JK awaonya wanafunzi wa vyuo vikuu kutojiingiza katika siasa

chidide

Member
Nov 11, 2010
91
0
Kikwete awaonya wanafunzi vyuo vikuu:

Imeandikwa na Mwandishi Maalumu, Dodoma; Tarehe: 27th November 2010 @ 07:20 Imesomwa na watu: 333; Jumla ya maoni: 0


RAIS Jakaya Kikwete, amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, kujiepusha kutumiwa na wanasiasa na badala yake kuelekeza nguvu zao katika masomo.

Alitoa kauli hiyo mkoani hapa jana katika mahafali ya kwanza ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na kuwaasa kuwa wanasiasa wanafanya hivyo kwa maslahi yao kwa kuwa walishamaliza masomo yao.

“Kwa nyie mnaoendelea na masomo yenu, elekezeni nguvu zenu kwenye masomo. Hilo ndilo lililowaleta hapa. Msikubali kurubuniwa na wanasiasa. Hawa wanataka kuwatumia tu kwa manufaa yao kwa sababu masomo yao walikwishamaliza.

“Ukijiingiza katika michezo hii ya siasa ni dhahiri utaharibikiwa. Ama utashindwa na kulazimika kurudia masomo ama utafukuzwa kabisa baada ya kushindwa kupata alama za kukuwezesha kuendelea mbele au hata kurudia mitihani,” alisema Rais Kikwete ambaye pia alitunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima (PhD).

Aliwaasa wanafunzi hao kujishughulisha na jukumu lililowaleta chuoni hapo ambalo ni kusoma na wala siyo kushiriki siasa.

“Msiwape nafasi wanasiasa kwa sababu watawaharibieni muda na malengo yenu. Mtawaharibia wazazi wenu mipango yao waliyokuwa nayo kwa kuwaleta chuoni.”

Ingawa hakuweka wazi sababu ya kutoa onyo hilo kama Rais na mzazi, lakini katika miaka ya hivi karibuni, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekuwa kikitumia siasa za ndani ya vyuo vikuu nchini, kuhamasisha vijana kujiunga na chama hicho.

Baada ya kupewa Shahada hiyo ya heshima, Rais Kikwete aliitunuku kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Watanzania wote wa Tanzania kwa kuunga mkono kwa dhati sera ya Serikali yake ya kuifanya elimu kuwa sekta kiongozi katika mgawo wa bajeti.

Mbali na Rais Kikwete, UDOM pia imemtunukia PhD mwanasiasa mkongwe wa Tanzania, Hayati Rashid Mfaume Kawawa ambaye alifariki dunia mwishoni mwa mwaka jana.

Mpaka sasa UDOM ambacho ndio chuo kikuu kikubwa kuliko vyote nchini, kina eneo lenye nafasi ya kilometa za mraba 15,600, wanafunzi 20,000 kati ya wanafunzi 40,000 watasoma kwenye chuo hicho ujenzi utakapokamilika.

Rais Kikwete amerejea Dar es Salaam jana jioni kutoka Dodoma na leo atakuwa na shughuli ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri.
Source: Habari leo


Najiuliza: Hivi wakati hawa wanafunzi wa UDOM wanamtolea mchango (1 Million) wa kuchukua fomu za kugombea urais mbele ya kadamnasi mbona hakuwakatalia????????
AU IKIWA NI YEYE SAWA BUT WENGINE NONGWA???????

Na hili gazeti la habari leo halioni aibu kila kibaya kuhusisha na CHADEMA????????????
 

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
3,737
2,000
Eti wanaowatumia walishamaliza masomo! Yeye alishamaliza masomo kweli?
Kumbe wakishaingia siasa wanadhani walishamaliza masomo!
 

MashaJF

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
246
195
Nafikiri anakosa ujasiri wa kusema wanafunzi ni ruksa kushangalia CCM na siyo vyama vingine.
 

kayumba

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
653
195
Najiuliza: Hivi wakati hawa wanafunzi wa UDOM wanamtolea mchango (1 Million) wa kuchukua fomu za kugombea urais mbele ya kadamnasi mbona hakuwakatalia????????

Hapa umenena mkuu!
 

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,180
2,000
Kwa hiyo wakati wana mchangia ile milioni kikwete hakua mwanasiasa? michezo mingine bwana kama ya watoto flani ivi, bytheway amekubali kiaina kua SLAA ni msomi
 

Mallaba

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
2,556
1,170
atueleze ,je kuna kiongozi gani ambaye hakupitia vuguvugu la chuoni kwa njia moja ama nyingine? mbona wanakuwa sio wakweli hawa viongozi wetu? wanataka wao tu ndio wawe viongozi na usultani wao.....lol:whoo:
 
Nov 23, 2010
50
0
Hii ni baadhi tu ya michango yake ambayo walio mpa huo udaktari wa heshima wameiona na akawa na sifa za kupewa. Lakini mtu aliyefilisika kisiasa mlifikiri ataongelea nini zaidi ya udini na kutoa ushauri uliochoka kama huu. kuanguka kwa mwanasisa kunapitia misukosuko mbalimbali kama ilivyo kufanakiwa kwake. Huyu bwana ni mwanasisa aneyepita katika misukosuko ya kuanguka kwake, natumuache pengine matokeo yake yatakuwa ndio kuokoka kwa TZ.
 

bernardp

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
619
1,000
"Ukijiingiza katika michezo hii ya siasa ni dhahiri utaharibikiwa. Ama utashindwa na kulazimika kurudia masomo ama utafukuzwa kabisa baada ya kushindwa kupata alama za kukuwezesha kuendelea mbele au hata kurudia mitihani,"

Hapa ni dhahiri kuwa waliompa (PHD) ya heshima walikosea. Ninaomba ufafanuzi kama kutakuwa na mpango wowote wa kuwahujumu wale vipanga wanapenda kunoa akili zao kwa critical thinking and analysis. Inanipa hofu kama mpenda elimu.
 

Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
14,155
2,000
Jamani, aisee, JK mbona unajisema mwenyewe? Si ww juzi unagombea Urais, hawa wanafunzi UDOM ndio uliwatumia wakuchangishie 1 mil, wakishangilia kila kona hapo Dodoma, yaani, just fews days kila mtu anakumbuka, sasa, unasema nini, anyway, i had never & i will never trust u, uongo mwingine, mmmhh, acha usanii plse
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom