JK: Anachosema Nape ndio msimamo wa chama

JK: Anachosema Nape ndio msimamo wa chama

Wakuu zangu kuna maswala mawili hapa na lazima tuwe makini sana na jinsi tunavyotazama picha nzima ya mgogoro huu wa Mafisadi.

Kwanza kabisa kwa MASLAHI ya TAIFA hawa mafisadi ni lazima wapoteze mamlaka waliyonayo iwe ndani ya chama au nje kwa sababu ya kinga ya chama tawala chini ya mfumo dume, hivyo kuondoka kwao ni muhimu kwetu sote ili wananchi wapate uwezo wa hata kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizopo juu ya hawa mafisadi..Pasipo wao kutolewa hatutakuwa tumefanikisha lolote ndani ya ushabiki huu ya kuitaka CCM isambaratike..

Pili, pamoja na kwamba JK amechelewa kuchukua hatua dhidi ya hawa mafisadi maswahiba wake bado anastahili kupewa motisha ya kumwezesha kuondoa uvivu wa akili ulomkumba baada ya kuchukua madaraka na tukumbuke tu kwamba JK analindwa na katiba dhidi ya machafu yote aloyafanya akiwa rais wa nchi, hivyo hao RACHEL hawawezi kumweka hatiani hata kama wakitafuta njia za kulipa kisasi kwa sababu ni hadi wapate nafasi ya kufanya hivyo..

Nguvu ya dola ni zaidi ya RACHEL, na mamlaka alokabidhiwa JK yanazidi uwezo wa chombo chochote nchini kudhibiti mtu au kundi la watu wanaotaka kuhatarisha usalama wa nchi yetu. In the name of National security, hao kina RACHEL wanaweza kupotezwa ama kulindwa na hakuna chombo wala chma cha kisiasa kinachoweza kupindua..kwa hiyo tunapowapa nguvu hawa mafisadi kwa saabu ya kuipinga CCM na utawala wa JK inanishinda sana kuelewa haswa sisi Wadanganyika tunataka nini?..

Na laukama tunachotaka ni hawa mafisadi kufikishwa mahakamani, nadhani CDM na vyama vinginevyo vijaribu kukusanya mashtaka ambayo kisheria yatatuwezesha kuwafikisha mahakamani kwa ushahidi ambao CCM wanaukalia au hawana kweli..sidhani kama ni jukumu la JK na CCM kuwafikisha RACHEL mahakamani lakini ni jukumu la chama kufanya mageuzi haya ikiwa hawa watu ni mwiba kwa maendeleo ya chama.

Wakuu zangu tumeona madudu mengi yakifanywa na tawala zilizopita, Ufisadi umekuwa ni desturi na maisha ya Mtanzania kiasi kwamba ni lazima tuwe na sehemu ya kuanzia na jitihada hizo zipongezwe. Binafsi sioni sababu ya JK kujivua gamba ikiwa yeye mwenyewe anakubali kutumiwa na kundi hilo lakini maadam leo hii amefikia maamuzi ya kuwatema basi tumpe nguvu ya kufanya haya ili tupate kusonga mbele badala ya kulalamika na kuhoji dhumuni la JK na CCM kuchukua hatua hii hali tunajua wazi CCM wanahitaji kuchukua maamuzi magumu kama haya kukiwezesha chama kushindana..

CDM wana muda na nafasi kubwa ya kuendeleza vagi hili hasa baada ya hawa Mafisadi kuondolewa ndani ya uongozi wa chama. CDM na vyama vinginevyo wanaweza kuwavua ubunge na hata kuwafikisha mahakamani maadam kinga hii itaondolewa. Again, navyofahamu mimi ushahidi wa kujitetea wa hawa Mafisadi hauwezi kukubalika mahakamani ikiwa utamhusisha rais kwa sababu JK analindwa na katiba..For the national security, hawa watu wanatakiwa kuondolewa haraka iwezekanavyo na sintoshangaa wakiwa Kolimbared!
 
