JK: Anachosema Nape ndio msimamo wa chama

JK: Anachosema Nape ndio msimamo wa chama

Mlengo wa Kati

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2011
Posts
2,730
Reaction score
492
Rais Jakaya Kikwete jana kaweka wazi kuwa Anachosema Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kuhusu mapacha watatu kutimuliwa kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa kwa Tuhuma ya Ufisadi ndio Msimamo wa Chama na CCM haina Mchezo kwa hilo na akaongeza Wananchi watarajie kuona mambo makubwa juu ya Vita ya Ufisadi!

Alisema sasa ni wakati wa Kurejesha Maadili ndani ya Chama.
 
RAIS Jakaya Kikwete amesema amepata moyo mpya wa kuendeleza kazi ya kujivua gamba na yeye na wenzake watajitahidi kuifanya kazi hiyo kwa haki bila kumwonea mtu.

Alisema alitangaza tangu Februari mwaka huu kuwa CCM itajivua gamba na sasa wameanza kuifanya kazi hiyo ingawa watu wengine wameanza kumtupia lawama Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye aliyekuwepo katika tamasha hilo.

Kabla ya kutoa kauli hiyo katika Tamasha hilo la Pasaka, lililofanyika mjini Dar es Salaam, Askofu wa Kanisa la Assemblies of God Tanzania (TAG) Onesmo Ndegi, alisema hatua ya kujivua gamba inayochukuliwa na CCM chini ya Mwenyekiti wake, Rais Kikwete ina mkono wa Mungu.

Askofu Ndegi alisema sherehe za Pasaka mwaka huu ni maalumu kwa kuwa ni mwaka ambao Tanzania itaadhimisha miaka 50 tangu Uhuru ambayo katika Ukristo inaitwa Jubilee na maana yake ni kuweka kitu huru ama kukiondoa katika mateso.

Alisema kutokana na hali hiyo, Mungu amempa ujasiri Rais Kikwete wa kujivua gamba, kitendo ambacho CCM ilikianza hivi karibuni kwa kuwaondoa madarakani baadhi ya viongozi wake wa juu.

“Ujasiri wa Rais wetu ni ujasiri aliopewa na Mwenyezi Mungu pamoja na dua tunazomwombea, tunaomba kujivua gamba huko kuwe kwa ukweli na kusiishie hapo tu,” alisema Askofu Ndegi.

Baada ya kumaliza kusema hayo, Askofu huyo aliomba maaskofu wengine waliokuwepo ukumbini kumwekea mikono Rais sehemu waliko na kumwombea dua ya kumpa ulinzi, ujasiri na hekina katika uongozi wake.

Lakini Rais Kikwete pia alisisitiza umuhimu wa kudumisha amani nchini na kuwataka wananchi kuvumiliana baina ya watu wa dini mbalimbali na kutowasikiliza watu wanaohubiri habari za udini kwa lengo la kutaka kuleta mafarakano nchini.

Tamasha hilo ambalo Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi, lililenga kuchangisha fedha za kusaidia yatima, watu wenye ulemavu na mahitaji kwa wanawake wasiojiweza.

Source: Gazeti la Habari Leo, April 25, 2011

BRAVO JK!!!
 
Mimi nauliza katika hao mapacha yeye JK atakosa kweliii!?
 
Lakini kwa nini JK asiseme fulani na fulani hawatakiwi kwenye chama. Full stop. Wht beat around the bush? Hivi Nyerere angemungunya maneno katika hili?
 
Usanii mtupu. Wala hathubutu kuwataja maana anajua nae ni mmoja wao
 
Lakini kwa nini JK asiseme fulani na fulani hawatakiwi kwenye chama. Full stop. Wht beat around the bush? Hivi Nyerere angemungunya maneno katika hili?

Nashukuru sana! sijui anamsibiri nani kuchukua hatua!
 
Rais Jakaya Kikwete jana kaweka wazi kuwa Anachosema Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kuhusu mapacha watatu kutimuliwa kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa kwa Tuhuma ya Ufisadi ndio Msimamo wa Chama na CCM haina Mchezo kwa hilo na akaongeza Wananchi watarajie kuona mambo makubwa juu ya Vita ya Ufisadi!

Alisema sasa ni wakati wa Kurejesha Maadili ndani ya Chama.

