JK: Anachosema Nape ndio msimamo wa chama

Thanks Mkuu kwa kutuletea hii post.
It will go a long way kuwanyamazisha wale doubting Thomases juu ya muelekeo wa chama.
Kimsingi itawafanya wale wapinzani-waandamanaji wakose mada ya kuongea hadharani-maana hawana sera wala mikakati ya kuwaendeleaza waTz, zaidi ya kukodolea
macho kiti cha Urais.
Muelekeo wa chama? Kwa hiyo ccm wana mambo ya chama kwanza nchi baadaye? Kuna sisi ambao hatuna vyama lakini tunataka maisha bora, utawala wa sheria vitu ambavyo ccm imeshindwa kuvifanya kwa miaka yote iliyokaa madarakani.

Leo mwenyekiti wa ccm kakiri hadharani chama kina mafisadi badala ya kuwachukulia hatua, wanabaki wanawachekea ooh siku 90 ooh tunarudi kule kwenye misingi ya ccm, blah blah blah! F this bs kwa kweli.
 
Aliongea jana kwenye Tamasha sio Gazeti la habari leo!

Kwanini vyombo vyote vya habari haviku report jinsi ulivyo report hapo juu kuwa anachofanya NAPE ndo msimamo wa chama, bali vimeeleza jinsi JK alivyokuwa anamkingia kifua Nape asilaumiwe, Msimamo wa chama ni ule unaopitishwa na vikao halali vya chama mzee na si vinginevyo
 
Dah,hii style ya jk kiboko.yeye haongei wanaongea wengine mnakumbuka mkutaö wa vijana pale pwani ?ilikua intro watu wakapuuzia na ikatokea.hivi sa watu wanamponda Nape lakini ndichosa kitatokea na wengi wataachwa midomo wazi.WAIT AND SEE
 
Nsimba,
Na "kichwa" nacho kina siku 90 kujivua Gamba. Ajenda ya Ufisadi itaisha kama wote kwenye List of Shame watajivua Gamba, watafikishwa mhakamani, na Fedha na Rasilimali zetu zitarejeshwa. Vinginevyo ngoma ndiyo inaanza. Usijidanganye. Kwa taarifa yako, hakuna anayesukumwa na uchu wa madaraka. 2007 hakuna aliyefikiria "uongozi" bali tuisukumwa na uchungu kwa Mama yetu Tanzania kufilisiwa na viongozi wasio na uchungu. Hatudanganyiki tena 'ngo' na propaganda.


Watakosaje cha kusema,sana sana watawashukuru kwa kujiona ccm ni mafisadi, dhana waliyokuwa wakiikataa muda mwingi. Maana hao mafisadi walisemwa zamani 2007 na wala siyo leo 2011; na ccm walikataa kata kata. Sasa mkuu hapa mshindi atakuwa nani?? CDM au CCM?? Tegemea kwa kuwa mtaondoa mafisadi wachache, CDM wataendelea kudai na wale waliojificha nao wajisafishe-hapo sasa patakuwa patamu!! Kusema kuwa waandamanaji watakosa cha kusema -ni kujidanganya, kwa kuwa hoja hii ccm wanadandia na hivyo wataendelea kudandia kila kitakachoibushwa baada ya hapo. UTAKUMBUKA UTABIRI HUU WANGU!
 
Nsimba,
Na "kichwa" nacho kina siku 90 kujivua Gamba. Ajenda ya Ufisadi itaisha kama wote kwenye List of Shame watajivua Gamba, watafikishwa mhakamani, na Fedha na Rasilimali zetu zitarejeshwa. Vinginevyo ngoma ndiyo inaanza. Usijidanganye. Kwa taarifa yako, hakuna anayesukumwa na uchu wa madaraka. 2007 hakuna aliyefikiria "uongozi" bali tuisukumwa na uchungu kwa Mama yetu Tanzania kufilisiwa na viongozi wasio na uchungu. Hatudanganyiki tena 'ngo' na propaganda.


Dr Slaa, salaam.

Unapokea mshahara kiasi gani kwa mwezi, na je unatokana na rasili mali za watanzania?

Take home yangu ni Tshs 600,000/mo na pesa hizi zinatokana na fedha a rasilimali za watanzania. Je nami naifilisi nchi yangu? ingekuwa vizuri nijue ili nijivue gamba mapema.
 
