JK atoa miezi sita CCM kutafuta sababu za kushindwa

Inashangaza sana nchi ambayo amigubikwa na matatizo kibao bado mpaka leo wanapongezana,hilo ni tatizo kubwa sana.Mimi naamini kabisa JK hana sifa za kuiongoza nchi hii wala hakutakiwa kupewa nafasi kamwe na yeye kupata nafasi hii ni matunda ya ufisadi kwani chini ya utaratibu wa kawaida wa kuchaguana ccm isingekuwa rahisi kuwazidi kina Salim.JK alipita kugombea urais kwa mbinu chafu na tutegemee ujinga hivyo hivyo mpaka kipindi chake kiishe.
 
Huyu rais DUDU?????

1. Hajui kwa nini tanzania ni maskini???????????????
2. Hajui kwa nini sababu za ccm kushindwa?????????????
Watanzania imekula kwetu.
 
Huyu rais DUDU?????

1. Hajui kwa nini tanzania ni maskini???????????????
2. Hajui kwa nini sababu za ccm kushindwa?????????????
Watanzania imekula kwetu.

siku zote CCm haitafuti majibu rahisi kwa maswali magumu, ingekuwa akina fulani wangekwisha kurukupuka CHAKACHUA.
 
Huyu jamaa na UWT yake (mashushu ya CCM) kweli ni vilaza. Yani hadi sasa hawajajua sababu za kushindwa?! Aisee jamaa ni mweupe upstairs. No wonder hadi kesho hajui sababu za waTZ kuwa masikini!
 
Labda atoe miaka 23 tena (yaani iundwe CCM accademia) kwa kuwa chamachenyewe kina umri huo NAMSHAULI aongeze kama hiyo....
Mpuuzi tu yeye na M/Kiti wa UWT
 
Huyu jamaa na UWT yake (mashushu ya CCM) kweli ni vilaza. Yani hadi sasa hawajajua sababu za kushindwa?! Aisee jamaa ni mweupe upstairs. No wonder hadi kesho hajui sababu za waTZ kuwa masikini!

Angekuwa angalau ANA KITU KUMKICHWA angejitahidi japo KUJUA WATANZANIA WANATAKA NINI KWA SASA..... basi angewatimizia .... ILA kutwa kucha anaangalia RA, EL, na riz1 wanataka nini na kuwatimizia..... CCM ni sawa na kusifia YULE PUMNDAMILIA ANA HIPS NZURIIII........... wanakati MAPUNDA YENYEWE HAYAANGALII MAUMBILE WAKATI WA KUTAKA MAJAMBOZI
 
Sababu kubwa ya ccm kushindwa ni moja tu, kushindwa kuchakachua matokeo katika majimbo ambayo watu walisimamia kura zao. Labda Jk awaulize wenzake walishindwa vipi kuchakachua katika majimbo hayo na kwa swali hili haiitaji miezi sita
 
Six months....? Give me 10 minutes and i will tell you why?... Free of charge ofcourse

Jamani hivi hatujamwelewa tu JK, ndio uwezo wake uko hivyo, usishangae akaunda tume ya kuchunguza uwepo wa mgao wa umeme na kuipa mwaka mmoja. Chini yake kitu chochote cha kushangaza kinawezekana
 
sababu za kushindwa anazo yeye mwenyewe wala asitafute mchawi....au km vp amuulize sheikh yahaya...............ajiulize kwa nini misafara yake huwa inapopolewa mawe km huko mbeya,,,,kwa nini anazomewa sehemu mbalimbali?......kwa nini mawaziri wake wanazomewa pia?.......kikwete anafikiri haya yote ni kwa sababu watz wana furaha naye?...............yeye ndiyo chanzo cha kukosa ushindi kwa KUKUMBATIA MAFISADI NA UDINI WAKE KIKWETE HAS TO HIMSELF PAY FOR THE RESULTS.
 
Tathmini ni muhimu. CCM tukifanya tathmini ya kina, ya kisayansi na ya kijasiri, mwaka 2015 asilimia 80 ya viti vilivyokwenda upinzani Tanzania Bara vitarudi CCM. Hata CHADEMA wangefanya tathmini ya kweli kujua kwanini Slaa hakushinda au angalau hawakupata wabunge zaidi ya 80 wa majimbo kama walivyojigamba awali ingewasaidia. Bahati mbaya tathmini yao inaishia kwenye wimbo wa CCM wamechakachua kura! Tathmini ya aina hii itawapeleka kaburi la kisiasa mwaka 2015. Mimi siwapendi Chadema lakini nawapa tu ushauri wa bure.

