tanzania yenye neema itapatikana na kuwa na uchumi bora zaidi ya nchi kama Kenya ambazo ziko mbele kwa sasa.
Alisema ushindi mkubwa alioupata Rais Kikwete ambao ulivunja rekodi ni dalili kuwa alikuwa chaguo la Mungu na hivyo hadi Mungu amsaidie kuifikisha Tanzania inapotarajiwa, ni lazima apite katika magumu kama ilivyokuwa kwa Yesu, ambaye aliteswa msalabani kwa ajili ya kuwakomboa wanadamu.
Askofu Cheyo ambaye hivi karibuni alimaliza masomo yake ya juu ya Theolojia katika chuo cha Limuru, Kenya, alisema shetani ana hofu kubwa na Rais Kikwete, kutokana na anavyokubalika duniani na mbinguni .
Alisema kufumuka kwa ujambazi nchini ni hofu ya majambazi kuona kuwa mtu aliyeshika uongozi si mbabaishaji na hivyo wako hatarini kudhibitiwa kama walivyofanywa kwa sasa.
Naye Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian nchini, Askofu Lusekelo Mwakafwila, alisema mtindo wa uongozi anaoutumia Rais Kikwete ni imara na wenye lengo la kukomboa Watanzania kuondokana na umasikini na kukuza uchumi.
Alisema kinachotakiwa ni kwa wanaomsaidia kuhakikisha wanafanya kazi yao kwa bidii bila kumwangusha, kama ambavyo watu wengi wamekuwa wakitoa maoni kuwa Rais anapaswa kuungwa mkono na mawaziri wake wote wakisaidiwa na watendaji wao.
Mhashamu Mwakafwila alisema hakutakuwa na maana kama wasaidizi wake watamwangusha huku wakitambua kuwa ana kazi kubwa ya kukuza uchumi na kutengeneza hali itakayoondoa mfumuko wa bei kama uliopo sasa.
Alisema kazi ya kurekebisha uchumi si kazi ya muda mfupi kama wanavyofikiri Watanzania wengi na hivyo kinachotakiwa, ni kwa makanisa na madhehebu yote kumwombea Rais ili aweze kufanikiwa kushinda katika kazi aliyo nayo.