Mwalimu
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 1,581
- 1,069
Kabla ya kutoa kauli hiyo katika Tamasha hilo la Pasaka, lililofanyika mjini Dar es Salaam, Askofu wa Kanisa la Assemblies of God Tanzania (TAG) Onesmo Ndegi, alisema hatua ya kujivua gamba inayochukuliwa na CCM chini ya Mwenyekiti wake, Rais Kikwete ina mkono wa Mungu.
Askofu Ndegi alisema sherehe za Pasaka mwaka huu ni maalumu kwa kuwa ni mwaka ambao Tanzania itaadhimisha miaka 50 tangu Uhuru ambayo katika Ukristo inaitwa Jubilee na maana yake ni kuweka kitu huru ama kukiondoa katika mateso.
Alisema kutokana na hali hiyo, Mungu amempa ujasiri Rais Kikwete wa kujivua gamba, kitendo ambacho CCM ilikianza hivi karibuni kwa kuwaondoa madarakani baadhi ya viongozi wake wa juu.
Source: Gazeti la Habari Leo, April 25, 2011
BRAVO JK!!!
Onesmo Ndegi sio askofu wa TAG, yeye ni mchungaji wa kanisa la Living Waters Ministry....