JK Ateua Makamishna wa Tume ya Haki za binadamu

Gembe

Gembe

JF-Expert Member
2,505
1,225
Heshima Mbele,naomba kuwaletea uteuzi mpya alioufanya Muungwana na atwaapisha leo..naomba muangalie majina ya hao watu na wasifu wao..

Jaji Amiri Ramadhan Manento---Mwenyekiti wa Tume
Mahfoudha Alley Hamid---Makamu wa mwenyekiti wa tume hiyo.

Joaquine De Mello -kamishna
Zahor Juma Khamis -kamishna
Bernadeta Gambishi-kamishna

Jaji Manento::---alistaafu nafasi ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Januari Mahfoudha Hamid:--aliyewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (2001-2006De Mello ni wakili wa kujitegemea,
Khamis ni mfanyabiashara
Gambishi ni Katibu wa Mkoa, Idara ya Huduma kwa Walimu Mkoa wa Shinyanga.
 
M

Mtanzania

JF-Expert Member
4,818
1,225
Mkuu Gembe,

Hivi hii tume inafanya kazi gani? Naona haki za msingi za Watanzania wengi
kama wale wa Tabata zinavunjwa na sijwahi hata siku moja kuwasikia wanasema neno.

Je tume kama hiyo kweli kuna haja ya kuwa chini ya serikali? Kama kuna ukiukwaji wa haki za binadamu TZ, basi kwa sehemu kubwa kunafanywa na serikali, sasa hiyo tume kuteuliwa na rais naona kunainyima kabisa makali ya kuikosoa serikali.
 
Masanilo

Masanilo

Platinum Member
22,295
1,250
Heshima Mbele,naomba kuwaletea uteuzi mpya alioufanya Muungwana na atwaapisha leo..naomba muangalie majina ya hao watu na wasifu wao..

Jaji Amiri Ramadhan Manento---Mwenyekiti wa Tume
Mahfoudha Alley Hamid---Makamu wa mwenyekiti wa tume hiyo.

Joaquine De Mello -kamishna
Zahor Juma Khamis -kamishna
Bernadeta Gambishi-kamishna

Jaji Manento::---alistaafu nafasi ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Januari Mahfoudha Hamid:--aliyewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (2001-2006)De Mello ni wakili wa kujitegemea,
Khamis ni mfanyabiashara
Gambishi ni Katibu wa Mkoa, Idara ya Huduma kwa Walimu Mkoa wa Shinyanga.
Kuna mwenye wasifu wa dada Joaquine De Mello isije kuwa muungwana analipa fadhila....
 
Mtu wa Pwani

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
4,161
1,250
Kuna mwenye wasifu wa dada Joaquine De Melloisije kuwa muungwana analipa fadhila....
kazi si ndogo JK akichagua mwanamke analipa fadhila ?

mengine mnajiaaibbisha wakuu
 
C

CHAUMBEYA

Member
69
0
Kuna mwenye wasifu wa dada Joaquine De Melloisije kuwa muungwana analipa fadhila....
JOAQUINE DE MELLO AMETOKA KUMALIZIA TERM YAKE KAMA RAIS WA CHAMA CHA MAWAKILI TANGANYIKA(TANGANYIKA LAW SOCIETY)ITS INTERESTING TO KNOW KUWA WAO HUWA HAWAITAMBUI NCHI YA TANZANIA. JOAQUINE ALIKUWA NDIYE RAIS WA KWANZA MWANAMKE WA CHAMA CHA MAWAKILI TOKA KIANZISHWE MWAKA 1925. AMEKUWA PIA MWANACHAMA WA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE TANZANIA (TAWLA) KWA MIAKA MINGI.

KWA KWELI NAAMINI AMEKWENDA KULE BY MERITS NA ANAKUBALIKA.
KWA WANAOMFAHAMU WATAKWAMBIA KUWA JOAQUINE NI MWANAMAMA MREMBO MNO ALIYEJALIWA. LABDA HILI NDILO LINALOLETA HISIA ZA KULIPA FADHILA ILA MIMI HILO SILIJUI.
 
