JK apanda chati DRC!!!

JK apanda chati DRC!!!

*Wabunge wajiandaa kwenda Dar kumshukuru, kumpongeza
*Wananchi wataka adhabu aliyopewa Iddi Amin irudiwe

KATIKA kile kinachoonesha kwamba raia wengi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wamechoshwa na vita visivyokwisha, mikakati inayofanywa na Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete kutafuta amani nchini humu imeipa heshima kubwa Tanzania.

Mbali ya hatua hizo za kutafuta amani ya DRC zinazoendelea kuchukuliwa na Tanzania, pia uwapo wa wanajeshi yake mashariki mwa Congo umewafanya wananchi wa huku kutembea ‘vifua mbele' wakiamini mwisho wa vita umekaribia.

Vyombo mbalimbali vya habari yakiwamo magazeti, redio, televisheni na mitandao ya kijamii vimekuwa vikimsifu na kumshukuru Kikwete kutokana na msimamo wake kuhusu mchakato wa kupata amani ya kudumu nchini humu.

Chagizo jingine la furaha kwa Wacongomani wengi ni ziara ya Rais wa Marekani Barack Obama iliyofanywa mwanzoni mwa Julai huko Tanzania na kuacha gumzo kubwa DRC hasa kutokana na matamshi ya kiongozi huyo kuweka bayana kuwa anaunga mkono jitihada za kuleta amani zinazofanywa na Tanzania pamoja na Jumuiya ya Kimataifa.

Katika mahojiano maalumu na RAI, Mbunge maarufu nchini DRC, Emery Okundji, wa chama cha FONUS akiwakilisha Jimbo la Oriental Kasai, alikuwa akitoka Waziri Mkuu wa kwanza wa Congo, Patrice Lumumba, alisema uamuzi wa Rais Kikwete ni njozi ambayo baadhi ya viongozi wa Afrika hawana.

"Maadui wa Congo walidhani Rais Kikwete anazungumza tu na hatatekeleza aliyoahidi na kukusudia kuyafanya kwa ajili ya kuwasaidia ndugu zake.

"Ukitafakari maamuzi na ushauri wake kwetu na kwa nchi jirani ya Rwanda, utaona kabisa Kikwete alikuwa amepata njozi, kwa sababu tunaamini sasa tunaelekea kwenye amani. Wananchi wa Congo wamekufa na kuteseka sana, sasa wakati wa amani na maendeleo umewadia.

"Ametoa ushauri mzuri kuwa kila nchi husika kwenye mgogoro wa Congo ikae na kuzungumza na waasi. Sisi tumefanya hivyo, lakini wenzetu wa Rwanda hawataki, halafu wanatulazimisha tuzungumze na waasi wa M23.

"Wao wanawatumia waasi wa Forces Democratic for Liberation of Rwanda (FDLR) kama sababu ya kuvamia ardhi ya Congo, lakini hawataki kukaa na kuzungumza nao, hili halikubaliki.

"FDLR hawataki kurudi Rwanda kwa sababu hawajahakikishiwa usalama wao, kwa hiyo kama Rwanda wangesikiliza na kufanyia kazi ushauri wa Kikwete, tunaamini hali ya usalama ingekuwa tofauti na ilivyo sasa.

"Yote yanayoitwa makundi ya waasi yaliyopita na sasa hawa M23, ni watu wanaotumiwa kuivuruga Congo, na kibaya zaidi miongoni mwao wapo Wacongo ambao hawana uzalendo kabisa. Lakini wakati wao sasa umefika.

"Nguvu ya kijeshi ya Rwanda kule Mashariki imepata pigo kubwa sana baada ya Tanzania kupeleka majeshi yake na tunawaomba kama itatokea wakashambuliwa, basi watoe kipigo kama walichompa Iddi Amin wa Uganda.

"Wasiwapige M23 ndani ya Congo pekee, bali wawafuate hadi kule wanakopewa jeuri, na Wacongo wote tutakuwa nyuma ya wanajeshi wa Tanzania," alisema.

Wabunge kuja Dar kushukuru

Katika hatua nyingine, Mbunge Okundji alitoa hoja binafsi katika kikao cha Bunge la DRC kilichomalizika Juni mwaka huu, ambapo alipendekeza Bunge liteue timu maalumu ya wabunge kutembelea Tanzania kumshukuru Rais Kikwete.

