JK ni Nabii

Sam

JF-Expert Member
Jun 6, 2006
415
89
Maaskofu: Kikwete ni 'Nabii'

Habari Zinazoshabihiana
• Maaskofu: Kikwete ni 'Nabii' 31.05.2006 [Soma]
• Maaskofu wampa mtihani Kikwete na yeye awatega 09.06.2006 [Soma]
• Makamba afuata nyayo za Kikwete 10.07.2006 [Soma]

Maaskofu: Kikwete ni 'Nabii'
*Wasema hata manabii wa kweli walianza kwa matatizo
*Wadai hata shetani sasa amejenga hofu kubwa kwake
*Wawataka wananchi kuvumilia 'mitikisiko' inayotokea
Na Charles Mwakipesile, Mbeya
MAASKOFU wa Kanisa la Moravian Tanzania, wamesema matatizo yanayoikumba Serikali ya Awamu ya Nne, ni ishara kuwa Rais Jakaya Kikwete anakubalika mbele ya Mungu na ni kama manabii walivyopata shida katika ukombozi kabla ya mafanikio.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi jana katika makao makuu ya Kanisa hilo jimbo la Kusini Magharibi, walidai kuwa hakuna kitu cha ajabu kinachotokea katika utawala wa Rais Kikwete, zaidi ya kuwa ni ishara kuwa Mungu anatarajia kuinyeshea Tanzania 'mvua ya baraka' kupitia kwake.

Askofu Mkuu wa Jimbo la Kusini Magharibi, Mhashamu Alinikisa Cheyo, alisema katika vitabu vitakatifu, inaelezwa wazi, kuwa watu maarufu kama manabii wakiongozwa na Yesu, walipata matatizo makubwa kabla ya kupata mafanikio.

Alisema wakati Rais Kikwete anachukua uongozi tayari kulikuwa na mambo mabaya yaliyokuwa yamefanywa na baadhi ya viongozi hata kuwafanya Watanzania kuwa na maisha duni.

Askofu Cheyo alisema kutokana na hilo, mara baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani, alikuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa anawasafisha mafisadi waliokuwa wamejificha serikalini.

"Watanzania lazima wakubali kuwa Rais Kikwete aliahidi kuwa tutapata maisha bora, ili kufikia ahadi hiyo si kazi ndogo, ni kubwa inayokufanya wewe kukubali kuwa na maadui wengi kwa kuwa lazima uwafichue na warudishe fedha walizoiba serikalini," alisema.

Alisema hata nyumba iliyochakaa na kuharibika, inapotaka kutengenezwa lazima walio ndani yake wakubali kutikisika, kama ambavyo Watanzania wamekuwa wakitikiswa na uhalifu na majanga ya ajabu yanayotokea tangu kuanza kwa Serikali ya Awamu ya Nne.

Askofu huyo alisema kutokana na uongozi wa Rais Kikwete, ambaye alisema ni mwaminifu na msafi, Tanzania yenye neema itapatikana na kuwa na uchumi bora zaidi ya nchi kama Kenya ambazo ziko mbele kwa sasa.

Alisema ushindi mkubwa alioupata Rais Kikwete ambao ulivunja rekodi ni dalili kuwa alikuwa chaguo la Mungu na hivyo hadi Mungu amsaidie kuifikisha Tanzania inapotarajiwa, ni lazima apite katika magumu kama ilivyokuwa kwa Yesu, ambaye aliteswa msalabani kwa ajili ya kuwakomboa wanadamu.

Askofu Cheyo ambaye hivi karibuni alimaliza masomo yake ya juu ya Theolojia katika chuo cha Limuru, Kenya, alisema shetani ana hofu kubwa na Rais Kikwete, kutokana na anavyokubalika duniani na mbinguni .

Alisema kufumuka kwa ujambazi nchini ni hofu ya majambazi kuona kuwa mtu aliyeshika uongozi si mbabaishaji na hivyo wako hatarini kudhibitiwa kama walivyofanywa kwa sasa.

Naye Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian nchini, Askofu Lusekelo Mwakafwila, alisema mtindo wa uongozi anaoutumia Rais Kikwete ni imara na wenye lengo la kukomboa Watanzania kuondokana na umasikini na kukuza uchumi.

Alisema kinachotakiwa ni kwa wanaomsaidia kuhakikisha wanafanya kazi yao kwa bidii bila kumwangusha, kama ambavyo watu wengi wamekuwa wakitoa maoni kuwa Rais anapaswa kuungwa mkono na mawaziri wake wote wakisaidiwa na watendaji wao.

