Kuelewa vyeo hivi ni lazima uelewe mtiririko wa mahakama zetu ulivyo..
a. Mahakama za Mwanzo
b. Mahakama za Wilaya
c. Mahakama Maalum (kama Mahakama ya Kazi, Biashara n.k)
d. Mahakama Kuu (ziko kikanda hizi) na hapa pia kuna mtiririko wa Mahakama ya Kuu ya Zanzibar
e. Mahakama ya Rufaa (ndiyo Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano ambapo kesi zote za rufaa iwe Zanzibar, Bara, au Majeshi zinatolewa uamuzi wa mwisho ambao hukumu yake haiwezi kukatiwa rufaa mahali pengine popote).
sasa: Mahakama za Chini zinaongozwa na Mahakimu na wa juu kati yao anakuwa ni Hakimu Mkuu Mkazi (maarufu kati ya mahakama hizo za chini ni hiyo ya Kisutu ingawa mahakama za Hakimu mkazi zipo mikoani vile vile kwa kadiri ninavyojua).
Mahakam Kuu ina majaji wengi na ndiyo chombo ambacho kinasimamia haki na watu wengi wanaujuzi nao katika maswala ya kawaida. Mkuu wa Majaji wa Mahakama Kuu ndiyo anaitwa Jaji Kiongozi, kutoka kwa Jaji kiongozi ndio utakutana sasa na namba za majaji mbalimbali kama tunavyozifahamu.
Kikatiba Majaji wa Mahakama Kuu hawatakiwi kupungua 15!
Majaji wa Mahakama ya Rufaa wako juu ya Majaji wengine kwa hiyo mtu akitoka Ujaji wa Mahakama Kuu (kama Jandu) na akipewa Mahakama ya Rufaa siyo uhamisho tu bali ni kupanda cheo.