Alisema hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wote, ambapo taratibu zinafanyika ili kufanikisha azma hiyo.

"Kazi aliyofanya Kikwete ni nzuri sana kutokana na umuhimu wake kwa nchi yetu, na baada ya kujadiliana na wabunge wenzangu, basi nikatoa hoja binafsi nikitaka Bunge litume ujumbe kwenda Dar es Salaam kumshukuru na kumpongeza Rais Kikwete.

"Kwa umoja waliikubali, kwa hiyo taratibu zikikamilika tutafika Dar es Salaam," alisema.

Tanzania ni moja kati ya nchi tatu zinazounda Brigedi Maalumu ya Umoja wa Mataifa yenye ruhusa ya kujibu mashambulizi (kupigana), ikiwa ni tofauti na walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa sehemu nyingine duniani.

Nchi nyingine ndani ya Brigedi hiyo inayoongozwa na Mtanzania Brigedia Jenerali James Mwakibolwa ni Afrika Kusini na Malawi, ingawa hadi wiki iliyopita Malawi ilikuwa imepeleka wanajeshi wa ‘utangulizi' kabla bataliani nzima haijakwenda.

Soma mahojiano kamili na Mbunge Okundji toleo lijalo

M23, Kagame lawamani

Wiki iliyopita ilijaa matukio mengi ya kimataifa kuhusu amani mashariki mwa Congo na eneo la Maziwa Makuu; la kwanza likiwa ni ripoti ya taasisi ya kimataifa ya Human Rights Watch iliyoituhumu serikali ya Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23.

Ripoti hiyo iliungwa mkono na serikali ya Marekani kupitia kwa msemaji wake, Jen Piski, aliyetoa onyo kwa Rais Paul Kagame akimtaka kuacha mara moja kuwasaidia waasi hao wanaotuhumiwa kufanya mauaji ya raia, ubakaji na kuwatumikisha watoto wadogo kama askari.

Mbali na M23, Rwanda pia inadaiwa kufadhiri kundi la waasi la CNDP lililokuwa chini ya uongozi wa Jenerali Bosco Ntaganda aliyejisalimisha ICC mapema mwaka huu.

Sehemu kubwa ya wapiganaji wa kundi hilo kwa sasa wameungana na waasi wa M23 kwa muktadha wa kujiimarisha kiulinzi katika maeneo yenye utajiri mkubwa wa madini Mashariki mwa Congo.

Rwanda haijafanya juhudi zozote za kuishawishi jumuiya ya kimataifa kwamba ripoti hizo ni za kughushi na kwamba haina mkono kwenye machafuku ya miaka mingi ya mashariki mwa Congo.

Balozi Tanzania UN agoma kuiomba radhi Rwanda, wa Rwanda anywea

Wakati wa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu amani eneo la Maziwa Makuu kilichofanyika wiki iliyopita nchini Marekani chini ya uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, John Kerry, Balozi wa Tanzania UN, Tuvako Manongi alisisitiza ushauri uliotolea na Rais Kikwete Mei mwaka huu kwamba serikali za nchi husika kwenye mgogoro wa Congo zinapaswa kuzungumza na waasi wenye silaha.

Alilitaka Baraza la Usalama la UN kumunga mkono Kikwete kwamba suluhu ya mgogoro wa Congo kamwe si vita, bali mazungumzo ya amani.

Kauli hiyo iliungwa mkono na wawakilishi kutoka Ufaransa, Ubelgiji na SADC katika mkutano huo muhimu.

Mitandao mbalimbali ya habari ilimripoti Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, mama Louise Mushikiwabo aliyeongoza ujumbe wa nchi hiyo kwenye mkutano huo akiwa mnyonge huku akitoa shukrani kwa waliohudhuria, hali iliyotajwa kuwa ni tofauti na mikutano mingine aliyowahi kuiwakilisha Rwanda UN.

"Hakuonekana mwenye furaha au amani. Mara nyingi mama huyu huwa anajiamini sana kwenye mikutano kama hii tofauti na leo. Si kawaida sana kwake kumwaga sifa kama alivyomfanyia leo Mwakilishi Maalumu wa UN eneo la Maziwa Makuu, Mary Robinson.