Mhashamu Mwakafwila alisema hakutakuwa na maana kama wasaidizi wake watamwangusha huku wakitambua kuwa ana kazi kubwa ya kukuza uchumi na kutengeneza hali itakayoondoa mfumuko wa bei kama uliopo sasa.

Alisema kazi ya kurekebisha uchumi si kazi ya muda mfupi kama wanavyofikiri Watanzania wengi na hivyo kinachotakiwa, ni kwa makanisa na madhehebu yote kumwombea Rais ili aweze kufanikiwa kushinda katika kazi aliyo nayo.
 
Maaskofu: Kikwete ni 'Nabii'Maaskofu: Kikwete ni 'Nabii'
*Wasema hata manabii wa kweli walianza kwa matatizo
*Wadai hata shetani sasa amejenga hofu kubwa kwake
*Wawataka wananchi kuvumilia 'mitikisiko' inayotokea

MMh.. kazi kweli kweli
 
kama kuna mambo yanatia kichefuchefu basi ni unafiki wa viongozi wetu wa dini. Wanajikomba huku wakishindwa kukemea ukweli. Hivi huyu askofu alisema haya kwa dhamira yake au ndio mambo ya kufikirika tu?
 
Hawa viongozi wetu wa dini naona wanajikanyaga wenyewe. Nikisoma hiyo habari ninashindwa kukubaliana na huyo Askofu Cheyo na kwamba mbali ninakubaliana na Mwakafwila.

Hivi huyu Askofu anataka kutuambia kwamba JK alisafisha nyumba yake kabla hajaingia Ikulu? Kama kweli aliisafisha imekuwaje leo hii agalagazwe na wananchi tena kwa makosa ambayo yametendwa na wasaidizi wake? Katika hiyo safu ya timu yake kuna watu ambao wamekuwa wakitumia uongozi/madaraka yao kwa manufaa yao binafsi na leo hii kuna mfano hai wa mkataba wa Buzwagi ambao hatuwezi kusema kwamba ulisainiwa wakati wa BWM. Huyo Askofu kajikita zaidi kwenye kumtetea JK kwa kusingizia kwamba matatizo mengi aliyakuta, yamerithiwa kutoka uongozi wa BWM, naweza kukubaliana na hiyo observation lakini kama kweli jamaa alikuwa committed kufanya usafi wa kweli alitakiwa asafishe kila kitu bila kujali kama kuna madudu yalifanywa na uongozi wa BWM.

Kwa kifupi ni kwamba pamoja na kurithi hayo matatizo, jamaa amekuwa mzito sana kuchukua hatua thabiti za kuthibiti ubadhirifu. Swala la BoT limepigiwa sana kelele, kama angekuwa na nia ya kuonyesha kwamba hapendi madudu angempiga chini Gavana pending uchunguzi, na baada ya uchunguzi akionekana hana makosa basi angerudishwa kazini na kuendelea kulitumikia taifa, lakini JK alifumba macho mpaka pale alipokuja kuwekwa kwenye kikaango na wafadhili kwamba madudu sasa yamevuka mipaka. Initially it was Twin Tower, sasa imeenda kwenye fedha za nje. Ina maana yeye alikuwa hayaoni aliyokuwa akiambiwa?

Kuna tuhuma ngapi ambazo BWM ametuhumiwa na bado JK amekaa kimya na hakufanya lolote na badala yake anakuja na cheap statement kwamba tumwache Mzee wetu apumzike!

Kwa hayo machache tu JK anaonyesha kwamba alikuwa analea uozo, na hapo ndipo inakuwa ngumu mwananchi kama mimi kuamini usafi wa JK katika swala zima la ufisadi.

Inawezekana kweli ni msafi na kama alivyosema Mwakafwila kwamba wasaidizi wake ndiyo wanamuangusha. Kama wasaidizi wake wanamuangusha kwanini asiwapige chini? Huwezi kumkumbatia mbadhirifu huku ukijua kwamba anakuharibia uongozi wako. Sasa hivi kila anakokwenda inabidi atoe majibu ya tuhuma za ubadhirifu zinazoendelea nchini kwake!
 
Aibu kubwa kwa kanisa. Nikiwa kama mkristo naumia sdana napo ona kuwa kuna watu wanatumia kanisa kama sehemu yao ya kupata umaarufu. Biblia yenyewe inatuonya sana kuhusu watu wa aina hii.
 
Kabla mwananchu hujapata kichefuchefu jiulize hawa ni maaskofu kweli wa Makanisa ama ni maaskofu wa vikijanisa ? Na mchango wao hawa umekuwa ni kitu gani kwa Taifa hili ama jamii ambayo inawazunguka ?