Wananchi hawaangalii nyoka kujivua gamba!!wanataka mabadiliko katika maisha yao,wanataka unafuu ili wajue kweli mambo yamebadilika
 
Lakini kwa nini JK asiseme fulani na fulani hawatakiwi kwenye chama. Full stop. Wht beat around the bush? Hivi Nyerere angemungunya maneno katika hili?

Hana ubavu huo kwa sababu anajua hao anaowataka waondoke walifanya naye madudu ya hali ya juu katika kuhakikisha anakuwa mgombea wa CCM. Hivyo walikusanya mabilioni ya shilingi kutoka kwa mafisadi mbali mbali nchini ili kuhonga wajumbe waliopiga kura kumchagua mgombea wa CCM na pia pesa hizo zilitumika kumchafua SAS. Mweka hazina wa mabilioni hayo alikuwa Rostam na si ajabu ana rekodi zote ya kile kilichojiri.

Sasa kama Lowassa, Rostam na Chenge wakiamua kuanika madudu hayo ya wana mtandao kwa Watanzania sidhani Kikwete ataendelea kuwa Rais na si ajabu wakati wa sherehe za miaka 50 ya uhuru wetu tukawa na Acting President. Kwa hiyo sasa hivi roho inamwenda mbio akijua wazi kwamba ahueni yake ni Lowassa, Rostam na Chenge kuondoka kimya kimya vinginevyo awamu yake ya pili iko katika mashaka makubwa sana.
 
Nsimba,
Na "kichwa" nacho kina siku 90 kujivua Gamba. Ajenda ya Ufisadi itaisha kama wote kwenye List of Shame watajivua Gamba, watafikishwa mhakamani, na Fedha na Rasilimali zetu zitarejeshwa. Vinginevyo ngoma ndiyo inaanza. Usijidanganye. Kwa taarifa yako, hakuna anayesukumwa na uchu wa madaraka. 2007 hakuna aliyefikiria "uongozi" bali tuisukumwa na uchungu kwa Mama yetu Tanzania kufilisiwa na viongozi wasio na uchungu. Hatudanganyiki tena 'ngo' na propaganda.

Mzee Slaa la Uchu wa Madaraka limeonekana kule Arusha kuhusu Umeya! Lakini swali langu kwako Dr Slaa na Chadema hivi kama Dr slaa una ushahidi wa Kutosha kuhusu mafisadi kwanini wewe na Chadema msiwafungulie kesi mafisadi mahakamani? Kwanini tusubiri serikali iwapelekke mahakamni wakati wewe una Ushahidi wa kutosha? Hii inatoa picha ya kuona mtu anaiba sehemu lakini mpita njia unasema atajijua mwenye mali! Mi naona ni muda muafaka kwa Chadema iwapeleke watuhumiwa hao mahakamani na sio kusbiri JK ndio awapeleke! Mbona kuhusu Dowans wanaharakati walifungua kesi kupinga isilipwe,hapa kigugumizi kinatoka wapi? Au hakuna ukweli ni siasa za maji taka? Chadema msiwapofushe Watanzania kama CCM inavyo fanya! Au Watanzania tuendelee kusubiri chama cha Ukombozi wa Ukweli ambacho bado hakija anzishwa!
 
Thanks Mkuu kwa kutuletea hii post.
It will go a long way kuwanyamazisha wale doubting Thomases juu ya muelekeo wa chama.
Kimsingi itawafanya wale wapinzani-waandamanaji wakose mada ya kuongea hadharani-maana hawana sera wala mikakati ya kuwaendeleaza waTz, zaidi ya kukodolea macho kiti cha Urais.

Bahati mbaya sana kugawana mbao za duka lililofilisika huishia kung'oana mapua. Nina wasiwasi sana kama kweli zoezi hili lina maandalizi ya kutosha. Tusubiri kidogo tu kwani hata hizo siku 90 zinaweza zifike kabla watu hawajaoteshana manundu na kuwekana pabaya.
 