Thanks Mkuu kwa kutuletea hii post.
It will go a long way kuwanyamazisha wale doubting Thomases juu ya muelekeo wa chama.
Kimsingi itawafanya wale wapinzani-waandamanaji wakose mada ya kuongea hadharani-maana hawana sera wala mikakati ya kuwaendeleaza waTz, zaidi ya kukodolea macho kiti cha Urais.
pole kaka, wanachofanya chama cha magamba ni usanii kama kweli wapo serious hao mapacha watatu wanatakiwa wawepo kizuizini huko kwenye vijiji vyao kama alivyo fanya Mwl. J.K Nyerere miaka ile ya sabina na themanini Vinginevyo J.K anapaka rangi upepo.
 
Dr Slaa, salaam.

Unapokea mshahara kiasi gani kwa mwezi, na je unatokana na rasili mali za watanzania?

Take home yangu ni Tshs 600,000/mo na pesa hizi zinatokana na fedha a rasilimali za watanzania. Je nami
naifilisi nchi yangu? ingekuwa vizuri nijue ili nijivue gamba
mapema.
Haya maswali mengine kiboko, mkuu ushasema mshahara kwa maana umeufanyia kazi, umeutolea jasho lako tofauti na wale wanaokwapua hela kutoka kwenye taasisi za umma mfano EPA.
 
Tafiti zilizofanyika hadi sasa kwa kuhusisha wananchi wa kada ya chini na wale wa kipato cha kati zinaonyesha chuki iliyojengeka dhidi ya vinara wa ufisadi ni kubwa sana na imehusishwa moja kwa moja na ccm. Kujivua gamba kwa ccm kuna nia mbili, kwanza ni kurudisha mwamko wa watu juu ya chama ambacho kimepoteza dira miongoni mwa wananchi, na pili katika hali ya kuuma na kupuliza kujaribu kuhamisha chuki juu ya ufisadi kama chama na kuipeleka chuki hiyo kwa walengwa wachache!

Kwa mantiki hii gamba halitang'oka ng'o, maana gamba ndio chama chenyewe, unless otherwise ccm imeguke kwa kupembua mafisadi out of the party waunde chama chao na wazalendo wa kweli wawe na chama chao.

CCM kama ilivyo sasa inategemea mafisadi kwa asilimia 88, na asilimia 11 ruzuku toka serikalini. Michango ya wanachama ni chini ya asilimia 1, hivyo ukiondoa mafisadi wote then ccm is dead, labda tena labda izaliwe upya bila the Mnauyes, the Makambas, the Nchimbis and so on and so forth.
 
Kama anachosema Nape ndio msimamo wa chama...mbona juzi alisita na akamrushia mpira Msekwa kuhusu kuwapa barua mafisadi? kama ilivyoandikwa kwenye NIPASHE? kwa hio huo ndio msimamo wa CCM wa kushindwa kutaja?
 
Uvivu umetuzidi wa tz angalia kenya wamefuta moi day..back to the point nadhani tungesherehekea kifo cha tanganyika na sio uhuru wa tanzania


Hivi Tanzania iliwahi kuwa koloni la nchi gani hata isherehekee miaka 50 ya uhuru wake? Ninachojua mimi ni Tanganyika ndio inasherehekea miaka 50 ya uhuru, Lakini , huyu Tanganyika yuko wapi? Kuna maana kusherehekea uhuru wa nchi ambayo kimsingi hai-exist?
 
NAPE & Co nashindwa kuwaelewa. Siasa zenu hazijifafanui vizuri - kama mnawakilisha matakwa / mnatetea maslahi ya chama au taifa.
Chama chenu kimeshika dola, na kwenye dola kuna sheria zake ambazo lazima zifatwe na kuheshimiwa. Inakuwaje nyie chama tawala mnawajua majizi na wabakaji wa uchumi wetu pasi na kuwachukulia sheria?
NAPE & Co mko 'limited' na nini?
 
Wewe unachanganya sana mambo. Politics ni perception, Chana kuwachukulia hatua ya nidhamu hakihitaji ushahidi wa mahakamani .majuzi dr Slaa alimwachisha kazi Katibu wa Chadema wa wilaya ya nzega, alihukumiwa mahakamani ya wapi? Hao mnaowaita mapacha watatu waliopewa siku 90 waliwahi kuwa viongozi wa ngazi ya juu katika chana na serikali kwa muda murefu ms pamoja na matatizo waliyo mayo kuna heshima wanayostahili.