kusema ukweli nakubaliana na ushauri wako.. kuna mambo mengi Chadema inabidi wajifunze.. kwa sababu suala si uchakachuaji tu.. kuna mamnbo mengi zaidi ya hapo... mimi nawapongeza CCM kwa kusema wanataka wajitathimini kuona wapi wamekosea.. kwa hiyo Chadema jitahidini, acheni longolongo za kutaka kufukuzana.. kaeni chini mrekebishane na muweke mkakati wa pamoja wa kufanya kazi na wananchi katika kuleta maendeleo na wakati huohuo kuweka mkakati madhubuti wa 2015. kumbuka kuna kundi kubwa la vijana walio secondary za kata watakuwa wamefikisha miaka 18!! je mna mpango gani kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa (hili nalo ni suala muhimu sana katika uimarishaji vyama)..
 
Ndani ya mwezi mmoja hata JK atakuwa amesahau alichokiongea achilia mbali hiyo miezi sita..
 
Hivi huyu JK mambo ya inchi huwa anaomba ushauri kwa mkewe na Ridhiwani tu? hasikilizi watu wengine
 
MWENYEKITI wa CCM, Jakaya Kikwete amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho katika ngazi zote, kuaangalia kwa makini mambo ambayo yalisababisha chama hicho kushindwa kwenye baadhi ya maeneo katika uchaguzi mkuu uliopita.

Hii itakuisaidea ccm endapo watakao wafanyia tathimini watawaeleza ukweli badala ya kukimbilia kwenye mambo kama udini! Ni vyema hata Chadema na Cuf wapitie mchakato huu ili 2015 wote wajue pakeweka nguvu zao!

“Shabaha yetu ni kuimarisha yale tuliyofanya vizuri, tufanye tathmini hii mapema ndani ya miezi hii mitatu au sita iwe imekamilika, tufanye tathimini katika ngazi zote, tukikamilisha tutajua wapi tumekosea wapi tumefanya vizuri, kwenye uchaguzi mkuu ujao tutaingia tukiwa na uhakika,” alisema Kikwete ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Hapa nakupa angalizo kuwa kuchakachua sio sehemu ya kufanya vizuri, najua wengine watataka njia za ushindi kwa njia yoyote ile ziigwe!

Kikwete ambaye alitoa hotuba fupi, aliwataka pia viongozi wa jumuiya hiyo, kuhakikisha wanawashawishi vijana na wasomi kujiunga katika jumuiya hiyo ili kuzidi kukiimarisha chama hicho.


Vijana wasomi itakuwa ngumu kuwashawishi kwasababu wanaona jinsi gani chama kisivyofuata kanuni na malengo yaliyohainishwa vitabuni YAANI CHAMA CHA WAKULIMA NA WAFANYAKAZI badala yake wenye nguvu ni MATAJIRI. Nakutahadhalisha: Vijana wa somi utakao wapata wengi wao watakuwa wale waliolenga maslahi yao nafsi na si maslahi ya taifa.



Alisema juhudi za wanawake ndizo zilizokisaidia chama hicho kuibuka na ushindi, huku akiwaelezea kuwa walikuwa wakijitokeza kwa wingi katika mikutano ya kampeni pamoja na siku ya kupiga kura.

Tunajua idadi ya wanawake ni kubwa katika Tanzania na duniani kwa ujumla, vyama vyote vichukue ushauri wa Mkuu wa kaya na vijitahidi kuwa na ushawishi kwa kundi hili.

Awali, Mwenyekiti wa UWT mkoani Dar es Salaam, Zarina Madabida, alimtaka Rais Kikwete kutomfumbia macho kiongozi yeyote atakayekwamisha utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2010/15.

Orodha ya hao ni ndefu, ila aanze na hawa wanaotaka hela yetu yote iende kwa DOWANS

Wakati huo huo, Rais Kikwete aliwakumbusha kuwa ukomo wa nafasi ya ubunge wa viti maalumu kupitia CCM utakuwa ni miaka 10 na kwamba baada ya kipindi hicho wabunge ambao watahitaji kurudi bungeni watalazimika kugombea kwenye majimbo,
“Tunataka viti maalumu iwe ni sehemu ya kujifua, baada ya vipindi viwili itabidi muende majimboni mkapambane,”

Tekeleza hili kwa matendo manake kama ni kusudio tumesikia tokea Sofia Simba alivyoingia madarakani!

Mwisho

Tutafurahi kama tathimini itawekwa adharani ili kama kuna makosa tuelezane!
 
Back
Top Bottom