Dah,hii style ya jk kiboko.yeye haongei wanaongea wengine mnakumbuka mkutaö wa vijana pale pwani ?ilikua intro watu wakapuuzia na ikatokea.hivi sa watu wanamponda Nape lakini ndichosa kitatokea na wengi wataachwa midomo wazi.WAIT AND SEE

Anakwepa lawama alifanya hivi kwa Kombani na mwanasheria mkuu kuhusu mambo ya Katiba. Alivyoona wananchi wamechacharuka akaja kivyake. Nnape watch your back! Huyu mtu sio mtu wakumwamini kabisa anaweza akabadili mwelekeo wakati wowote ukabaki kituko.
 
Mzee Slaa la Uchu wa Madaraka limeonekana kule Arusha kuhusu Umeya! Lakini swali langu kwako Dr Slaa na Chadema hivi kama Dr slaa una ushahidi wa Kutosha kuhusu mafisadi kwanini wewe na Chadema msiwafungulie kesi mafisadi mahakamani? Kwanini tusubiri serikali iwapelekke mahakamni wakati wewe una Ushahidi wa kutosha? Hii inatoa picha ya kuona mtu anaiba sehemu lakini mpita njia unasema atajijua mwenye mali! Mi naona ni muda muafaka kwa Chadema iwapeleke watuhumiwa hao mahakamani na sio kusbiri JK ndio awapeleke! Mbona kuhusu Dowans wanaharakati walifungua kesi kupinga isilipwe,hapa kigugumizi kinatoka wapi? Au hakuna ukweli ni siasa za maji taka? Chadema msiwapofushe Watanzania kama CCM inavyo fanya! Au Watanzania tuendelee kusubiri chama cha Ukombozi wa Ukweli ambacho bado hakija anzishwa!

Hivi kwanini it is all about CDM vs CCM. Kwanini wananchi hatuwezi kujiuliza maswali ya msingi bila kulewa haya maji ya bendera? Tungetanguliza utaifa kwanza wala tusingefika hapa tulipo. Mimi sina chama, lakini naelewa kabisha viongozi walioko madarakani hawawezi kazi. Inawezekana kuna watu walioko ndani ya CCM wenye uchungu na taifa lakini wanauoga wakukosao, pia kuna walioko CDM ambao wana matatizo. Lakini sisi kama wananchi tuna-soln gani kwa umaskini tulionao?? Kumbeza Slaa haitatusaidia whether anachosema ni kweli au sio kweli kwasababu hana position yeyote kwenye serikali. Kuipigia serikali kelele itasaidia kwasababu wao ndio wameshikilia all the resources. Unapompa mtu pesa kwaajili ya shughuli fulani halafu huoni kazi iliyofanyika hilo ni tatizo tena kubwa!
 
Haya maswali mengine kiboko, mkuu ushasema mshahara kwa maana umeufanyia kazi, umeutolea jasho lako tofauti na wale wanaokwapua hela kutoka kwenye taasisi za umma mfano EPA.

hivi híi EPA is it not just a case of taking a loan and not paying back?
Just a bad payment of debt payment i mean some peoples took that money in form of loan with document to prove that only they didnt pay back .what do you do when someone took a loan and dont pay back?what is the rule?worse still the EPA fund was foregner .am a little bit confused here.just what the hell is EPA?
 
[
Alisema alitangaza tangu Februari mwaka huu kuwa CCM itajivua gamba na sasa wameanza kuifanya kazi hiyo ingawa watu wengine wameanza kumtupia lawama Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye aliyekuwepo katika tamasha hilo.

