Facts1
JF-Expert Member
- Dec 23, 2009
- 307
- 28
Monday, 06 December 2010 08:45 Fredy Azzah
MWENYEKITI wa CCM, Jakaya Kikwete amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho katika ngazi zote, kuaangalia kwa makini mambo ambayo yalisababisha chama hicho kushindwa kwenye baadhi ya maeneo katika uchaguzi mkuu uliopita.
Kikwete ambaye ni rais wa Jamhuri Muungano Tanzania, alisema hayo juzi jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Jumuiya wa Wanawake wa chama hicho (UWT) Biafra wilayani Kinondoni.
Shabaha yetu ni kuimarisha yale tuliyofanya vizuri, tufanye tathmini hii mapema ndani ya miezi hii mitatu au sita iwe imekamilika, tufanye tathimini katika ngazi zote, tukikamilisha tutajua wapi tumekosea wapi tumefanya vizuri, kwenye uchaguzi mkuu ujao tutaingia tukiwa na uhakika, alisema Kikwete ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Kikwete ambaye alitoa hotuba fupi, aliwataka pia viongozi wa jumuiya hiyo, kuhakikisha wanawashawishi vijana na wasomi kujiunga katika jumuiya hiyo ili kuzidi kukiimarisha chama hicho.
Alisema juhudi za wanawake ndizo zilizokisaidia chama hicho kuibuka na ushindi, huku akiwaelezea kuwa walikuwa wakijitokeza kwa wingi katika mikutano ya kampeni pamoja na siku ya kupiga kura.
Mnaotakiwa kupongezwa leo (juzi) ni nyie.., kupitia nyie hata wanaume na vijana walikipigia kura Chama Cha Mapinduzi, alisema Kikwete.
Alisema serikali yake itaendelea kutoa nafasi za juu kwa wanawake, ili kutimiza lengo la usawa kitu ambacho alieleza kuwa ni sera ya CCM.
Kikwete alisema serikali yake itaendelea kuzitafutia ufumbuzi mila mbalimbali ambazo zinazowagandamiza wanawake na watoto.
Alifafanua kwamba, sambamba na hilo tume ya kurekebisha sheria inaendelea kupitia na kurekebisha sheria mbalimbali zinazogandamiza wanawake na watoto.
Awali, Mwenyekiti wa UWT mkoani Dar es Salaam, Zarina Madabida, alimtaka Rais Kikwete kutomfumbia macho kiongozi yeyote atakayekwamisha utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2010/15.
Alimtaka kuendelea kutoa mikopo ya fedha mabilioni ya JK na kumuomba ahakikishe kuwa masharti ya kuombea fedha hizo yanapunguzwa.
Yale mabilioni yalitusaidia sana na tunaendelea kuunda vikundi ili kujikwamua, tunaomba uendelee kuzitoa hizo fedha lakini utusaidie ili mashariti yake yapunguzwe, alisema Madabida.
Wakati huo huo, Rais Kikwete aliwakumbusha kuwa ukomo wa nafasi ya ubunge wa viti maalumu kupitia CCM utakuwa ni miaka 10 na kwamba baada ya kipindi hicho wabunge ambao watahitaji kurudi bungeni watalazimika kugombea kwenye majimbo,
Tunataka viti maalumu iwe ni sehemu ya kujifua, baada ya vipindi viwili itabidi muende majimboni mkapambane, alisema
Alisema CCM imeamua utaratibu huo ili kuondoa dhana ya wanawake kubebwa na pia kupunguza malalamiko katika uteuzi wa viti hivyo.
Mambo ya kusema huyu kapendelewa yataisha, lakini muongeze ushirikiano na umoja, wanawake mkishikana hakuna mwanaume atakayewaweza, kwenye uchaguzi wa mwaka huu tumeona mmewatoa wanaume jasho kweli, ile dhana ya kuwa ukigombea na mwanamke unaona umepata mteremko sasa haipo, aliongeza Kikwete.