"Hii ni dalili kwamba sasa serikali ya Rwanda imeona wazi kuwa ipo hatarini kutengwa na jumuiya ya kimataifa kutokana na kushiriki kwake kwenye migogoro ya mashariki mwa Congo.

"Lakini tangu mama Mushikiwabo alipopoteza nafasi yake kama Mkurugenzi wa Wanawake UN (nafasi iliyochukuliwa na mama Phumzile Mlambo-Ngcuka wa Afrika Kusini) Julai 10 mwaka huu, amekosa furaha kabisa. Huenda pia amechoka kumtetea rais wake (Kagame) kwenye vikao ambavyo wahudhuriaji wote wanamtuhumu," unaandika mtandao wa habari wa kimataifa wa afroamerica.net.

Hotuba ya JK, Jenerali Mwakibolwa zatia chumvi kidonda

Akizungumza kwenye sherehe za Siku ya Mashujaa wa Vita vya Kagera kwenye Kambi ya Jeshi ya Kaboya wiki iliyopita, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Kikwete alisema jeshi la Tanzania lipo imara kulinda mipaka ya nchi na raia wake.

Kikwete aliongeza kwamba yeyote atakayethubutu kumega ardhi ya Tanzania atashughulikiwa kama alivyoshughulikiwa Nduli Idd Amini Dada alipotaka kuchukua eneo la mkoa wa Ziwa Magharibi (sasa Kagera) enzi hizo.

Kauli ya Kikwete ilitafsiriwa na wadadisi wa mambo kuwa aliielekeza kwa Kagame wa Rwanda ambaye kwa miezi takriban miwili sasa hayupo kwenye uhusiano mzuri na Tanzania.

Wiki hiyo hiyo, Kiongozi wa Brigedi Maalumu ya UN huko Congo, Jenerali Mwakibolwa alinukuliwa na BBC akiwaambia waandishi wa habari mjini Goma, DRC kwamba kikosi chake kinakaribia kukamilika.

"Bado vitu vidogo vidogo tu na bataliani ya Malawi nayo haijawasili yote. Lakini tuliopo hapa tuko imara na tupo tayari wakati wowote tutakapoamriwa kuanza kazi ya kuwapokonya silaha waasi.

"Tunawahakikishia raia wa maeneo haya kwamba wasiwe na wasiwasi, tupo na tutawalinda. Hizi propaganda kwamba kuna askari wetu wanapigana upande wa waasi si za kweli. Tutakapoanza kazi, tutawataarifa," alisema Jenerali huyo kauli iliyotafsiriwa na mchambuzi wa BBC kwamba kikosi hicho kipo imara na huenda kimekwishaanza kazi.

DRC ina watu millioni 70, ina madini, ina misitu... lakini inasumbuliwa na Rwanda yenye watu milioni 12? Hata ukijumlisha na milioni 34 wa Uganda, kweli ndio wa kuinyanyasa ncho kubwa namna hiyo?!!!
Kweli waafrica tumelaaniwa... si bure...

Unashangaa ya DRC na Rwanda, katafute ya Israel na majirani zake ndio balaa.....
 
naona kama vile kule ndio anafit zaidi sasa hebu ona hapa kaanzisha thread imejaa title tupui haina taarifa nyingine zozote.......

mkuu, si tumemsaidia kwa kuliscani hilo gazeti lote ili ulisome? yeye ameona asiongeze chochote bali kutoa dondoo ili zitusaidie sisi
 
tunakushukuru mkuu maana kuna watu walikuwa wanasema kuwa huo ni udaku wa mleta mada
 
Mbali ya hatua hizo za kutafuta amani ya DRC zinazoendelea kuchukuliwa na Tanzania, pia uwapo wa wanajeshi yake mashariki mwa Congo umewafanya wananchi wa huku kutembea ‘vifua mbele’ wakiamini mwisho wa vita umekaribia.

Vyombo mbalimbali vya habari yakiwamo magazeti, redio, televisheni na mitandao ya kijamii vimekuwa vikimsifu na kumshukuru Kikwete kutokana na msimamo wake kuhusu mchakato wa kupata amani ya kudumu nchini humu.