BabaH

BabaH

JF-Expert Member
704
195
kazi si ndogo JK akichagua mwanamke analipa fadhila ?

mengine mnajiaaibbisha wakuu
Hii niko pamoja nawe kwa 100% mkuu
sio kweli kwamba kila mwanamke akichaguliwa fikra ziwe kulipa fadhila, yawezekana hao wanawake wengine wanastaili kupata nafasi hizo, ina wezekana fadhila wanapewa wengine tusiowajua
Naomba tufuate utaratibu wa kuangalia wadhifa na mafanikio ya viongozi wanaoteuliwa na Mh. Kabla ya kuanza kujaji uteuzi wa hawa jamaa wa Mh. Kila siku
 
Masanilo

Masanilo

Platinum Member
22,295
1,250
JOAQUINE DE MELLO AMETOKA KUMALIZIA TERM YAKE KAMA RAIS WA CHAMA CHA MAWAKILI TANGANYIKA(TANGANYIKA LAW SOCIETY)ITS INTERESTING TO KNOW KUWA WAO HUWA HAWAITAMBUI NCHI YA TANZANIA. JOAQUINE ALIKUWA NDIYE RAIS WA KWANZA MWANAMKE WA CHAMA CHA MAWAKILI TOKA KIANZISHWE MWAKA 1925. AMEKUWA PIA MWANACHAMA WA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE TANZANIA (TAWLA) KWA MIAKA MINGI.

KWA KWELI NAAMINI AMEKWENDA KULE BY MERITS NA ANAKUBALIKA.
KWA WANAOMFAHAMU WATAKWAMBIA KUWA JOAQUINE NI MWANAMAMA MREMBO MNO ALIYEJALIWA. LABDA HILI NDILO LINALOLETA HISIA ZA KULIPA FADHILA ILA MIMI HILO SILIJUI.
Asante kwa ufanunuzi Mkuu binafsi sijui kabisa profile yake, zaidi ya kumwona alivyo mrembo wa kiafrica asilia...
 
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
2,505
1,225
Asante kwa ufanunuzi Mkuu binafsi sijui kabisa profile yake, zaidi ya kumwona alivyo mrembo wa kiafrica asilia...
Mie bado nina maswali mengi,Hivi hii tabia ya kurecicle viongozi itaisha lini??Jaji manento keshachoka kwanini wasipewe vijana wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo ..hawa wastaafu wanaenda kula pesa tu pale na siajwahi kusikia jambo lolote la maana ambalo wanafanya hawa watu wa haki za binadamu.Hawajawahi kukemea mambo ya msingi.

1.Mfano wa suala la kupigwa kwa Katibu wa CHADEMa huko Kiteto.walikaa kimya
2.kuhusu suala la kufungiwa kiana Maxenco Melo,hawakuliongelea mathalani linahusu utawal bora na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Mie nadhani kuna haja ya taaisis nyingi za serikali kupunguzwa ili zibaki chache zenye watendaji walio na tija ni sio watu wa kufanya semina kila siku.CHRAGG wamekuwa watu wa kufanya semina tu na hakuna cha maan awanachofanya.

alafu kuna jambo between the underlines..kuliongelea hapa inabidi uwe na akili ya mwendawazimu.
 
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
11,826
0
kwanza hiyo tume ya haki za binaadamu sijawahi kusikia imefanya kazi wapi. (kama ishawahi naomba kufahamishwa).
pili kuchaguliwa wajumbe wa tume na Rais kunaikosesha credibility tume hiyo kwa sababu katika nchi nyingi hasa za Afrika haki za binaadamu zinavunjwa na serikali.
tatu; hatusemi kuwa viongozi watu wazima wasipewe wadhifa lakini pia tungependa kuona sura mpya ambazo zingekuja na mawazo mapya. hivi recycle za kila siku ndo unakuta nchi ina muono mdogo.
 
jamani eeh katika sheria tume haiwezi kuchukua majukumu ya kutetea haki za binadamu za kila mmoja bila kuletewa malalamiko. kama watu wa chadema walipigwa wapeleke malalamiko halafu waone tume kama haitayafanyia kazi(ingawa tuwe wakweli huwa wanachukua muda mrefu sana kwa sababu ya kukosa wafanyakazi wa kutosha.)

mi nashauri watanzania tusiwe watu wa kulaumu tu!! tuwaelimishe watu wetu
 
C

CHAUMBEYA

Member
69
0
kwanza hiyo tume ya haki za binaadamu sijawahi kusikia imefanya kazi wapi. (kama ishawahi naomba kufahamishwa).
pili kuchaguliwa wajumbe wa tume na Rais kunaikosesha credibility tume hiyo kwa sababu katika nchi nyingi hasa za Afrika haki za binaadamu zinavunjwa na serikali.
tatu; hatusemi kuwa viongozi watu wazima wasipewe wadhifa lakini pia tungependa kuona sura mpya ambazo zingekuja na mawazo mapya. hivi recycle za kila siku ndo unakuta nchi ina muono mdogo.
tume imefanya kazi mbalimbali. imetembelea magereza ya tanzania na kuchunguza hali za wafungwa. wametoa mapendekezo mazuri. serikali imeyafanyia kazi na ndio maana misamaha ya rais siku hizi inawahusisha wafungwa wengi.

pia wamechunguza vituko vya mkuu wa wilaya ya tarime na ocd. walitoa hukumu kubwa wakashauri rais awafukuze kazi lakini rais akaogopa. sasa mnataka tume wafanye nini iwapo watendaji wa serikali hawataki kufuata masharti na madhumuni ya kujiunga na tume.
 
