JK kwenda Ufaransa leo

M

MegaPyne

Guest
Habari ni kwamba. JK anaondoka leo kwenda Ufaransa. atafanya ziara huko na pia kabla ya kurudi nyumbani, atakwenda kuonana na PAPA Benedict.

Habari zaidi zitawajia baadaye
 
Vasco Da Gama!

Labda ana kitu anataka kuvumbua! give him time.

By aliyekata tamaa ya maisha bora kwa kila Mtz
 
naona ni vizuri tu kwa mheshimiwa wetu asafiri every time he can, anaenda nje 2 wks anakaa nyumbani siku 4 ( mapokezi ya nguvu ) then anasafiri tena wk kadhaa ! wow ! i like that idea !
 
si mliambiawa safari z raisi zimezaa matunda? wana JF bwana vichwa vigumuuu dah! Mlishaambiwa ndege inapaa na raisi wenu hawezi kukaa Ikulu akichunga Njiwa huko au mmesahau aliyowambia Dr wetu Mchimbi kule Manyara? Mwache muungwana ale matunda ya utandawazi bwana ila sijui maraisi wetu wajisikiaje kwa safari zao za kuomba tuu kuomba tuu kila mara zaidi ya miaka arobani tunaomba tuu. May be sasa anaenda kupata baraka za papa ili mambo y arudi kwa msitari
 
Licha ya safari hii ya France na Italy pia kabla ya Mwaka kwisha atakwenda Japan na Spain na Katikati ya Novemba ana safari ya Uganda kwenye Commonwealth Summit!,Safari hii ya France/Italy pia anaambatana na Wafanyabiashara.
 
Duh, si angeunganisha Spain kwenye hii trip ya sasa hivi.Anyways wacha achome jet fuel...watoto wa mjini wanakwambia Jet fuel abuser(metaphor)
 
naona ni vizuri tu kwa mheshimiwa wetu asafiri every time he can, anaenda nje 2 wks anakaa nyumbani siku 4 ( mapokezi ya nguvu ) then anasafiri tena wk kadhaa ! wow ! i like that idea !

Hii kitu yako imenichekesha flani!!
haya bwana.....mambo ya shamba la bwana heri, na mbuzi wa bwana heri.......!!
 
Licha ya safari hii ya France na Italy pia kabla ya Mwaka kwisha atakwenda Japan na Spain na Katikati ya Novemba ana safari ya Uganda kwenye Commonwealth Summit!,Safari hii ya France/Italy pia anaambatana na Wafanyabiashara.

Jana tuu nilikuwa na wadau wa Japan wakawa wanasema siku aliyoenda Japan mwaka jana jamaa alikuja na watu wanaoitwa wafnya biashara lakini in real sense sio. Nikauliza kwanini wanasema hivyo? nikaambiwa waliokuja ni wajanja wajanja tuu waliopata pesa kutoka serikalini kwa njia ya tenda za serikali tuu. Jamaa akaendelea kukandamiza kuwa wafanyabiashara wenyewe hawako updated na issue za biasara za kisasa kama kutumia IT. Nikauliza amejuaje jamaa akaniambia inakuwa je mfanyabiashara anasafiri na raisi hana hata busness card? Tuliowapa busnes card zetu hawajawai kupiga wala kuandika e mail. Nikajisemea moyoni hao ndio wafanyabiashara wa Bongo land.
 
Good to be president. Let him have fun, who hate Limo rides, nice lunch and dinner, meet popular people in the world, look at the beautyful peace of structures. Let Mr President have good time.
 
KIKWETE KWENDA UFARANSA NA ITALIA;

Mwandishi WetUu,

HabariLeo; Monday,October 15, 2007 @00:02
RAIS Jakaya Kikwete anaondoka nchini leo kwenda Italia kwa ziara ya kikazi ya siku nane nchini humo na Ufaransa ambako pia ataonana na viongozi mbalimbali akiwamo Papa Benedicto XVI.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu jana ilisema akiwa Italia ambako anakwenda kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Romano Prodi, kesho atashiriki na kuhutubia katika sherehe za Siku ya Chakula Duniani ambazo zimeandaliwa na Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO).

Katika sherehe hizo ambazo hufanyika kila Oktoba 16, mada kuu itakuwa Haki ya Chakula ikisisitiza haki ya msingi ya mwanadamu kupata chakula, haki ambayo Shirika hilo linasema haizingatiwi ingawa kuna zaidi ya watu milioni 850 duniani kote ambao wana tatizo kubwa la ukosefu wa chakula.