Nimekuwa natatizwa na huu msemo wa CCM kujivua gamba na nimeona watu wengi wetu tumekuwa tunasema tu labda bila kujua kwa nini "nyoka" wanapoteza ngozi asililia na kuvaa ngozi mpya. Soma hapa chini

"The skin of snakes is often a point of curiosity among those who observe them. Unlike many other animals, snakes shed their skin on a periodic basis. While other creatures may simply shed skin cells or hair, a snake actually rids itself of its skin in one continuous piece, a procedure that can be likened to removing a sock. This shedding is not without purpose. Snakes shed their skin to allow for growth, as well as to remove parasites along with their old skin.

Snakes shed their skin by brushing against something hard and rough, like a rock, and creating a rip in their skin. Usually, this rip is initiated in the nose and mouth area. A snake continues to work on this rip until it can shed its skin completely. Snakes shed their skin rather frequently. Many snakes shed more than once per year with some species shedding on a bi-monthly basis.

Snakes shed when they grow too big for their skin, comparable to the way humans outgrow clothing. Humans shed skin cells too. However, instead of losing skin cells as one continuous and noticeable piece, humans lose numerous, tiny skin cells each day. No one really notices this shedding, as human skin cells are small enough to escape observation.

Interestingly, snakes shed their old skin when their new skin is formed beneath it. The new skin has the same patterns and colors as the old skin that is ready for shedding. When the old skin is shed, however, it doesn’t look exactly the same as its replacement. It takes on a nearly transparent appearance".

Ninaomba ndugu zangu mnisaidie katika hili, CCM wanavyosema wanajivua gamba WANAMAANISHA KITU GANI. Hawa maaskofu nao wanadandia tu vitu bila kuchambua, nimesikitika sana
 
hivi híi EPA is it not just a case of taking a loan and not paying back?
Just a bad payment of debt payment i mean some peoples took that money in form of loan with document to prove that only they didnt pay back .what do you do when someone took a loan and dont pay back?what is the rule?worse still the EPA fund was foregner .am a little bit confused here.just what the hell is EPA?
Mkuu labda ifuatilie barua ya Lipumba kwenda IMF utaelewa kilichofanyika.. bofya hapa
 
Yeyote aliye na uchungu na nchi hii na akawa na evidence atapeleka kesi mahakamani badala ya kutuletea abdacadabra lukuki.
Na kuhusu kujivua gamba sisiem hilo ni suala lao sisiem how does it relate to CDM.Ni suala la wenyewe wameamua ivo wawatoe jamaa hata kama hamna evidence ya kuwapeleka kwa plato .sasa nashindwa kuelea vyama kama cdm wameshupaa kuliöngelea ka vile wana share sisiem.
Kikubwa hapa hebu cdm pelekeni kesi mahakamani dunia imebadilika rais haezi weka mtu kizuizini kwa pressure za kisiasa naye si mwendesha mashitaka.sisiem wamefanya uamuzi wa kisiasa kwa manufaa yao kujivua gamba kukifaniwa ni tishio kwa cdm ndo maana ghafla cdm wamegeuka kuwaunga mkono watu ambao kila kukicha waliku wakiwasema hell i cant stand turncoats
 
Changanya changanya hadi mchanganyikiwe, mkiwaacha tutasema mnafuga mafisadi mkiwatoa tunawatetea mmewaonea siyo watatu tu yaani hadi raha hapo mmemeza ndoano dawa siyo kuivuta, na kwa kizungu wanasema a square peg in a round hole.
 
RAIS Jakaya Kikwete amesema amepata moyo mpya wa kuendeleza kazi ya kujivua gamba na yeye na wenzake watajitahidi kuifanya kazi hiyo kwa haki bila kumwonea mtu.
 