Chagizo jingine la furaha kwa Wacongomani wengi ni ziara ya Rais wa Marekani Barack Obama iliyofanywa mwanzoni mwa Julai huko Tanzania na kuacha gumzo kubwa DRC hasa kutokana na matamshi ya kiongozi huyo kuweka bayana kuwa anaunga mkono jitihada za kuleta amani zinazofanywa na Tanzania pamoja na Jumuiya ya Kimataifa.

Katika mahojiano maalumu na RAI, Mbunge maarufu nchini DRC, Emery Okundji, wa chama cha FONUS akiwakilisha Jimbo la Oriental Kasai, alikuwa akitoka Waziri Mkuu wa kwanza wa Congo, Patrice Lumumba, alisema uamuzi wa Rais Kikwete ni njozi ambayo baadhi ya viongozi wa Afrika hawana.

“Maadui wa Congo walidhani Rais Kikwete anazungumza tu na hatatekeleza aliyoahidi na kukusudia kuyafanya kwa ajili ya kuwasaidia ndugu zake.

“Ukitafakari maamuzi na ushauri wake kwetu na kwa nchi jirani ya Rwanda, utaona kabisa Kikwete alikuwa amepata njozi, kwa sababu tunaamini sasa tunaelekea kwenye amani. Wananchi wa Congo wamekufa na kuteseka sana, sasa wakati wa amani na maendeleo umewadia.

“Ametoa ushauri mzuri kuwa kila nchi husika kwenye mgogoro wa Congo ikae na kuzungumza na waasi. Sisi tumefanya hivyo, lakini wenzetu wa Rwanda hawataki, halafu wanatulazimisha tuzungumze na waasi wa M23.

“Wao wanawatumia waasi wa Forces Democratic for Liberation of Rwanda (FDLR) kama sababu ya kuvamia ardhi ya Congo, lakini hawataki kukaa na kuzungumza nao, hili halikubaliki.

“FDLR hawataki kurudi Rwanda kwa sababu hawajahakikishiwa usalama wao, kwa hiyo kama Rwanda wangesikiliza na kufanyia kazi ushauri wa Kikwete, tunaamini hali ya usalama ingekuwa tofauti na ilivyo sasa.

“Yote yanayoitwa makundi ya waasi yaliyopita na sasa hawa M23, ni watu wanaotumiwa kuivuruga Congo, na kibaya zaidi miongoni mwao wapo Wacongo ambao hawana uzalendo kabisa. Lakini wakati wao sasa umefika.

“Nguvu ya kijeshi ya Rwanda kule Mashariki imepata pigo kubwa sana baada ya Tanzania kupeleka majeshi yake na tunawaomba kama itatokea wakashambuliwa, basi watoe kipigo kama walichompa Iddi Amin wa Uganda.

“Wasiwapige M23 ndani ya Congo pekee, bali wawafuate hadi kule wanakopewa jeuri, na Wacongo wote tutakuwa nyuma ya wanajeshi wa Tanzania,” alisema.

Wabunge kuja Dar kushukuru

Katika hatua nyingine, Mbunge Okundji alitoa hoja binafsi katika kikao cha Bunge la DRC kilichomalizika Juni mwaka huu, ambapo alipendekeza Bunge liteue timu maalumu ya wabunge kutembelea Tanzania kumshukuru Rais Kikwete.

Alisema hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wote, ambapo taratibu zinafanyika ili kufanikisha azma hiyo.

“Kazi aliyofanya Kikwete ni nzuri sana kutokana na umuhimu wake kwa nchi yetu, na baada ya kujadiliana na wabunge wenzangu, basi nikatoa hoja binafsi nikitaka Bunge litume ujumbe kwenda Dar es Salaam kumshukuru na kumpongeza Rais Kikwete.

“Kwa umoja waliikubali, kwa hiyo taratibu zikikamilika tutafika Dar es Salaam,” alisema.

Tanzania ni moja kati ya nchi tatu zinazounda Brigedi Maalumu ya Umoja wa Mataifa yenye ruhusa ya kujibu mashambulizi (kupigana), ikiwa ni tofauti na walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa sehemu nyingine duniani.

Nchi nyingine ndani ya Brigedi hiyo inayoongozwa na Mtanzania Brigedia Jenerali James Mwakibolwa ni Afrika Kusini na Malawi, ingawa hadi wiki iliyopita Malawi ilikuwa imepeleka wanajeshi wa ‘utangulizi’ kabla bataliani nzima haijakwenda.

