JK ateua Mkurugenzi Mtendaji TANESCO

Shirika la ovyo sana, JK ni moja ya watu walioliangamiza kwa kuingia mkataba wa kifisadi na IPTL, akiwa ni waziri wa nishat na madini,

Mkuu, unaweza kutuwekea tuhuma za ufisadi za JK, kama ambavyo ilitajwa na Dr. Slaa pale mwembe yanga temeke?

Mkurugezi aanzie na hapo, kisha ashushe gharama za bei ya umeme.
Huyu si alituhumiwa na mwenyekiti wa bodi kwa maamuzi yenye shaka???
 
MKATA KIU Idrisa Rashid Bwn vijisenti Alimfungulia ACCT huko New Jesy akamuwekea Pound Stearing 600,000/".
Alipo hojiwa akadai alipewa kununua fenicha, mara kufuga kuku!! Sifa zake ziliishia pale!!
Nchi ni gonjwa inahitaji oparation
Kuondoa uozo CDM wanaweza kazi hiyo, wapewe!!
 
Last edited by a moderator:
Eng Mramba amekuwa kaimu wa nafasi hiyo kwa mda mrefu tangu alipofukuzwa kazi Eng Mhando,

Ninamfahamu vizuri na ni rafiki yangu wa karibu, uzuri zaidi nikuwa jamaa ni mtu wa kiroho yani ni mlokole halisi asiyependa njia za mkato, Amekumbana na urasimu wa wanabodi wakiongozwa na Gen Mboma hasa wakishinikiza ishu za dowansi lakini wameshindwa na sasa tanesco imeongezw ukusanyaji wa mapato kutoka milioni 12 kwa siku hadi 50milioni kwa siku, haya ni mafanikio makubwa kwake.

Kwa utendaji na uadilifu sina hofu nae labda abadilike baada ya kukabidhiwa kiti rasmi,
Hii ni taarifa njema. Tumuombee afanye kazi kwa ufanisi ingawa kuna habari last week katika Mawio ikimhusisha katika ugomvi mkubwa na Mboma.
 
Rais Kikwete jioni hii amemtangaza rasmi Mhandisi felchesmi mramba kuwa mkurugenzi mtendaji wa Tanesco uteuzi ambao umeanza rasmi leo hii
Mramba ni msikivu na anafuatilia hata jambo dogo.
Nilimwona kwa tatizo langu pale Mbeya na alilitatua kirahisi baada ya kuona karibu natapeliwa na vishoka waliokuwa na uongozi wa Tanesco Mbeya.
 
Felichesmi Mramba ameokoka, ni mzee wa Kanisa la TAG Ubungo. Wakati mwingine husimama madhabahuni kuhubiri. Hivyo naamini ni mtu safi, ana msimamo, kwa hivyo kama Gen Mboma ni fisadi, watatofautiana sana kimtazamo.
Kuokoka sio hoja sana mkuu kwani hivi sasa wachungaji na wanaojiita manabii ndio vinara wa ubakaji kama ilivyptokea Dodoma, Mbeya na hata kesi ya kuwatia mimba waumini wao kama kiongozi wa kanisa moja maarufu la kilokole pale Mwenge. Usiamini sana watu kutokana tu na kitu kiitwacho kuokoka.
 
huyu eng. Mramba ni mtu makini na asiyehongeka kirahisi (kwa kumbukumbu zangu za nyuma.). Nina furahi kusikia kwamba hata eng. Boniface njombe ni mtu wa kaliba hiyo hiyo. Labda jambo la kujiuliza hapa ni , je hawa watu wataruhusiwa kufanyakazi kwa kuzingatia weledi wao? Je hawa watu watawezeshwa kufikia malengo ya shirika? Ningeomba yeyote mwenye taarifa za zaidi kuhusu huyu eng. Mramba aziweke hapa.

sifa kuu ambao wengi hawapendi kusikia na kuiamini ni kuwa huyu mtu ni mcha mungu kwa jina lisilopendwa na wengi mlokole.fuatilia usibishe tu kwa atakayetoa comment
 
kuokoka sio hoja sana mkuu kwani hivi sasa wachungaji na wanaojiita manabii ndio vinara wa ubakaji kama ilivyptokea dodoma, mbeya na hata kesi ya kuwatia mimba waumini wao kama kiongozi wa kanisa moja maarufu la kilokole pale mwenge. Usiamini sana watu kutokana tu na kitu kiitwacho kuokoka.

kaka panua fikra kidogo kwani akitokea muislam mmoja kala kitimoto ndio tunajenga hoja kuwa hakuna uislam, au hakuna muislam aliye muaminifu, hiyo ni fallacy- hasty generalisation
 