Chadema wameamua kutoa jina la sumaye kwa vile ameomba kujiunga na chama hicho kikubwa cha siasa kinachoendana na jina lake.
Mbona umekimbia swali kajibu kwanza kule watu wanasubiri data za Sumaye kujiunga na hicho chama kama ni umbea tuambie.
 
mimi nilishasema haya magamba ni mchezo wa JK hakuna kitu, uwezi kung'oa msingi wako mwenye,
yeye ana mpango wa kuwalipa nini hao RACHEL wakifunguliwa kesi na kwenda jela,

KAMA RACHEL watafukuzwa ndani ya chama baada ya hizi siku 80, next move ni serikali kuwashitaki, maana kama chama kitawafukuza ina maana kina ushahidi kwamba wameiba, na hapo bila kuwapeleka mahakamani hakuna kitu watakachokua wamefanya, ili kurudisha hiyo imani kutoka kwa wananchi
na kama wakiwasimamisha mahakamani JK hata wafungaje midomo hawa RACHEL wasimtaje kwamba walimuweka wao madarakani? kwa huo wizi wa EPA!!!!!!
mimi nachokiona ni kesi itakayopigwa kalenda mahakamani mpaka tutachoka na JK atamaliza miaka yake mitano bila bubhuza, na kama hakuna umakini huu ni mtaji utakao warudisha ccm madaraka 2015 kwa kudanganya watu mafisadi wanakesa mahakamani, kumbuka mahakama zetu kwa kupiga stop kesi zake kuripotiwa ndio zenyewe
 
Hivi Tanzania iliwahi kuwa koloni la nchi gani hata isherehekee miaka 50 ya uhuru wake? Ninachojua mimi ni Tanganyika ndio inasherehekea miaka 50 ya uhuru, Lakini , huyu Tanganyika yuko wapi? Kuna maana kusherehekea uhuru wa nchi ambayo kimsingi hai-exist?

Jamhuri ya Tanganyika = Tanzania Bara! Jamhuri ya Watu wa Zanzibar = Zanzibar! Mbona majina ya pande zote mbili yalishabadilika baada ya Muungano ndugu? Kwa hiyo tunasherehekea uhuru wa Tanzania Bara! Majina yasikuchanganye!
 
Ujasiri huo atautoa wapi?
Nyerere alikua kidume bana angeshafumulia mbali huu uchafu wa wanao jiita mapacha watatu .
Lakini kwa sasa hawa mapacha watatu ni zaidi ya roho kwa CCM labda wawaombe watupige changa la macho lakini sio kwa kwa nguvu ya kina Nape,kikwete na vidagaa vingine.

Hivi mkuu umesahau huyu ndiyo yule wa :_ORODHA YA WAUZA MADAWA YA KULEVYA NINAYO ,ORODHA YA MAJAMBAWAZI NINAYO Hawa wote aliwafanya nini ?
NA SASA ANAKUJA NA KUFUA MAGAMBA WATU UNATEGEMEA KUNA HATUA ZA KIJASIRI ZITACHUKULIWA HAPO?
LABDA WALE WACHEZA NGOMA KULE MSOGA NA BAGAMOYO.

hizi ni fikra mgando na kudhani kwamba kila kitu kifanyike nyerere's way. Hoja ya msingi ni hatua zinazochukuliwa na dhamira ya hatua hizo. Suala la RACHEL hatma yake ni hiyo, waanze mbele na kama wana nguvu wakaasisis chama chao halafu washike dola. Hizi harakati za kupita katika nyumba za ibada kupotosha mada au kujifungia na wahariri usiku kucha na kugawa milioni tatu kwa kila mtu haziwezi kuzima huu moto.

Walidhani wangemtenga Nape na maamuzi ya vikao ili aonekane ni mropokaji lakini JK ameweka wazi na sasa hakuna kurudi nyuma. Tunajua akina Laizer wataibuka kupitia gazeti la Mtazania lakini ukweli ni kwamba chama kimeshawa-flush hawa jamaa na wale wanaowapenda wajiunge nao halafu tuone kama kweli wana nguvu za kufanya chochote. Hivi ushahidi unaotakiwa ni nini? Huyu mkubwa wao ana historia hiyo ya kuiba hata fedha za msaada wa mafuriko ya kule kusini miaka ya mwanzoni mwa 1990.
 
Back
Top Bottom