Nasema JK kama ni nabii basi nabii mbishi wa kupingana na waliomchagua na amekuwa nabii wa washikaji zale wala Nchi yetu .
 
hahahahaha... This non sense make me bust kucheka kazini. Hawa maaskofi ni wa momony nini? This is BS and real BS.
 
sasa sisi waumini tutakimbilia wapi kama hata hawa watu wa mungu wanadiliki kusema hayo? mimi naona huyo jamaa katumwa ili ccm wavune wanachama kupitia dini. kweli kiongozi wa kiroho unadiliki kusema hayo mbele ya jamii inayojua ukweli? mimi nafikiri JK akikubali ukweli kuwa kuna mafisadi na huyu jamaa wa dini ajiuzulu kwa kutetea mafisadi
 
Nadhani hii habari imepitwa na wakati, kama sikosei imetolewa takriban mwaka mmoja uliopita.
 
Maaskofu: Kikwete ni 'Nabii'

Habari Zinazoshabihiana
• Maaskofu: Kikwete ni 'Nabii' 31.05.2006 [Soma]
• Maaskofu wampa mtihani Kikwete na yeye awatega 09.06.2006 [Soma]
• Makamba afuata nyayo za Kikwete 10.07.2006 [Soma]

Maaskofu: Kikwete ni 'Nabii'
*Wasema hata manabii wa kweli walianza kwa matatizo
*Wadai hata shetani sasa amejenga hofu kubwa kwake
*Wawataka wananchi kuvumilia 'mitikisiko' inayotokea
Na Charles Mwakipesile, Mbeya .

hii habari ni ya lini sam?
 
duh,hiki nacho kichefuchefu,nabii gani anatembea nje ya ndoa!watu wengine wakikoswa jamba la kuongea bwana,Kikwete ni nabii wa mafisadi.
 
hii habari ni ya lini sam?


Well, pamoja na kwamba habari yenyewe ni ya 'zamani' kidogo lakini kutokana na hali halisi ya mambo hivi sasa imeonekana ni muhimu iwekwe hapa ili iwakumbushe hao maaskofu kuangalia , pengine huo utabiri wao kama hadi sasa hivi ni valid ama la!

Tunahitaji kukumbushana pale inapoonekana mambo yanakwenda kinyumbe na ilivotarajiwa, au tuseme wakati wa 'mapito' bado haujaisha?

Ni wakati wa kutafakari kila kinachosemwa na kila mmoja wetu...hata hao 'maaskofu'

Kwa upande wangu mi naona hiyo ni sehemu ya kampeni ya baadhi ya vyombo vya habari kutaka kumpa sifa Muungwana aonekane safiii mbele ya wananchi..maana mi naona habari yenyewe, na uaizto wake, na walioisema (no offence meant) inantia wasi wasi...
 
Unabii ni kitu kingine uwezi kufananisha na Nabii na Jk, Dini na Siasa.Lazima Ufikilie kwanza kabla ya kuandika hayo maneno yako
 
Viongozi wa dini walipoteza umaarufu pale waliposhabikia mambo ya siasa na kusahau kuwa wao ni wachungaji wa KONDOO. Yaani nao inabidi warudishe imani kwa wahumini kama KIKWETE anavyotakiwa kurudisha imani kwa WALALAHOI. Zamani kiongozi wa dini alikuwa mtu wa heshima kwenye jamii lakini siku hizi na "MAFISADI" wamo.
 
Kiongozi wa Dini makini, kamwe hawezi kukurupuka kunena maneno kama ya askofu cheyo. siamini kama Cheyo na wasaidizi wake walipata nafasi ya kutosha kutathmini mwenendo wa Serikali ya JK.

Ni kweli kwamba manabii huko nyuma walikumbana na misukosuko baadaye wakafanikiwa, lakini tofaouti na JK wale walikuwa wakichukua hatua zilizostahili na kwa uwazi. Mfano Yesu kuwafukuza wafanyabiashara katika hekalu, kuwasema hadhalani waandishi wa habari na mafarisayo n.k (wengine mtanisaidia manabii wengine)

Tulichoona kwa JK ni tofauti sana, akimwajibisha mtu, ni kumhamisha wizara, akifukuza mtu basi ni ngazi ya ukuu wa wilaya, katibu wa ccm wa wilaya, tarafa, kata n.k hatujaona hasa akigusa pale panapotakiwa.

Jk bado anayo nafasi ya kurekebisha mambo kama anayo nia, na kama dhamira inamsuta. Ugumu ni mtandao aliouunda, kwa maana nyingine dhambi ya kuanzisha makundi ndani ya CCM inamtafuna. anahitaji kuwa jasiri na Moyo wa paka kutengua mtego aliouweka mwenyewe.