Soma mahojiano kamili na Mbunge Okundji toleo lijalo

M23, Kagame lawamani

Wiki iliyopita ilijaa matukio mengi ya kimataifa kuhusu amani mashariki mwa Congo na eneo la Maziwa Makuu; la kwanza likiwa ni ripoti ya taasisi ya kimataifa ya Human Rights Watch iliyoituhumu serikali ya Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23.

Ripoti hiyo iliungwa mkono na serikali ya Marekani kupitia kwa msemaji wake, Jen Piski, aliyetoa onyo kwa Rais Paul Kagame akimtaka kuacha mara moja kuwasaidia waasi hao wanaotuhumiwa kufanya mauaji ya raia, ubakaji na kuwatumikisha watoto wadogo kama askari.

Mbali na M23, Rwanda pia inadaiwa kufadhiri kundi la waasi la CNDP lililokuwa chini ya uongozi wa Jenerali Bosco Ntaganda aliyejisalimisha ICC mapema mwaka huu.

Sehemu kubwa ya wapiganaji wa kundi hilo kwa sasa wameungana na waasi wa M23 kwa muktadha wa kujiimarisha kiulinzi katika maeneo yenye utajiri mkubwa wa madini Mashariki mwa Congo.

Rwanda haijafanya juhudi zozote za kuishawishi jumuiya ya kimataifa kwamba ripoti hizo ni za kughushi na kwamba haina mkono kwenye machafuku ya miaka mingi ya mashariki mwa Congo.

Balozi Tanzania UN agoma kuiomba radhi Rwanda, wa Rwanda anywea

Wakati wa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu amani eneo la Maziwa Makuu kilichofanyika wiki iliyopita nchini Marekani chini ya uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, John Kerry, Balozi wa Tanzania UN, Tuvako Manongi alisisitiza ushauri uliotolea na Rais Kikwete Mei mwaka huu kwamba serikali za nchi husika kwenye mgogoro wa Congo zinapaswa kuzungumza na waasi wenye silaha.

Alilitaka Baraza la Usalama la UN kumunga mkono Kikwete kwamba suluhu ya mgogoro wa Congo kamwe si vita, bali mazungumzo ya amani.

Kauli hiyo iliungwa mkono na wawakilishi kutoka Ufaransa, Ubelgiji na SADC katika mkutano huo muhimu.

Mitandao mbalimbali ya habari ilimripoti Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, mama Louise Mushikiwabo aliyeongoza ujumbe wa nchi hiyo kwenye mkutano huo akiwa mnyonge huku akitoa shukrani kwa waliohudhuria, hali iliyotajwa kuwa ni tofauti na mikutano mingine aliyowahi kuiwakilisha Rwanda UN.

“Hakuonekana mwenye furaha au amani. Mara nyingi mama huyu huwa anajiamini sana kwenye mikutano kama hii tofauti na leo. Si kawaida sana kwake kumwaga sifa kama alivyomfanyia leo Mwakilishi Maalumu wa UN eneo la Maziwa Makuu, Mary Robinson.

“Hii ni dalili kwamba sasa serikali ya Rwanda imeona wazi kuwa ipo hatarini kutengwa na jumuiya ya kimataifa kutokana na kushiriki kwake kwenye migogoro ya mashariki mwa Congo.

“Lakini tangu mama Mushikiwabo alipopoteza nafasi yake kama Mkurugenzi wa Wanawake UN (nafasi iliyochukuliwa na mama Phumzile Mlambo-Ngcuka wa Afrika Kusini) Julai 10 mwaka huu, amekosa furaha kabisa. Huenda pia amechoka kumtetea rais wake (Kagame) kwenye vikao ambavyo wahudhuriaji wote wanamtuhumu,” unaandika mtandao wa habari wa kimataifa wa afroamerica.net.

Hotuba ya JK, Jenerali Mwakibolwa zatia chumvi kidonda

Akizungumza kwenye sherehe za Siku ya Mashujaa wa Vita vya Kagera kwenye Kambi ya Jeshi ya Kaboya wiki iliyopita, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Kikwete alisema jeshi la Tanzania lipo imara kulinda mipaka ya nchi na raia wake.