C

Chingwanji

Member
54
0
Niliwahi kupeleka malamiko yangu kwenye Tume hiyo chini ya Kisanga kama sikosei ikawa shida kubwa .Hawajali na wanasema niende mkoani nikabebe faili niwapelekee .Nikashangaa sana hadi leo hii .
 
M

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
5,194
0
Hii tume inafanya kazi bure au inaendeshwa kwa gharama za serikali? na kama inaendeshwa kwa pesa ya serikali, ni sahihi kusema kuwa hii ni extension ya central govt kiutendaji?
 
F

FDR Jr

JF-Expert Member
249
0
JOAQUINE DE MELLO AMETOKA KUMALIZIA TERM YAKE KAMA RAIS WA CHAMA CHA MAWAKILI TANGANYIKA(TANGANYIKA LAW SOCIETY)ITS INTERESTING TO KNOW KUWA WAO HUWA HAWAITAMBUI NCHI YA TANZANIA. JOAQUINE ALIKUWA NDIYE RAIS WA KWANZA MWANAMKE WA CHAMA CHA MAWAKILI TOKA KIANZISHWE MWAKA 1925. AMEKUWA PIA MWANACHAMA WA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE TANZANIA (TAWLA) KWA MIAKA MINGI.

KWA KWELI NAAMINI AMEKWENDA KULE BY MERITS NA ANAKUBALIKA.
KWA WANAOMFAHAMU WATAKWAMBIA KUWA JOAQUINE NI MWANAMAMA MREMBO MNO ALIYEJALIWA. LABDA HILI NDILO LINALOLETA HISIA ZA KULIPA FADHILA ILA MIMI HILO SILIJUI.
Dada Joakina ni mchapakazi na ni mtu anayeheshimu watu na pilika zao,ni dada asiyependa majungu na hili limejitokeza sana ktk firm yao ya mwanzo aliachana na wenzake kwa kuepuka hilo then akaamua kukomaa na TAWLA ambako alikuwa kama Tresurer wao then Executive Director akichukuwa nafasi ya mchapakazi mwengine Tuma Silaa ambaye aliitema chance hiyo baada ya kulemewa na majungu ya Uhaya chini ya chairperson Mama Rwebangira(Ambaye aliirithi chance hiyo toka kwa Mh.Balozi Majar), akiwa hapo TAWLA chini ya Mama Rwebangira naye aka face the same problem na huyo chair akaamua ku-resign na kuendelea na mambo yake,then Tanganyika Law Society na sasa ni Kamishina,ana uwezo, muaminifu ktk taaluma,mpenda haki ,amesoma vizuri,amesaidia mabint wengi ktk kujipatia elimu zaidi ktk wigo wa sheria,aliwahi olewa na akatengana na mumewe(hilo ni jambo la kawaida ktk ndoa hususani pale unapoona utofauti wenu unahatarisha uhai),ni mzazi na zaidi ktk orodha ya wale professional Lobbyist according Rich Kasesela definition ;Joakina is one of the smartest Lobbist.JK is right on picking her fot the Commission. Bravo
 
Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
12,659
0
Mwanamtama, kama huna uhakika uliza kwanza, badala ya ku-attack bila facts mkuu, nashukur kuwa umeliona hilo wazi.

Mkuu Babah,

Heshima mbele kwa kukubali ukweli angalau for once.

Ahsante Mkuu.
 
F

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
4,956
1,500
Lobbyist according Rich Kasesela definition ;Joakina is one of the smartest Lobbist.
Rich Kasesela definition ni ipi? From where I am standing, hii siyo sifa ya kujivunia!
 
Nyalotsi

Nyalotsi

JF-Expert Member
6,412
2,000
Kuna mjadala ulikuwepo toka siku nyingi wa de mello. Kumbe ndo huyu ambaye jamaa wa ruta anataka kurudisha majeshi.! Aafu kumbe max amewahi kufungiwa? Makabrasha ya zamani yana umuhimu wake,siyo tu tunafaidi jf kumbe kuna waliowekwa korokoroni kwa ajili yake!
 
Forum statistics

Threads
1,424,525

Messages
35,065,993

Members
538,010
Top Bottom