I wish hawa wateule wangekuwa wanapewa malengo yaliyowazi i.e performance criteria na performance standards zingewekwa hadharani ili mwisho wa siku wakishindwa kutimiza malengo wawajibishwe! its all about deliverables ...
 
huyu mramba siyo yule yule mramba jamani? kwani hakuna watu wengine ambao hata majina ya wazazi wao sio makubwa wanaoweza hizi kazi nao wakapewa nafasi jamani?:bored:
 
Acha kutumia data za vijiweni. Kama hujui uliza. Mramba kafanya B.Sc. in Electrical Engineering na alimaliza 1996 - UDSM - Faculty of Engineering (FoE) kama ilivyokuwa inaitwa wakati huo. Alirudi kufanya MBA baadaye.

Hivi Mramba amekuwa mhandisi lini? Alimaliza BA pale Chuo 1995, uhandisi una misingi yake na sijui kama kufanyia Tanesco muda mrefu mtu anweza kujiendeleza hadi akwa mhandisi kamili?
 
Kwisha habari ya Taa ne sconga! Maana imedhihirika sasa kuwa hilo shirika ni la wapare na wachaga, na kwa sababu jamaa wamevamia mapenzi kwa kasi ya upepo basi hatutashangaa kusikia kuwa ili upate umeme lazima uwe nyumba ndogo ya meku au baba dhao! Wameuza shirika kwa bei ya kujigawia! Bye bye shirika bovu lililobaki linasuasua!
 
Uliwahi kumuhonga Bw. Njombe akakataa? Kwani kwa kawaida watumishi wa umma husaidia [hupendelea] watu wa makabila yao? Na je hayo ndiyo matarajio ya wananchi wa makabila mbalimbali re. mtu wa kabila lako katika ofisi ya umma atakusaidia/atakupendelea? Na unataka wasomaji wa ujumbe wako tuamini kwamba Bw. Njombe ana sifa za kuwa mtendaji mkuu wa TANESCO kuliko Bw. Mramba? Au ulitegemea tu Bw. Njombe ateuliwe? I think you are making rather a too general statement to be taken seriously. Na kwanini hawa wakuu wa mashirika wanateuliwa? Kwanini wasishindanishwe na mwenye kushinda apewe kazi ya kuongoza shirika. Uteuzi siku zote unazingatia value judgment na hivyo kwa asili ni biased.
Umeongea kama vile unatokea kwenye Sayari mpya ambayo haina contamination!
 
Kuokoka sio hoja sana mkuu kwani hivi sasa wachungaji na wanaojiita manabii ndio vinara wa ubakaji kama ilivyptokea Dodoma, Mbeya na hata kesi ya kuwatia mimba waumini wao kama kiongozi wa kanisa moja maarufu la kilokole pale Mwenge. Usiamini sana watu kutokana tu na kitu kiitwacho kuokoka.
Hii ni commentya kijima kabisa na fyongo, yenye nia tofauti kabisa na mada ya awali...ukiitazama kwa jicho la 3 utaona kuwa ina mkono uliofichama
 
Hongera Mate Wa Kibaha Secondary Eng Felchism Mramba uadilifu wako ni Tunu kwa TANESCO na Taifa. Umefata nyayo za Dr Kazaura Kamugisha Dir General TTCL. I'm proud of you guys.

TTCL kuna progress gani so far zaidi ya shirika kuangamia?
 
Labda kwa mengine ila kwa ubadhirifu huyu jamaa ninamjua kuwa sio mbadhirifu kabisa maana ni mtumishi wa Mungu aliyetukuka... labda abadilike. Nimewahi kuwa nae kwenye kanisa moja la Assemblies of God(TAG) na kwa kwa kweli si wa kumtilia shaka uaminifu wake ... naamini kwa hapa mafisadi walie tu..

Let's be patient and see if he can deliver. Time will tell. Let's also not forget that everybody has a price
 
Du! Mungu mkubwa. Mafisadi wamejitahidi kwa kila njia kuhakikisha jamaa hashiki position maana aliwazibia ulaji. Ukisikia mtu anatetewa na Maswi ujue jembe huyo. God bless u Mramba.
 
huyu mramba siyo yule yule mramba jamani? kwani hakuna watu wengine ambao hata majina ya wazazi wao sio makubwa wanaoweza hizi kazi nao wakapewa nafasi jamani?:bored:
Wewe ungesomea engineering labda ungefikiriwa. Hii nafasi inahitaji Mhandisi tena aliyefauu vizuri. We kalaga baho.
 
Back
Top Bottom