Kikwete aliongeza kwamba yeyote atakayethubutu kumega ardhi ya Tanzania atashughulikiwa kama alivyoshughulikiwa Nduli Idd Amini Dada alipotaka kuchukua eneo la mkoa wa Ziwa Magharibi (sasa Kagera) enzi hizo.

Kauli ya Kikwete ilitafsiriwa na wadadisi wa mambo kuwa aliielekeza kwa Kagame wa Rwanda ambaye kwa miezi takriban miwili sasa hayupo kwenye uhusiano mzuri na Tanzania.

Wiki hiyo hiyo, Kiongozi wa Brigedi Maalumu ya UN huko Congo, Jenerali Mwakibolwa alinukuliwa na BBC akiwaambia waandishi wa habari mjini Goma, DRC kwamba kikosi chake kinakaribia kukamilika.

“Bado vitu vidogo vidogo tu na bataliani ya Malawi nayo haijawasili yote. Lakini tuliopo hapa tuko imara na tupo tayari wakati wowote tutakapoamriwa kuanza kazi ya kuwapokonya silaha waasi.

“Tunawahakikishia raia wa maeneo haya kwamba wasiwe na wasiwasi, tupo na tutawalinda. Hizi propaganda kwamba kuna askari wetu wanapigana upande wa waasi si za kweli. Tutakapoanza kazi, tutawataarifa,” alisema Jenerali huyo kauli iliyotafsiriwa na mchambuzi wa BBC kwamba kikosi hicho kipo imara na huenda kimekwishaanza kazi.

tunakushukuru mkuu maana kuna watu walikuwa wanasema kuwa huo ni udaku wa mleta mada
 
DSC_0054_12534.JPG
Gazeti la Leo Alhamis 08/01/2013la Rai Nguvu ya Hoja.
thanks. I stand corrected.

sorry Boflo, kumbe ulikuwa serious (this time). thumbs up :smile-big:
 
Last edited by a moderator:
Magamba kwa kuanzisha majiviwanda ya uongo tu hamjambo mbona JWTZ wapo busy kupiga na kubaka watu huko Mtwara? au M23 ndo wapo mtwara siku hizi?

Ndugu, hapa tunaongelea mambo ya nchi dhidi ya nchi za nje. Mambo ya magamba yanakujaje ndugu? Inapokuja kutetea taifa dhidi ya udhalim wa kutoka nje twahitaji kusimama pamoja. Mambo ya ndani si mahali pake kwenye hii thread ndugu. Samahan km ntakua nimekosea. Ni mtazamo wangu. Nampenda Rais wangu Mh Jakaya Kikwete, naipenda nchi yangu Tanzania
 
Mkuu Ritz hajui hifadhi ya Virunga kuna mafuta,hajui ziwa Tanganyika lina mafuta na gesi.

Msome vizuri Mkuu Ngongo, hakuna mahala ametaja dhahabu.

Kaongelea ardhi sijui kama unajua ukubwa wa ardhi nzuri ya kilimo/misitu ya mbao, ambayo haijawahi kuguswa toka dunia iumbwe.
 
Last edited by a moderator:
Hata mimi napenda alichofanya JK lakini asisahau kuchukuwa madini na mbao huko kulipia gharama tunazoingia wakati wa kutekeleza jukumu letu la kuwafanya Wakongo nao waishi na kuifurahia nchi yao kama binadamu wengine.
Rwanda walianza hivyo kujidai wanalipia gharama za kumng'oa mobutu sasa imegeuka ufisadi mkubwa wa viongozi wa rwanda kuipora congo maliasili zake kwa manufaa ya watawala wa rwanda. Hatutegemei kua hivyo kwa tanzania.
 
*wananchi wamuona mkombozi,shujaa wao!

*wabunge wa drc kufunga safari hadi ikulu ya magogoni kumshukuru!

*kumuomba kichapo cha nduli amini kirejewe kwa kagame!

*m23 waishi kama ngedere kwa matunda porini!

*ni baada ya kichapo cha masaa2 tu toka jwtz!

*wakimbia waacha silaha,vyakula!

