*Wananchi wamuona mkombozi,shujaa wao!
*Wabunge wa DRC kufunga safari hadi ikulu ya Magogoni kumshukuru!
*Kumuomba kichapo cha Nduli Amini kirejewe kwa Kagame!
*M23 waishi kama Ngedere kwa matunda porini!
*Ni baada ya kichapo cha masaa2 tu toka JWTZ!
*Wakimbia waacha silaha,vyakula!
*Saa 48 walizopewa kuweka silaha chini zazidi kuyoyoma!
Ni post kama hizi zinaishushia hadhi JF halafu wapuuzi wanaoleta posti kama hizi ndio wa kwanza kueneza upuuzi wao kwingineko kwamba JF kumejaa uzushi na umbea. Zamani kidogo mtu akileta mada kama hii wadau kabla ya kuchangia walijitahidi angalau kupata ukweli wa mambo kabla ya kuanza kuchombeza huku wakichakachua kama ilivyo kawaida ya wapuuzi wenzao popote pale walipo.
Ni vizuri kwanza kujiuliza; ni kitu gani kinatokea Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo au
République Démocratique du Congo na kwa nini wapiganaji wetu wako huko. Je mleta mada anaijua MONUSCO, The United Nations Organization Stabilization Mission in the Democratic Republic of the Congo or
MONUSCO? Utafiti kidogo tu ungemsaidia mleta mada kuelewa kwa nin wapiganaji wetu wako Congo na wanatimiza wajibu kwa maelekezo ya nani.
Sitapoteza muda wangu kujibishana na mleta mada (nakataa katakata kukimbizana na kichaa!) ila nitamwambia tu kwamba Tanzania ni mojawapo kati ya nchi nyingi tu karibia sitini (60) zilizoitikia wito wa UN zenye askari wake nchini Congo kulinda amani. Mpaka mwishoni mwa mwezi wa Juni
MONUSCO ilikuwa na askari zaidi ya
20,438 na nchi zinazoongoza kwa kuwa na askari wengi ni pamoja na;
- India..............3,731
- Pakistan.........3,714
- Bangladeshi....2,540
- .
- .
- .
- Tanzania.........1,247
Kwa ufupi ni kwamba idadi ya askari wa Tanzania walioko Congo ni kama asilimia 5% tu ya wapiganaji kutoka nchi mbali mbali. Sasa swali langu kwa mleta mada ni hili; je huo ukombozi kama upo utakuwa umeletwa na Kikwete au Umoja wa Mataifa. Ushauri wangu kwa wote walichangia hii mada; kuna mbinu ya kuichafua JF kwa mada za kipuuzi na kijinga zimeshika kasi, tuchukue tahadhari tunapozichangia.
Toka mwaka 2010 kuna virusi vinaishambulia JF kwa lengo la kulidhoofisha nguvu na siku zinavyosogea ndio virusi vinaongezeka...tusije tukashangaa kwa hii ari na kasi mpya kuelekea 2015. Kuwatambua ni rahisi sana wanapovamia mada, hawatoi nafasi hata ya kujibiwa...unaweza kuta kurasa moja imejaa majibu kutoka kwa kirusi hicho hicho kimoja, vina mission maalum lakini dawa za kinga pia zipo, kazi kwenu.