Pengine viongozi wa dini wana maana hiyo kwamba akiliweza jinamizi hili basi kwa hakika anaweza kufananishwa na Nabii. hadi hapo atakapoweza ndipo tutakapowaunga mkono. vinginevyo kwa sasa naye anahesabiwa mmoja wao ktk utatu wao
 
Ingebidi tuwatafuta hawa wachungaji ambao wanachukunga kondoo wakati wao wenyewe wamepotea.. kama bado wanaamini kuwa JK ni nabii..
 
Ukifuatilia kwa makini unaweza kuta kuna kajimsaada wanakafukuzi ndo maana wanampamba JK.
Manabii wote kwa elimu yangu ya biblia kwa miaka sita wadeal na genuine problems za watu na always wanapewa directives na mungu mwenyewe kwa kila kitu waongeacho na kutenda.
Infact kila nabii anatumwa kwa watu kwa makusudi fulani akiwa na ujumbe maarumu kwa watu na si vinginevyo
Sasa nabii gani uyo anayehodhi watenda maovu,nabii gani anaewabagua watu kwa grounds za mtandao leave alone upinzani
Tusichanganye dini na siasa hasa siasa za Tanzania ambazo watu hawaoni ata haya kudhulumu mali za watu na umma kwa ujumla
 
Nyie mnajua namna watanzania wanavyofanywa wajinga na kuibiwa????

Kwanza viongozi
ambao wanaiba na kutapanya rasilimali za taifa kana kwamba ni urithi wao, na wanavyoiba wanafanya kitaalam kiasi kwamba watu wachache hustukia...

Pili viongozi wadini
baada ya wananchi kuibiwa kutoka ktk mfuko wao wa taifa, wanaibiwa na viongozi wa dini ambao wanawatuliza kwa kuwapa iai kwamba utajiri wa duniani hauna maana huku wakikusanya senti chache kutoka ktk mifuko ya wananchi hoooi.

Hivyo basi sioni ajabu kwa askofu (mwanadamu) kusimama na kutetea kwa kuupaka rangi ufisadi...
Eeee Mungu Tusaidie...
 
Kama kuna kundi moja la wanafiki Duniani ifikapo wakati wa kuongelea siasa, kundi hilo ni la viongozi wa Dini,tena dini zote duniani.

Viongozi wa Dini walikuwa nyuma ya Hitler wakati wa Unazi wake.
Viongozi wa Dini walikuwa nyuma ya Biashara ya Utumwa miaka yote ilipofanyika huko Amerika ,Ulaya Uarabuni na duniani kote.

Viongozi wa Dini walikuwa mstari wa mbele kuunga mkono ubaguzi wa rangi.
Viongozi wa Dini Duniani kote wamesaidia kuimarisha ukoloni wa iana zote.
Viuongozi wa Dini wamesaidia kuwagawa watu kwenye makundi ya kitabaka kwa kutumia misahafu.

Viongozi wa Dini mpaka leo hii wanaunga mkono ubaguzi wa namna zote ili kurahisisha aina yeyote ya utawala wa serikali.

Hawa maaskofu wanachofanya ni kuimarisha shughuli za ufisadi chini ya kivuli cha Dini.

Tena kwa taarifa yenu maneno waongeayo kutoka midomoni mwao si yao na hayatoki rohoni mwao wala si ya kiroho. maneno hayo Ni uzushi, wamewekewa midomoni ili wayaseme.

Ninafahamu kwa undani sana jinsi Mashirika mengi ya Dini yanavyotapatapa kiuchumi na jinsi yalivyo na uhanga wa fedha. Kwa mtaji wa uhanga wa fedha hayeshi kupokea vijisenti kutoka kwa Mahabithi Fisadi wa serikali ya SISIEMU na kueneza sumu kuabudu Uharamia katikati ya kondoo wa Bwana.

Hawa maaskofu wamesahau kwamba kazi yao kubwa ni Kueneza Ufalme wa Mbinguni si Ufalme wa Dunia hii.
Ufalme wa mbinguni haunezwi kwa kufungamana na Serikali yeyote Duniani.
Mtumishi wa Mungu yu tayari kufa kuliko kusalimu Amri na kueneza ufalme wa Fisadi yeyote Duniani.

Maaskofu hawa tuwaogope kuliko UKIMWI, UKIMWI unaua mwili lakini ujumbe wa ndimi zao unaua mwili na Roho.
 
Back
Top Bottom