Sielewi kwa mini mnaona kuwapa siku 90 ni jambo la ajabu. Wenye tuhuma zenye ushahidi wa kimahakama wako mahakamani. Wenye zinazowakera jamii Chana kina haki ya kuwawajibisha bila kusubiri mahakamani. Kinachonishangaza ni cdm kuwatetea licha ya kuwasema kola kukicha kwenye majukwaa. Kama sasa wamekuwa Mali wachukueni vinginevyo miscue unafiki milele.
 
RAIS Jakaya Kikwete amesema amepata moyo mpya wa kuendeleza kazi ya kujivua gamba na yeye na wenzake watajitahidi kuifanya kazi hiyo kwa haki bila kumwonea mtu.

Alisema alitangaza tangu Februari mwaka huu kuwa CCM itajivua gamba na sasa wameanza kuifanya kazi hiyo ingawa watu wengine wameanza kumtupia lawama Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye aliyekuwepo katika tamasha hilo.

Kabla ya kutoa kauli hiyo katika Tamasha hilo la Pasaka, lililofanyika mjini Dar es Salaam, Askofu wa Kanisa la Assemblies of God Tanzania (TAG) Onesmo Ndegi, alisema hatua ya kujivua gamba inayochukuliwa na CCM chini ya Mwenyekiti wake, Rais Kikwete ina mkono wa Mungu.

Askofu Ndegi alisema sherehe za Pasaka mwaka huu ni maalumu kwa kuwa ni mwaka ambao Tanzania itaadhimisha miaka 50 tangu Uhuru ambayo katika Ukristo inaitwa Jubilee na maana yake ni kuweka kitu huru ama kukiondoa katika mateso.

Alisema kutokana na hali hiyo, Mungu amempa ujasiri Rais Kikwete wa kujivua gamba, kitendo ambacho CCM ilikianza hivi karibuni kwa kuwaondoa madarakani baadhi ya viongozi wake wa juu.

Ujasiri wa Rais wetu ni ujasiri aliopewa na Mwenyezi Mungu pamoja na dua tunazomwombea, tunaomba kujivua gamba huko kuwe kwa ukweli na kusiishie hapo tu, alisema Askofu Ndegi.

Baada ya kumaliza kusema hayo, Askofu huyo aliomba maaskofu wengine waliokuwepo ukumbini kumwekea mikono Rais sehemu waliko na kumwombea dua ya kumpa ulinzi, ujasiri na hekina katika uongozi wake.

Lakini Rais Kikwete pia alisisitiza umuhimu wa kudumisha amani nchini na kuwataka wananchi kuvumiliana baina ya watu wa dini mbalimbali na kutowasikiliza watu wanaohubiri habari za udini kwa lengo la kutaka kuleta mafarakano nchini.

Tamasha hilo ambalo Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi, lililenga kuchangisha fedha za kusaidia yatima, watu wenye ulemavu na mahitaji kwa wanawake wasiojiweza.


Source: Gazeti la Habari Leo, April 25, 2011

BRAVO JK!!!
Hahahaha kweli siasa noma kumbe kujivua gamba ni maelekezo ya Mungu! Sawa Askofu tutayaamini maneno yako.Jk ushaombewa usikopeshe fanya kweli.
 
Muhimu ni kurudisha fedha walizokwiba na kutengeneza mfano wengine wasije hata kufikiria kufisadi, kuwatimua chamani pekee haitoshi!
 
Lakini kwa nini JK asiseme fulani na fulani hawatakiwi kwenye chama. Full stop. Wht beat around the bush? Hivi Nyerere angemungunya maneno katika hili?

Ujasiri huo atautoa wapi?
Nyerere alikua kidume bana angeshafumulia mbali huu uchafu wa wanao jiita mapacha watatu .
Lakini kwa sasa hawa mapacha watatu ni zaidi ya roho kwa CCM labda wawaombe watupige changa la macho lakini sio kwa kwa nguvu ya kina Nape,kikwete na vidagaa vingine.

Hivi mkuu umesahau huyu ndiyo yule wa :_ORODHA YA WAUZA MADAWA YA KULEVYA NINAYO ,ORODHA YA MAJAMBAWAZI NINAYO Hawa wote aliwafanya nini ?
NA SASA ANAKUJA NA KUFUA MAGAMBA WATU UNATEGEMEA KUNA HATUA ZA KIJASIRI ZITACHUKULIWA HAPO?
LABDA WALE WACHEZA NGOMA KULE MSOGA NA BAGAMOYO.
 
Back
Top Bottom