Thanks Mkuu kwa kutuletea hii post.
It will go a long way kuwanyamazisha wale doubting Thomases juu ya muelekeo wa chama.
Kimsingi itawafanya wale wapinzani-waandamanaji wakose mada ya kuongea hadharani-maana hawana sera wala mikakati ya kuwaendeleaza waTz, zaidi ya kukodolea macho kiti cha Urais.
 
haya sasa yetu macho alafu waje wamgeuke na zaidi ni kwamba awatoe kadi za chama
 
Rais Jakaya Kikwete jana kaweka wazi kuwa Anachosema Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kuhusu mapacha watatu kutimuliwa kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa kwa Tuhuma ya Ufisadi ndio Msimamo wa Chama na CCM haina Mchezo kwa hilo na akaongeza Wananchi watarajie kuona mambo makubwa juu ya Vita ya Ufisadi!

Alisema sasa ni wakati wa Kurejesha Maadili ndani ya Chama.

mbona habari ya habari leo na yako ni Vitu viwili tofauti, Habari leo hawakumnukuu JK anasema anachofanya NAPE ni msimamo wa chama, naona mzee unafanya spinning kweli
 
Sijali cha habari Leo au cha nani lakini Kama mpenda nchi Nadhani Huu ni wakati muafaka kuhakikisha wenye ushahidi kwa mafisadi wawatangaze ili washughulikiwe sidhani Kama wako watatu tu tuache kuzungumza ya jana. Na bwana Executive Kama isingekuwa msimamo wao CCM si bwana mkubwa angempinga Nape ? Au kumwambia Kama Magufuli slow down. Mimi Nadhani ujasiri Wa Nape unatoka kwa JK
Remember there is no permanent friend in politics.....
 
HabariLeo acheni uhuni fanya kazi sio usanii kana kwamba shule yenu ni finyu na hamwezi kujitegemea, andika kile alichokisema rais sio mawazo yenu.
 
Lakini kwa nini JK asiseme fulani na fulani hawatakiwi kwenye chama. Full stop. Wht beat around the bush? Hivi Nyerere angemungunya maneno katika hili?

Mbona kila Mtanzania anawajua Nape alisha wataja Lowassa,Rostam na Chenge au mpaka JK awataje nae?!
 
mbona habari ya habari leo na yako ni Vitu viwili tofauti, Habari leo hawakumnukuu JK anasema anachofanya NAPE ni msimamo wa chama, naona mzee unafanya spinning kweli

Aliongea jana kwenye Tamasha sio Gazeti la habari leo!
 
Hivi Tanzania iliwahi kuwa koloni la nchi gani hata isherehekee miaka 50 ya uhuru wake? Ninachojua mimi ni Tanganyika ndio inasherehekea miaka 50 ya uhuru, Lakini , huyu Tanganyika yuko wapi? Kuna maana kusherehekea uhuru wa nchi ambayo kimsingi hai-exist?
 
Thanks Mkuu kwa kutuletea hii post.
It will go a long way kuwanyamazisha wale doubting Thomases juu ya muelekeo wa chama.
Kimsingi itawafanya wale wapinzani-waandamanaji wakose mada ya kuongea hadharani-maana hawana sera wala mikakati ya kuwaendeleaza waTz, zaidi ya kukodolea macho kiti cha Urais.

Watakosaje cha kusema,sana sana watawashukuru kwa kujiona ccm ni mafisadi, dhana waliyokuwa wakiikataa muda mwingi. Maana hao mafisadi walisemwa zamani 2007 na wala siyo leo 2011; na ccm walikataa kata kata. Sasa mkuu hapa mshindi atakuwa nani?? CDM au CCM?? Tegemea kwa kuwa mtaondoa mafisadi wachache, CDM wataendelea kudai na wale waliojificha nao wajisafishe-hapo sasa patakuwa patamu!! Kusema kuwa waandamanaji watakosa cha kusema -ni kujidanganya, kwa kuwa hoja hii ccm wanadandia na hivyo wataendelea kudandia kila kitakachoibushwa baada ya hapo. UTAKUMBUKA UTABIRI HUU WANGU!
 
Only in Tanzania mwizi na mbadhirifu wa mali ya umma anapewa siku tisini aachie madaraka chamani lakini aendelee kuwa mbunge, mwenyekiti wa kamati badala ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Hii nchi inatia kichefu chefu kwa kweli hivi tuna utawala wa sheria ama ndio ukifika kwa viongozi waandamizi wa ccm sheria zinapuuzwa?
Alafu kinachonishangaza ni kuwa rais katamka hadharani kuwa ccm kuna mafisadi lakini mpaka sasa sijasikia vyombo husika vikiwafikisha mahakamani au kuwachukulia hatua.
 
Back
Top Bottom