Namuunga mkono J.M. Kikwete (Tanzania) kwa kuendeleza Amani ukanda huu wa maziwa makuu. Hii ndiyo sifa kuu ya nchi yetu iliyojengwa/pikwa na Mwl. J.K. Nyerere. Lakini kwa mfumo tulionao napata utata kidogo. Itakumbukwa kuwa Mwl. J.K. Nyerere (Tanzania) alizisaidia sana nchi nyingi za Africa (Namibia, Msumbiji, Angola, South Africa, n.k) kupata Uhuru kwa kutumia rasilimali zetu wenyewe (fedha, silaha, muda, ardhi n.k), bila sisi Tanzania kufaidi chochote kutoka kwa mataifa hayo zaidi ya Heshima tu iliyojengeka miongoni mwetu. Kwa kipindi hicho sipaswi kujiuliza wala kumlaumu Mwl Nyerere eti kwanini alitumia rasilimali nyingi tu bila ya kupata faida zaidi ya kujijengea heshima. Hii ni kwasababu ya msimamo itikadi ya Mwl. Nyerere (Tanzania) kuwa Africa ni moja na binadamu wote ni sawa, hakuona tofauti ya Mtanzania, Mkongo wala Msouth Africa kiuchumi, kisiasa, kijamii, na kiutamaduni kwakuwa wote ni ndugu. Lakini kwa kipindi hiki cha mfumo wa UBEPARI (Capitalism), sio rahisi kutumia mawazo ya Mwl Nyerere na katika kusisaidia DRC na kwingineko kuwa huru kijeshi, kiuchumi na kijamii. Sera za ubepari zinatambua wazi kabisa kwamba hata siku moja hakuna rafiki wa kudumu bali kuna maslahi ya kudumu. Kwamba nje ya mipaka hakuna Dada wala Kaka, wala Mjomba, kuna maslahi ya nchi. Sasa swali ninalojiuliza maslahi yetu DRC, Comoro n.k ni yepi? Nini sera yetu katika ukanda huu wa maziwa makuu? Najua sera yetu ya mambo ya nje ni Economic Diplomacy, Je inatekelezwa au inatekelezeka huko DRC, Comoro?. Kagame na Kaguta sera zao zilikuwa wazi kabisa DRC kwamba waifanye isitawalike ili wao (Kagame & Kaguta) wafaidi Madini na rasilimali nyinginezo (ambapo kimsingi wapo sawa kulingana na sera na mfumo wa ubepari), Je Tanzania kuifanya DRC, Comoro etc zitawalike nini tulifaidi/tunafaidi kwa mtizamo wa sera na mifumo ya kibepari Vs economic diplomacy ya kwetu?