Tsh. Milioni 10.6 Zapatikana Harambee Katika Kanisa la Waadventista Wasabato la Central Handeni Mjini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,076
1,001

Tsh. Milioni 10.6 Zapatikana Harambee Katika Kanisa la Waadventista Wasabato la Central Handeni Mjini

Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini, Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo tarehe 26/05/2024 alishiriki na kuwa mgeni rasmi kwenye Harambee ya Kanisa la Waadventista wasabato La Central Handeni Mjini kuchangia upatikanaji wa vifaa vya Kwaya na kupatikana Shilingi 10,651,400.

Akizungumza kwenye Kanisa, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini, Mhe. Kwagilwa Nhamanilo amechangia ununuzi wa vifaa vya muziki vya Kwaya na amewashukuru sana watu wote waliojumuika na kuiwezesha Harambee ya ununuzi wa vyombo vya muziki vya Kwaya kufanyika kwa mpangilio mzuri hata kupata Shilingi Milioni 10.6.

Mbunge Kwagilwa Nhamanilo amewashukuru sana viongozi wa CCM Handeni Mjini (Wajumbe wa Kamati ya Siasa, Wenyeviti wa Kata, Makatibu wa Kata, Wenezi wa Kata, Madiwani) wakiongozwa na Mwenyekiti Changogo, DC Msando, Mkurugenzi, Taasisi mbalimbali, Wafanyabiashara, Kwaya za Makanisa mbalimbali, Viongozi wa Dini zote, Wananchi, Waumini wote, wageni waalikwa na kwa namna ya pekee sana Mwenyekiti wa Halmashauri Ndugu Mussa Mkombati.


WhatsApp Image 2024-05-27 at 15.14.27.jpeg
WhatsApp Image 2024-05-27 at 15.14.28.jpeg
WhatsApp Image 2024-05-27 at 15.14.28(1).jpeg
 
Back
Top Bottom