*saa 48 walizopewa kuweka silaha chini zazidi kuyoyoma!
; no research no right to speak. Tell usa the sources
 
bila shaka wewe upo ulimwengu wa shetani. hivi ni kweli hujui kuwa majeshi yetu yapo DRC? au unajitia ukipofu tu? kama uliagizwa umpinge jk si kwa kila kitu. huo ni utumwa wa mawazo

Huyu jamaa sijui ni mtutsi anayewaunga mkono m23! Anyway watu waliokosa uzalendo ni kuwapa vipande vyao na kuwadharau tu! Mh Kikwete ni Rais wetu na tutakua sambamba na yeye kumpa support..
 
Ndugu zangu wa Tanzania, na haswa wale wanachama/mashabiki wa chadema. Katika mambo ambayo Julius Nyerere aliwahi kusema na ninakubaliana nayo ni kwamba. "Tanzania inapokuwa imara na tulivu, majirani zetu wanakuwa na matumaini." Hii kauli alipoitoa kwa wakati ule sikuwa nimeielewa kutokana na umri wangu na uwezo wangu wa wakati ule katika upembuzi wa siasa za kimataifa na hata za kitaifa. Tukumbuke kwamba, majirani wakiwa wana matuamini na imani na Tanzania, basi hivyo ndiyo hadhi ya nchi yetu kimataifa inavyopanda juu. Kama Congo wanadhania JK anasimama mahali sahihi, basi hizi sifa ni sifa za Tanzania na wala siyo za JK. JK baada ya miaka miwili ijayo hatokuwa rais wetu. Lakini Tanzania itaendelea kuwepo. Kama Tanzania ndiyo nchi yenye nguvu kiuchumi na kijeshi katika ukanda wa maziwa makuu; basi Tanzania inakuwa na majukumu ya kusimamia haki na usawa hata nje ya mipaka yetu; ili mradi tuu tusivuke mipaka ya kisheria na kuingilia serikali/tawala halali za majirani zetu.

Majirani zetu kama Congo/Burundi/Zambia na wengineo wanapokuwa na imani na Tanzania; wanakuwa wepesi kufanya biashara na Tanzania na pia wanakuwa wepesi zaidi kutumia miundo mbinu yetu kama bandari. Pia watanunua kazi zetu za kisanaa na hii itawezesha kiswahili kufika mbali zaidi na kuchangia ukuaji wa uchumi wetu. Kwa hivyo basi; CHADEMA hawana sababu ya kuona kama vile wanapigwa bao kwa sababu umaarufu wa JK umepanda chati Congo. Wa-Congo hawaijui Chadema na wala hawaijui CCM. Wao wanaijua Tanzania. Upo muda katika Siasa ambapo mwananchi unaweka maslahi ya nchi mbele na ya chama chako nyuma.
Kama hii habari ya M23 kurudishwa nyuma na JWTZ ni kweli; basi W. Slaa kama angekuwa mjanja kisiasa angekuwa wa kwanza kulipongeza jeshi letu. Siyo lazima ampongeze JK. Alipongeze jeshi letu inatosha.
 
mkuu hakuna mtu ambaye anaweza kumhurumia kagame amefanya umafia kwa watu wengi ameua watu wengi sana ni mshenzi wa washenzi.

Surely Simiyu yetu, huyu jamaa na baadhi ya watutsi wenzie wamejaa damu za watu mikononi mwao. Tuwasake huko Ngara, Karagwe, Kigoma na popote walipo warudishwe kwao na pia wasipewe opportunity ya kuwa hata wenyeviti wa vitongoji hata kama wamezaliwa hapa TZ. Pia Chama kiwe makini na Wabunge wa kitutsi kama akina Ntukamazina na Serukamba
 
Dhambi kubwa sana inayowakabili wacongoman ni uoga!

I can't imagine nchi kubwa na yenye nguvu kazi kubwa ya kutosha kabisa kama DCR kunyanyaswa (tena kijinsia) na ka nchi kama rwanda!

Enzi za kabila chini ya mwamvuli wa SADC tuliwasaidia ku recruit wanajeshi vijana wa kicongo wa kutosha kabisa kuilinda nchi yao, cha ajabu kwa uoga wao wakawa wa kwanza kuikimbia vita au kujiunga na upande wa maadui, huku nchi yao ikitegemea utetezi wa majeshi ya SADC kutoka Angola, Zimbabwe, Botswana na sasa Tanzania kwa mwamvuli wa UN
 
Back
Top Bottom