Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,888
Mwandishi Wetu
Daily News; Saturday,March 29, 2008 @19:03
MWENYEKITI Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete juzi aliongoza harambee ya kuchangia CCM Mkoa wa Mara na kufanikiwa kukusanya Sh milioni 305. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais na Habari ilisema katika harambee hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Peninsula Beach Complex mjini Musoma Sh 50,600,050 zilikusanywa wakati ahadi ni Sh milioni 254.
Taarifa hiyo ilisema CCM mkoani Mara inakusudia kuzitumia fedha hizo kuendesha uchaguzi wa jumuiya mbalimbali za chama na pia kujenga jengo la kitega uchumi kukiwezesha kujitegemea katika fedha. Mbali na watu wengine Rais Kikwete ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM alichangia Sh milioni 15 na Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM) Nimrod Mkono Sh milioni 50.
Taarifa hiyo ilisema Rais Kikwete alihamasisha uchangiaji kwa kusema kuwa CCM ni chama kilichothibitisha kuwa kinaweza kutunza amani na hivyo kuchangia chama hicho ni kuchangia amani ya nchi.
Kama mnavyojua ndugu zangu, chama chetu ni chama ambacho kimedumisha amani ya nchi hii, hivyo hata kwa wafanyabiashara kuchangia CCM ni kuchangia amani na hakuna lolote, ikiwamo biashara inayoweza kufanyika bila nchi kuwa na amani, kwa hiyo nawaombeni ndugu zangu kuchangia chama chetu, alisema.
Mwenyekiti wa CCM yuko mkoani Mara kuhudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kilichoanza jana mchana katika Kijiji cha Butiama alikozaliwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.