Baada ya kuhudhuria sherehe hizo, Rais atakutana na kuwa na mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na viongozi wengine.

Keshokutwa atakuwa na mazungumzo na Waziri Mkuu Prodi wakati Alhamisi atashiriki mkutano utakaowakutanisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Italia.

Mkutano huo utafanyika Milan ukiwa na lengo la kuwashawishi wafanyabiashara na wawekezaji wa Italia kufanya biashara na wenzao wa Tanzania na kuwekeza nchini.

Ijumaa Rais Kikwete atakwenda Vatican ambako atakutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Benedicto XVI .

Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais kukutana na Baba Mtakatifu tangu ashike madaraka ya urais wa Tanzania.

Akiwa Italia, Rais atakuwa mgeni rasmi katika mkutano wa kimataifa unaowakutanisha viongozi wakuu wa madhehebu mbalimbali ya dini duniani (Interfaith Conference). Mkutano huo umeandaliwa na Jumuiya ya Sant'Egidio na utafanyika Napoli.

Rais amealikwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo kutokana na Tanzania kuwa nchi ya mfano duniani ambako watu wake wanaishi kwa maelewano, ushirikiano na amani bila ya kujali tofauti zao za dini na imani.

Baada ya kuhutubia mkutano huo, Rais atakwenda Ufaransa ambako atahudhuria Mkutano wa 34 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Mada kuu katika mkutano huo ambao hufanyika kila baada ya miaka miwili itakuwa ni Elimu na Maendeleo.

Akiwa Paris, Rais pia anatarajiwa kukutana na Rais Nicolas Sarkozy.

Rais na ujumbe wake wanatarajiwa kurejea nchini Oktoba 24.
 
Naona Kwa Papa JK anakwenda kuwashtaki akina Pengo! Haitasaidia, lakini Muungwana anapenda photo opportunity. Itapendeza sana akionekana ameshikana mkono Na Papa Benedict. Akumbuke basi kumpa mwaliko wa kuja Kariakoo!

Hao wafanyabiashara anaokwenda nao wanachekesha wakati mwingine. Nasikia kuna wakati mmoja wao alipeleka sample ya viatu vya ngozi ya chatu Marekani. Mmarekani mmoja akavipenda sana, na akatoa order ya pair 500. Masikini, mfanyabiashara wetu akasema anaweza kupata pair 10 tu! Tusiposomesha zaidi hatufiki popote!
 
Inachekesha sana, anaenda kuhutubia nini kwenye sherehe za siku ya chakula duniani wakati watu kibao huko vijijini wana shida ya chakula? Du I wish ningekuwa prezo wa Tz hata kwenye ndoto ili ni enjoy kutalii kila nchi kama muheshimiwa.
 
kumbe mimi ninaona heri ya beni aliyekaa ofisini kufanya biashara ambayo sasa hivi angalau inatutunzia fedha zetu kuliko huyu anyeenda kukaa guest za ughaibuni na kunufaisha wafanyabiashara wa huko.
 
Nashangaa na kustaajab, labda kwa kuwa sio mwansiasa au mwanadiplomasia.. ina maana mikutano yote ya nje lazima rais aende? ina maana hawezi kutuma mwakilishi kama waziri mkuu au makamu wake? Kuna hoja za msingi sana ambazo hajajibu kwa wananchi nashangaa anakimbia tena.. jamani wana JF tusiishie tuu kuandika kwenye hii forum popote ulipo tuwe mabalozi wa mageuzi. nchi hii inahitaji mapinduzi ya kweli sio blaaa blaa tuu. Mfano kule Nairobi vijana wote lazima weekend waende vijijini kwao na wakifika kule wanakaa na wazee wao wanawaeleza nini kinaendelea kwenye nchi yao hususani siosa. ndio maana wakiamua kwa kauli moja kuwa hawamtaki fulani wanampiga chini. sisi tunaolelewa ni wachache mno. naomba kuwasilisha
 
Hivi JK huwa ana muda wa kukaa chini wa kufikiri na kutafakari? Haishangazi hadi leo anasema hajui chanzo cha umaskini wa nchi ambayo yeye ni Rais!!
 
This is pathetic. Huyu jamaa hata hana aibu?? Nadhani anafanya makusudi maana anaona moto huku nyumbani umekua mkali sana na hivi akienda kuhutubia watu hawampigii makofi kama ilivyokua zamani anaona bora akajifariji kwa kuzunguka nchi za watu. He's a FOOL, a bigass FOOL.
 
Back
Top Bottom